Uchaguzi 2020 Hoja za Tundu Lissu Bagamoyo ni mwiba mchungu kwa CCM. CCM inapomjibu Lissu anawasha moto zaidi

Uchaguzi 2020 Hoja za Tundu Lissu Bagamoyo ni mwiba mchungu kwa CCM. CCM inapomjibu Lissu anawasha moto zaidi

GUSSIE

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2014
Posts
3,880
Reaction score
11,134
Mkutano wa Tundu Lissu akiwa Bagamoyo umenikatisha tamaa kwa hoja zake zisizo na majibu bali zinahitaji utekelezaji wa Serikali.

Mosi, Tundu Lissu anasema wananchi wa barabara ya Kimara wengi wamekufa kwa presha baada ya nyumba zao kubomolewa na viongozi wa CCM kupitia mamlaka kuu,Anasisitiza hawakulipwa pesa kosa barabara.

Pili, Tundu Lissu anasisitiza walimu na mapolisi kwa miaka mitano hawajaongezewa kitu chochote ,na wakati wa Mei Mosi hujibiwa kwa kiburi tunajenga barabara.

Tatu, Tundu Lissu amewauliza wananchi hali ya maisha yao na wafanyabiashara wanaonaje,Wananchi wamejibu hali ni ngumu sana

Nne, Anatuhumu kuwa pesa na michango ya Corona imeliwa yote waliyochangisha wana CCM na Mamlaka Kuu. Anasema madaktari na manesi waliahidiwa wakati wa corona kulipwa lakini mpaka sasa hawajalipwa hata senti tano.

Hii ya Bagamoyo leo Tundu Lissu lengo lake ni kumjibu Mama Samia Suluhu kwa hotuba zake Lindi.

Kwa hoja na kauli ngumu kama hizi za Tundu Lissu nani atazijibu?

Mzee Yusuf Makamba amejitokeza leo kujibu lakini utamuonea huruma hana la kujibu wala namna bali kutifurahisha vijana.

Mzee Makamba anasema CCM ndio imejenga uwanja wa Rais Chato na sio Rais kajenga, amesisitiza kuwa Chato ni Tanzania

Mzee Makamba anasema mbuga ya Chato ni ongezeko la vivutio kwani lile pori lilikuwa tupu wanakaa majambazi.

CCM kama chama changu tuache kumjibu huyu mtu majukwaani tuongelee yetu.

Mbona suala la hotuba yake Zanzibar tumekaa kimya na yeye mwenyewe kapotezea, tungejibu ishu ya Zanzibar angetupa taabu sana.
 
Mbona ishu ya hotuba yake zanzibar tumekaa kimya na yeye mwenyewe kapotezea,Tungejibu ishu ya zanzibar angetupa taabu sana
Kuntu

Mzee Yusuf Makamba amejitokeza leo kujibu
Huyualiyepewa onyo kali na John baada ya kulalamika kuwa anatukanwa na Musiba amejitokeza leo? Hivi anamdanganya nani huyu mzee kwamba anampenda John?

Daah! Kweli Lisu kiboko.
 
bongomagazinetz_20200910_8.jpg

Sawa Bwashehe.....CCM can not waste her time to answer somebody shit, kazi yao ni moja tuu, kuwafikia wapiga kura walipo na kuwatatulia shida zao ..... Hakuna impact yyte ya sera Kwa mda uliobaki... Ni kushikilia ulicho nacho
 
View attachment 1565570

Ulimuona mzee Yusufu Makamba leo? Alijaribu kumsugua mtu kwa jiki.
 
Mkuu, subiri kwenye sanduku ndo utajuwa ulikuwa ni mwiba au kijiti cha nyasi. Na kwa kupitia ndo utaona kama CHADEMA ulikuwa na mgombea wenye faida au kakiingiza chama mkenge? Stay tuned uchaguzi uishe na Magu aapishwe ndo utaikumbuka comment hii.
 
View attachment 1565570
Sawa Bwashehe.....CCM can not waste her time to answer somebody shit, kazi yao ni moja tuu, kuwafikia wapiga kura walipo na kuwatatulia shida zao ..... Hakuna impact yyte ya sera Kwa mda uliobaki... Ni kushikilia ulicho nacho

..hizo landcruiser thamani yake siyo sawa na zahanati huko vijijini?

..kwa haraka nimehesabu kama landcruiser tisa.

..viongozi wa kiafrika ni makatili sana.

cc Kilatha
 
..hizo landcruiser thamani yake siyo sawa na zahanati huko vijijini?

..kwa haraka nimehesabu kama landcruiser tisa.

..viongozi wa kiafrika ni makatili sana.

cc Kilatha
Zahanati takriban 300 zimejengwa nchi nzima with in 5 yrs , rekodi ya kipekee Sana , wakat kikwete alijenga zahanati 150 Kwa mda wa miaka kumi, zahanati hzo zinasubir watumishi wa afya waajiliwe mwaka ujao wa fedha
 
..hongereni.

..wananchi wanazihitaji kwasababu wanakula mlo mmoja kwa siku.
 
View attachment 1565570
Sawa Bwashehe.....CCM can not waste her time to answer somebody shit, kazi yao ni moja tuu, kuwafikia wapiga kura walipo na kuwatatulia shida zao ..... Hakuna impact yyte ya sera Kwa mda uliobaki... Ni kushikilia ulicho nacho
Wote hao mifukoni uchumi umekauka hivyo Magu ajiandae.
 
Back
Top Bottom