Hoja za Utanganyika na Uzanzibari ni Hoja Muflis za Ujinga wa Ukosefu Elimu ya Uraia. Tuwatoe Ujinga Huu Kwa Elimu ya Uraia au Tuwaache na Ujinga Wao?

Huna hoja mkuu Zanzibar ina ukubwa wa wilaya mbili za huku bara, hicho kinachopelekwa huko kimeanza kwenda jana au juzi?.

Unapalilia chuki na madhara yake yanaweza kabisa kuja kuwa sumu kama sio leo basi hata muongo mmoja ujao.
Tunayosema hapa ni mageni?
Maalimu Seif kayasema hadi anaingia kaburini
OMO, Jussa, Duni wanayasema kila siku achiia mbali walioko mitandaoni
Wazanzibar wanamlaani Nyerere '' Lanatullah' aliyeleta Muungano kila siku. Mbona hutkuwahi kukisikia
Wazanzibar ndio wamerudisha Utanganyika tena kwa jina

Mbona hatukwahi kusikia ukikemea?

Kuhusu Ukubwa wa Zanzibar, nitajie Wilaya moja mja tu ya Bara yenye Mbunge aliyechaguliwa na watu 3,300!
Tupe SqKM za Zanzibar halafu tafuta Wilaya moja tu ulinganishe
 
Rasilimali zinatolewa kila eneo la Tanzania cha muhimu tuongeze pato la taifa ili na zenyewe ziongezeke kwa wingi wake.

Bado haujanishawishi kuachana na visiwa hivi kwa hoja za mgao wa kinachopatikana hapa Tanzania. Ukikaa na mzenji atakuja na mawazo tofauti yenye kudhani kuwa mtu wa bara anamuonea mzenji.

Ni hisia binafsi za kila mtu kadri ya uelewa wake. Muungano ni muhimu kuliko chochote. USA wana miaka 247 ya uwepo wao na ni kwa sababu ya umoja wao.

Hata kama jimbo la Los Angeles linazalisha mara tano zaidi ya jimbo la Mississipi wanaendelea kuwa pamoja wakijua kuwa ule umoja wao ndio silaha yao muhimu dhidi ya kina Russia na China.
 
Ningekuwa na uwezo visiwa hivi ningevisogeza mbali kabisa kutoka hapo vilipo, kauli ya Mwalimu Nyerere miaka ile ya mwanzoni mwa uwepo wa Tanzania.


Kuvumiliana ndio mpango mzima.
 
Hawajielewi wazenji wanadhani kuwa wajomba zao waarabu watawasaidia siku wakiachana na bara, ni roho za uislamu zinawasumbua.
 
Wanaodhoofisha muungano si OMO, Jusa, Duni na wengine wenye kauli kama zao. Ni CCM walioshika kila kitu wanaobadilisha katiba. Cheo cha Makamo wa kwanza ni ceremonial.
 
Wameondosha lini uhamiaji kwenye muungano. Nadhani bado ipo chini ya Wizara ya Mambo ya ndani.
Hayo ya kuondoa Uhamiaji si maneno yangu, ni maneno ya makamu wa kwanza wa Rais Othman Masoud (OMO)

Rejea bandiko 196 nimeweka habari kwa hisani ya gazeti la Mwananchi. Soma kipande chini kabisa kinachosema ' giza neno mbele''. OMO anasema hivi ' kuna mambo yameondolewa katika Muungano lakini akija Kiongozi mwingine anaweza kuyarudisha' na kwamba kuondolewa ni hisani.
OMO akataja haya
Ushuru wa Forodha
Bandari
Uhamiaji
Mafuta na Gesi

OMO ametupa uhakika wa kile tulichohoji siku nyingi kwamba Rais wa Zanzibar ana mamla gani kikatiba kutoa Uraia?
Rais Mwinyi alitoa Uraia kwa raia wa kigeni. Sasa kwa maneno ya OMO kumbe Uhamiaji imeondolewa kinyemela.

Lakini OMO kasema ukweli, mapato ya Uhamiaji Zanzibar si ya Muungano , na hii ni kwasababu Uhamiaji imeondolewa kwa siri kama ilivyokuwa Bandari, mafuta na gesi.

Pascal Mayalla nilikuuliza kama unajua makusudi kabisa kwasababu wewe husema '' Uraia ni wa Tanzania'' kumbe nyuma ya pazia Uhamiaji haimo, kwa mujibu wa OMO na ushahidi wa gazeti upo.

Mag3
 
Ningekuwa na uwezo visiwa hivi ningevisogeza mbali kabisa kutoka hapo vilipo, kauli ya Mwalimu Nyerere miaka ile ya mwanzoni mwa uwepo wa Tanzania.


Kuvumiliana ndio mpango mzima.
Sikubaliani na kauli hiyo hadi utakapoleta ushahidi Mwalimu alisema lini na wapi
 
Wee Mayala unasema hakuna utanganyika wala uzanzibari wote watanzania, sasa kwanini mtanganyika hawezi kumiliki ardhi Zanzibar, yaani Raisi katoka Zanzibar na anaweza kumiliki ardhi Zanzibar lakini anaotuongoza hatuwezi kumiliki ardhi Zanzibar kama Raisi wetu, huoni Hilo ni tatizo? huo sio muungano
 
Bado haujanishawishi kuachana na visiwa hivi kwa hoja za mgao wa kinachopatikana hapa Tanzania. Ukikaa na mzenji atakuja na mawazo tofauti yenye kudhani kuwa mtu wa bara anamuonea mzenji.
Huu ulikuwa upuuzi wa Wazanzibar zama hizo, siku hizi tunakwenda na namba. Kwamba kwa uchumi wa Zanzibar wanaonewa wapi? Mwenyekiti wa ACT kasema 54% ya mapato ya uchumi yanatoka Muungano ambao ni Tanganyika.

Hizi hadithi za Wazanzibar tulishamalizana nazo, hakuna ulinganifu hata kwa bahati mbaya.
Kuna watu walikuwa wanawasomea vitabu .

Waulize, bajeti ya Ulinzi ni 3.3, wao wamechangia kiasia gani?
Waulize Bajeti ya mambo ya ndani mwaka jana ilikuwa 1.3 T, wao wanachangia nini
Waulize, ukiache kelele za kutaka nafasi za ubalozi, mambo ya nje wanachangia nini
Waulize, Muungano na Wizara na taasisi zake wao wana mchango gani
Waulize ile 4.5% ya Bajeti ya Tanganyika ni kiasi gani ukilinganisha na Bajeti ya SMZ
Waulize pesa za mikopo wanalipa kutoka bajeti gani ya SMZ
Kuna fedha nyingi sana wanapata kutoka bara wao wakisema Muunganp

Kwasababu wao wanalalamika, tunawaambia wana hiari! Tanganyika haina cha kupoteza!
Muungano ni muhimu kuliko chochote. USA wana miaka 247 ya uwepo wao na ni kwa sababu ya umoja wao.
Yes Muungano ni muhimu lakini lazima uwe muungano wenye tija, muungano usio na kelele
Kwa mfano wa USA, unakubaliana nasi kwamba sasa ni wakati Tanganyika iwepo na Zanzibar iwepo
Kabla ya kuendelea na muungano watasema wao, wapewe kura ya maoni.

Swali langu lipo pale pale, Tanganyika ina fadika na nini, na ina nini cha kupoteza?
Hata kama jimbo la Los Angeles linazalisha mara tano zaidi ya jimbo la Mississipi wanaendelea kuwa pamoja wakijua kuwa ule umoja wao ndio silaha yao muhimu dhidi ya kina Russia na China.
Yes! lakini hakuna mtu anatoka California kwenda Mississipi kwa Passport. Na Muungano wa USA una mambo machache ya Federal mengine ni state zinatawala. Ndicho tunahitaji sasa kwamba tuwe na Tanganyika halafu Wazanzibar kama wanataka waieleze Tanganyika ! Sisi Tanganyika hatuna cha kupoteza
 
Pascal Mayalla nilikuuliza kama unajua makusudi kabisa kwasababu wewe husema '' Uraia ni wa Tanzania'' kumbe nyuma ya pazia Uhamiaji haimo, kwa mujibu wa OMO na ushahidi wa gazeti
Mkuu Nguruvi3, nimeshindwa kabisa kuelewa jinsi akili za baadhi ya Watanganyika wenzetu zinavyofanya kazi.

Karibia nusu ya wanaojitambulisha kama Wazanzibari makazi yao ni Tanganyika na walezi wao ni Watanganyika.

Kama vile watoto wadogo, kwa kauli ya Baba wa Taifa, ingawa tumewapakata wanatunyea na tukiwaacha wanalia.

Inavyonekana sasa baada ya kupata ufadhili upya kutoka wa wajomba zao hawatuhitaji tena Watanganyika.

Ila wakikumbuka maziwa na asali ya mama Tanganyika bado wanasita kwa hadaa za mama wa kambo.

Kwa msaada wa wajomba na kina Pascal Mayalla watakomba kila wanaloweza na kuiacha Tanganyika hoi.

Hakika uvumilivu una mwisho…
 
Umenikumbusha kauli ya JPM kuwa Mayala ni jina la kisukuma na maana yake ni njaa. Ila hakuchukua hatua!
 
Hakuna binadamu zaidi ya wawili wanaoweza kuishi pamoja bila ya kuwepo kelele au kutofautiana, hiyo ni sifa ya kiumbe chenye uhai.

Mchango wao ni kuwa sehemu ya taifa la Tanzania. Watakapoanza kujitenga ndio tutaona kuwa hizo figures hazina faida yoyote kulinganisha na kuwa kitu kimoja kama taifa.
 
Zanzibar ni sawa na wilaya moja ya mkoa wa Tabora, uache kumiliki ardhi tupu iliyojaa huku bara uende ukatake kuimiliki ya Unguja!, hizo ni nongwa tu.
 
Miaka hiyo hiyo ya sitini baada ya kuwa tumeungana, sio kila kinachofanyika ndani ya JMT basi ukitambue wewe kwa ushahidi fulani.
Kuna hadithi za Wazanzibar za kumfanya Nyerere aonekane dhalimu na hii ni mojawapo. Hoja hii ililetwa mwaka 2011 tukawauliza watuambie Nyerere alisema lini, akiwa na akina nani na wapi! hadi leo hakuna anayesema. Ni uzushi tu

Juzi nimesikia akina Jussa wanasema eti Zambia walitaka kuungana na Tanzania, wwalipoona muundo wa Muungano wakakacha. Ni hadithi za kwenye kahawa! ukiuliza nani alisema wanasema '' marehemu Maalimu' alisema

Majungu na upuuzi tu!
 
Mpango mzima ni kuungana, kwanini Tanzania tufikirie kuungana na Sudan Kusini walio kilomita zaidi ya 3000 halafu tufikirie wakati huo huo kutengana na Zanzibar?. Ni somo lenye kuhitaji hekima nyingi sana kuliko jazba na visasi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…