Home of AC Milan, Official Thread

Home of AC Milan, Official Thread

naona inter alitangulizwa na baiskeli ya mbao dereva sneider kuvika kilima ibrahimovic kona ya boateng pumzi imekata.......napata hisia msimu huu ac milan watafanya vizuri sana!

absolutely Yes...
Mwaka wa Milan huu.
Na tulichomfanyia Inter pale Beijing Stadium ni salaam tu kuwa Buluda anakuja kuongeza idadi ya makombe ya kimataifa kabatini mwake.

nimependa zaidi usugu wa wazee watatu waliokuwa wanatimbwilika pale katikati yaani Van Bomel, Gatusso na Mzee Seedolf.
Kama Ibra ataendelea na kiwango kilekile basi tutachukua Scudeto mapema sana, na tutaenda beba champions league ya 8

Pato ailikuwa anawatukana wachina au?

Teh teh Pato hawezi kuwatukana wala kuwatania wachina, coz macho yake yenyewe ni kama ya wachina

naona msimu mmeanza kwa nchechemenchecheme!!!!ila kwa cassano pale mmelamba dume na asanteni kwa bunduki Andrea Pirlo The Magician,jana katisha sana akiwa na mkongwe Del Piero Fundi kuhakikisha Bianconeri tunarejesha heshima!

naona lazio wamewatoa jasho baada ya kutoka suruuu ya 2 2..

Mkuu kwanza hongera kwa kupata uwanja.

Pia sasa nimeanza kuhofia hii kasi ulioanza nayo na usajili ulionao duh...moto utawaka.

Serie A mi naipenda sana coz kuna timu zinawavua nguo watu wazima ile mbaya.

Kwa mfano ndugu yangu mechi ijayo Milan nakwenda kwa Napoli kisha namkaribisha Udinese...hizi mechi mbili lazima pachimbike

naona lazio wamewatoa jasho baada ya kutoka suruuu ya 2 2..

Lazio wale nao wanataka kuwa kama Parlemo ambao wako radhi wafungwe 7-0 na Udinese lakini wakikutana na Milan pachimbike...lol

naona mmewabahatisha barca leo!

Komredi kompanelo ktk watu ninaowaamini sana ktk swala la soka hapa JF miongoni mwao ni wewe.

Mi nilianza kutamba kabla ya mechi kwa sababu nilijuwa kwa usugu wa Milan basi vile vibarcelona vitaishia kupiga vipasi vyao tu palepale nje ya 18 na hizo pasi hazitokuwa na madhara.

Walichokifanya Rosonelli ni kitendo cha kuurudisha ukuta karibu na kipa wao so Barca wakashindwa kupiga zile pasi zao za mwisho ambazo mtu anabakia na kipa na kisha kumchambua anavyotaka.
wakati huohuo wazee sugu kama Ambrosini, Seedorf na Van Bommel wakitimbwilika pale katikati na kuhakikisha wanaupoza mchezo ili uende sawa na kasi ya umri wao.

Hao wazee sugu watatu niliokutajia woote wanapewa shkamoo na kocha wa Chelsea

Mkuu lini mtaacha sera zenu zilizo kinyume na za Asenali - sera za kujaza wazee wasioweza kukimbizana na vijana kama Afellay? Halafu hata madogo wenu kama Pato mbona wanaanguka hovyo utadhani wazee? Na huyo Robinho lini atakua? Si heri mumuombe Gaucho na Kaka warudi San Siro?

Wazee wametoshana nguvu na vijana tena wa Barcelona.
Sasa hivyo vitoto vya Arsenane na Manchester mbona kila kukicha vinachapwa tu?

komredi kumbuka hakuna kijiji kisicho na wazee.
milan mwaka 2003 walibeba champions league wakiwa na kipa Dida, kulia Cafu, kushoto Maldini, 4 Stam na mkoba Nesta.

Hakuna kijiji kisicho na wazee sheikh fahamu hilo

Nesta jana alimpa paja Messi, Messi akabaki akipigapiga kwa mikono nyasi..... Nesta ni big soo

Jana pamoja na kuelemewa beki ya Ac Milan ilihakikisha tiki taka ikiingia kwenye boksi inadunda haaha.

tumefungwa kwa taaaabu goli 3-1 toka kwa Napoli.
Magoli yao kafunga Cavani na letu kafunga Aquilani.
Nahisi ni uchovu wa safari toka Spain

tumefungwa kwa taaaabu goli 3-1 toka kwa Napoli.

Magoli yao kafunga Cavani na letu kafunga Aquilani.

Nahisi ni uchovu wa safari toka Spain

Poleni sana, mmefungwa kwa taaaabu kweli bao 3 kwa 1!

tumefungwa kwa taaaabu goli 3-1 toka kwa Napoli.
Magoli yao kafunga Cavani na letu kafunga Aquilani.
Nahisi ni uchovu wa safari toka Spain

haahaah!mkuu unanikumbusha story la jeba lililoliwa kiboga!limekiri kuliwa ila kwa taabu!!!!.......mkuu hao watoto Napoli mikosi sana watasumbua sana serie A msimu!huyo Cavani ni mnyama namkubali sana!!!!!formation letu Juve la 4-2-4 unalizungumziaje?kati mipira inapita shughuli mbele kwani huyo pirlo sawa na viungo watatu!!!!!

Ukiwa na jitu kama Pirlo yaani unakuwa na amani ktk timu.
Hilo ni Maestro sheikh.
Ila tuwape muda kwanza, isije ikawa presha ya uwanja mpya tu

tumefungwa kwa taaaabu goli 3-1 toka kwa Napoli.
Magoli yao kafunga Cavani na letu kafunga Aquilani.
Nahisi ni uchovu wa safari toka Spain

Mkuu how long does it take to travel from Barcelona to Milan? Au wanatumia usafiri wa bus?

Mkuu how long does it take to travel from Barcelona to Milan? Au wanatumia usafiri wa bus?

huwa timu zikitoka spain kwenda italy sababu zao huwa zinafanana mkuu unakumbuka na kipindi kile barca wanatolewa na inter walisema ni uchovu ndio maana wakapoteza kwa 3 - 1 na hawa milan naona wako hukohuko

Back
Top Bottom