Home of AC Milan, Official Thread

Home of AC Milan, Official Thread

Hahahaha Naona Watu wa AC Milan wanajipa moyo tehtehteh!!! Timu yenyewe bora hata Kobe anaweza Kuwa na Speed Vizee vya AC Milan vimechoka mbayaaaaa Wa Juve wapo fiti Del Boy sio Del Man atauwa Leo.
 
half time bila bila!vucinic anasumbua sana ngome ya milan sidhani kama ac milan leo watatoka kwa huu mziki
 
FT....JUVE 2 AC MILAN 0...huu mziki wa juve msimu huu ni wa kurudisha heshima kikombe lazima!milan ndembendembe!gang chomba pole sana mzazi
 
Milan hawana kitu hao. Wao wanadhani mechi muhimu ni kati yao na Barca tu! Waache wafunzwe adabu kidogo.
 
Tehteh washabiki wa AC MILAN mpo wapi? mlikuwa haoa mnaita Juve vizee mara mtatuvalisha hijab na baibui maneno yote mmemaliza nyie sasa KIZEE ni yule NESTA anashika goti mtumieni mafuta ya kisiwani ya karafuu apake...

Kuhusu Hijab na baibui sasa Kipa wenu kavalishwa G-String ya Bikini kabisa mlibanaaaa mara Pwaaaaaaa mmeachia. Juventus 2 Ac Milan zinjatropus 0. sasa waziri mkuu wa italy anawasubiria kwake.
 
Hii Milan bado sana,sioni mbadala wa Pirlo.Seedorf anahitaji msaidizi ,Juventus wakikomaa wanaweza kurudia zama zao
 
wametufungwa 2-0 lakini kwa taaaaaaaabu...

kwa tabu ila na mimba juu!.....conte ni mwalimu si msimamizi wa mazoezi nadhani umeona jinsi alivyoisuka juve akitumia wakongwe kadhaa!wanadefend kwa pamoja na kushambulia pamoja katikati mipira haikai ikimkuta fundi pirlo ni kuitupia nusu ya pili ya uwanja huko ni vipaji na kusumbua ngome ya ulinzi wa timu pinzani!....jembe ac milan inahitaji injini mbili moja ndo mmetuuzia pirlo!mna kazi kubwa nyie na inter!
 
Leo Juve asingeshinda isingekuwa haki kabisa, ila Vidal naye alikosa kosa nafasi mbili tatu za wazi. Ila ile howler ya Abbiati lazima impe nightmares.
 
kwa tabu ila na mimba juu!.....conte ni mwalimu si msimamizi wa mazoezi nadhani umeona jinsi alivyoisuka juve akitumia wakongwe kadhaa!wanadefend kwa pamoja na kushambulia pamoja katikati mipira haikai ikimkuta fundi pirlo ni kuitupia nusu ya pili ya uwanja huko ni vipaji na kusumbua ngome ya ulinzi wa timu pinzani!....jembe ac milan inahitaji injini mbili moja ndo mmetuuzia pirlo!mna kazi kubwa nyie na inter!

Myao Conte kachanganya wazee gani?
Timu yao woote ni damu changa wale na mzee ni Pirlo na Gigi golini.

So huwezi kuwafananisha na Milan ambao wachezaji wao 6 tu yaani Abiati, Ambrosini, Nesta, Zambrotta, van Bommel na Seedorf ukijumlisha miaka yao ya kuzaliwa utapata miaka 208.

Milan kwa sasa ni usugu tu ndio tumebakia nao lakini haraka iwezekanavyo timu ya kwanza wanatakiwa waanze kina Taiwo kwa Zambrotta, Flamini kwa Van Bommel, Nocerino kwa Gatusso, Mexes kwa Nesta na Robinho kwa Seedorf.

Pia kuna baadhi ya wachezaji ni marufuku kucheza.
Wachezaji hao ni Luka Antonini na Daniele Bonera.

Juve mlipata unafuu wa mechi baada ya mkulungwa Nesta kutoka na kisha Bonera kutupiwa ndani na antonini kuingia shavu la kulia.
Kwa hiyo Juve wakafanikiwa hata kupiga zile one-two kwa kuwa tu hakukuwa na Nesta.

hakika Kwa sasa Maldini, Baresi na Costacurta wanatakiwa wawepo ktk kila mechi ili kuhakikisha wanaihamasisha timu.

Alegri peke yake hawezi liongoza jahazi la Milan.
 
gang ukiwa na kipa mzoefu na injini ya kati mzoefu damu changa zikiwa ndani lazma upande uhondo ule!vijana watajifunza pia kwa mjomba piero!sera ya wazee milan inabidi muachane nayo kwani wale napoli wananitia sana mashaka kwa kabumbu lao!
 
washabiki wa Juve mpoo?
Teh teh naona juzi mmeshikwa shati mnaanza kuweweseka.

Napoli nao hoi wamekubali kutoa haja kubwa sebleni kwao na kukubali kipigo dah.

Roma Derby ikaisha kwa SS Lazio kuwasasambua mahasimu wao AS Roma kwa Jumla ya magoli 2-1.

Udinese nao kama Juve wakaambulia patulo ya bila kufungana na majezi yao ya Pundamilia.

Milan wakawafturu Parlermo kwa juma ya magoli matatu kwa bila.
Huku Robinho akiwaarifu mabeki kuwa sasa amerudi.

Dah Inter kuwazungumzia sitaki.
Ila napenda kuziona Picha za Moratti za hivi karibuni, je mpayukaji yule anafanania vipi kwa sasa?
 
Ndetichia juve wanaongoza Ligi huku wakiwa wanambwela...
 
uefa champions league result...

lille 0-1 inter...
Napoli 1-1 Bayern...
 
Back
Top Bottom