Home of AC Milan, Official Thread

Home of AC Milan, Official Thread

hawa jamaa ni noma sijui itakuwa kwao Napoli siku ya marudiano..

Napoli wanaponipa wasiwasi ni kitendi chao cha timu yao kuwa hiyohiyo kila mechi.
Yaani nikilala na kuamka najuwa lazima Golini awe de Sanctis, mabeki ndio walewale kina Paolo Canavaro, hugo armando campagnaro, viungo ndio kina Inler, maggio, Hamsik, Lavezzi, Zuniga sijui na mtu wao wa mbele sina haja ya kulitaja kutokana na kitendo alichonifanyia msimu huu.
Ila all in all heshima nawapa.
Na nawatakia kila la kheri ktk tashtiti zao
 
uefa champions league result:
MILAN 2-0 BATE.
Ibrahimovich and Boateng wameiwezesha AC Milan kupata ushindi wa goli mbili kwa bila na kuifanya timu hiyo yenye mafanikio zaidi hapa Duniani kuwa na Point 7.
Mchezo huo ulipigwa ktk uwanja wa Sansiro Meazza.

Forza Milan.
 
hiv mashindano haya ya UEFA champions league je Juve wamecheza juzi Jumanne au jana Jumatano?
 
juve 2-2 Genoa...
Teh teh teh

pamoja na kutoka suluhu chama kubwa juventus bado linashika usukani huku wazee wenzake milan na inter hata wakishinda mechi zao za viporo bado hawawezi kuifikia juve!....ni matokeo ya ushindi ya udinese,cagliari,lazio ndo yanaweza kufanya usukani tuuweke rehani!
 
pamoja na kutoka suluhu chama kubwa juventus bado linashika usukani huku wazee wenzake milan na inter hata wakishinda mechi zao za viporo bado hawawezi kuifikia juve!....ni matokeo ya ushindi ya udinese,cagliari,lazio ndo yanaweza kufanya usukani tuuweke rehani!
Naona mbio za Juve zimeshaanza kufifia
 
Naona mbio za Juve zimeshaanza kufifia

vilabu vimejizatiti mkuu win win situation tunairudia mbona!wewe unadhani inter na ac milan wanapenda kuwa katika nafasi wanazoshika?watoto wanakomaa!wana njaa aibu.....
 
wakuu nacheki game hapa Milan na leece dakika ya 57 sasa milan kashapigwa bao tatu ..
 
prince. " boateg" katoka benchi kaja kupiga bao tatu peke yake 63min milan 3 .. lecce 3
 
Lecce 3-4 Milan.
Magoli matatu yaliyofungwa na Kelvin Prince Boateng yalipelekea Buluda Milan kusawazisha magoli yote matatu ambayo waliyapata Lecce 1st Half na kisha nguli toka Colombia Mario Alberto Yepes akafunga goli la ushindi na kupelekea Milan kupata ushindi wa goli 4-3
 
kaka game ilikuwa tamu.. baada ya kurudisha zile tatu nilijuwa basi.. milan washamaliza kazi
 
Back
Top Bottom