Home Shopping Centre wazusha taharuki Kariakoo

Tutabishana hadi kiama hapa lakini tutazame source,ni kwa nini watz wengi wameamua kufuata mkondo wa ukwepaji kodi na rushwa?je,hizo kodi,taratibu za serikali pamoja na huduma za wafanyakazi wa sekta hii kama TRA,bandari n.k zinaruhusu mtu wa kawaida kutumia njia za halali kupata mali yake na kufanya biashara kwa mafanikio?hebu jaribu kusafirisha kacorolla kako toka Japan kwa kufuata kila njia halali uone ni kwa nini rushwa haiishi Tz!sasa sielewi kuwa watu kama Said wanatake advantage ya mazingira au wako ndani ya mtandao maalum wa wakubwa wanaohakikisha njia za halali zinakuwa ngumu ili tuwapigie magoti na kuwapa wao "kodi" badala ya serikali.
 
Haya yote ni makelele, mwisho wa siku makontena yataachiwa na huyo Masamaki ataondolewa hapo Bandarini. Hii nchi inaongozwa na mafisadi, usipo kubaliana nao lazima wakutose! Tusubiri tuone!
 
Nataka niwatangazie tangu Said ashtukiwe kariakoo imetulia kwa kupaki olela magari yake kwani kabla alikuwa anapaki anavyotaka magari yake na kuziba njia kariakoo nzima bila kuchukuliwa hatua zozote. sasa kariakoo safi gari zake hazizibi tena njia.
 
kitu kinachoitwa umasikini wa Watanzania ni kukosa huduma stahiki za kijamii (shule, matibabu, barabara, maji, umeme, makazi, chakula nk) ambavyo inabidi vitolewe na serikali. Serikali haina miradi wala haifanyi biashara, pesa yake inatokana na watu wake kulipa kodi - halali. Na kodi ispokusanywa ndio matatizo unayoyaona hivi leo.
Kama kweli ikithibitika kuwa hawa jamaa wanafanya mchezo wa kukwepa kodi basi hiyo ni sawa na uhaini, na kibaya zaidi isije kuwa sio Watanzania.
Kwa maana hiyo unachotaka kusema ni kama mtu ambaye anafaidika na mfumo wa ujambazi. Kwamba waporaji wanakugawia kiasi cha mali walizopora lakini hujafikiria wanaoporwa (wananchi wa kawaida) wana machungu kiasi gani.
Fuatilia Ulaya, Marekani, Brazil, China, India, Uarabuni wote hawa ni jinsi gani walivyo makini kwenye suala la kutoza kodi na sio ajabu ndio maana wanaendelea. Ukiseme kuwa serikali iachie wajanja wachache waunde 'TRA 'B' zao hatutaenda popote.
Yote haya yategemee ushahidi kama kweli kuna mchezo mchafu kama haupo basi apewe biashara zake aendelee

 
juve2012, umeyanena vizuri haya mambo.
Kama tulivyoua elimu, afya na nyanja nyingine na sasa tunaua uti wa mgongo wa taifa ambao ni mfumo wa kodi. Hawa wanaoitwa wakubwa ni wanasiasa, na wanasiasa mpaka sasa tumeshaona kuwa uwezo wao wa kufikiri ni wa chini sana lakini wameendelea kuwapo hivyo kuthibitisha kuwa tatizo sio wao bali ni Watanzania kwa ujumla wao.
Sio ajabu Benki ya dunia iansema tumepoteza Us $1.2 billion mwaka jana kwa bandarini tu. Sasa hapa watu wanavyoongea kuwa huyu mtu mmoja tu anasimamia kiasi kikubwa hivi cha mizigo na yupo zaidi ya miaka kumi unapata picha gani kama si TRA kwa kipindi hicho kupoteza $ trillion 70!!??
Wanaosema tatizo ni mfumo wana hoja na tusisahau kuwa mfumo hauna jina lingine zaidi ya CCM

 
HOME SHOPPING CENTRE WAPO VIZURI WAPEWE PONGEZI ZAO.

Maadui wakubwa wao ni Wafanyabiashara Wakubwa waliojijengea MONOPOLY ktk Biashara Fulani na KATU KWA UDIKTETA hawataki Mwingine yeyote Aingilie!

Untouchables Vijana hawa Wamevunja Mwiko huu na wanachokipata sasa Kuchafuliwa ni Matokeo ya Mipango ya Muda mrefu ya watu hawa kupitia Vikundi,Magazeti na Watu Mbalimbali Kuwachafua,
Pia Baadhi ya Mawakala sio wote ambao Wanalalamikia Kuporwa sijui kazi zote na Hawa Vijana,Hivi ht ingekuwa Kweli ktk Zama hizi za Soko Huru ,Unaweza Kweli Kulalamika kwanini Kampuni fulani Wananunua Maji yake kuliko ya Kampuni yako na Kuanza Kuchafua kujenga UHALALI
Nilikuwepo ktk Kikao kimoja cha waziri na mawakala Nawachallenge Mawakala wa Nyuma waweke Hadharani Kuona wao wanalipa vp na hawa HSC wanalipa vipi!???
Ni Majungu Matupu tu kwa wasiojua wanakimbilia Kuhukumu tu,Nendeni TRA Mkaangalie rekodi kontena ya Bidhaa Tofauti walicholipa wao na wengine km Kuna Tofauti yoyote? Ulongo mtupu na Majungu WANAPATA KAZI TOKANA NA SERVICE YAO NZURI DOOR TO DOOR sio jambo linginelo lolote
 
HSC WANAJUA WANACHOKIFANYA...WATANZANIA WENGI WAVIVU UBUNIFU WA HAWA JAMAA UNAWACHANGANYA
DONT HATE THE PLAYER, HATE THE GAME...
Wakurugenzi wa Kampuni Hii wana Asili ya Saudia na Yemen,Wana Uhusiano wa Karibu na Viongozi wa Saudia Mtakumbuka alipokuwepo Balozi aliyepita wa Saudia waliwahi kupitia yeye HSC kutoa Pampu 800 Za Maji Zilizosambazwa Nchi Nzima Kusaidia Mama Zetu na Dada Zetu Vijijini kwa USHAWISHI wao
Mmoja kati ya Matajiri wa Dunia hii wa Kisaudia TRILIONAIRE PRINCE TALAL AL SAUD AL WALEED alipozuru Nchini Walikuwa Wenyeji na Ndio walimpokea Airport na ht Kumpeleka Kwa Viongozi wa Serikali na walihudhuria Mazungumzo ya Uwekezaji
Sasa Ajabu gani kwa Mtu anayejua Medani za Biashara za kimataifa Vijana hawa kuwa Matajiri??!
Sent from my BlackBerry® smartphone provided by Airtel Tanzania.
 
MAJUNGU HAYAFAI HSC WAPO VIZURI WAUNGWE MKONO
Vijana hawa Fedha Nyingi Wanappata Nje ya Nchi lakini Wanawekeza hapa Tanzania mfano kutokana na Uaminifu wao na Kuaminiwa na Watanzania wengi wanakusanya Kontena Nyingi sana kwa Mwezi na kupewa SPECIAL RATES na wenye MELI,Hivyo wanapata Faida kidogo kwa Kila kasha na kwakuwa Mizigo ni Mingi Hutengeneza Faida kubwa(NJE YA NCHI)
Wanatoa Misaada Mingi kwa Jamii Kuliko hao Wafanyabiashara Matycoon Wanaofyonza Nchi kwa Mabilioni na mmekaa Kuwatukuza,Maskini vijana hawa Wanashambuliwa ajili ya Mafanikio yao ya Muda mfupi,Tufanye Kazi na Kuacha Majungu
 
Mada ni Home Shopping Centre au mada ni makontena kukwama bandarini?

Hivi hawa kina Rished Bade hili limewashinda kabisa?
 
mkuu kipasta, hili suala sasa naanza kuliogopa maana sikujua kama lilikuwa na maelezo haya yote.
Hebu linganisha maelezo yako na haya ya kwenye gazeti la Tanzania Daima then utupe mwanga zaidi ya muendelezo wa hili suala.
 
Mada ni Home Shopping Centre au mada ni makontena kukwama bandarini?

Hivi hawa kina Rished Bade hili limewashinda kabisa?
au ni 'habari ndani ya habari' kwa hiyo hazitenganishiki
 

Hata wewe pia unachangia kuangamiza Taifa hili kwa kutumia JF ambao pia hawalipi Kodi! Hakuna wa kumnyooshea Kidole mwingine TZ!

 
hsc wako vizuri tuache majungu.....
Vijana hawa Fedha Nyingi Wanappata Nje ya Nchi lakini Wanawekeza hapa Tanzania mfano kutokana na Uaminifu wao na Kuaminiwa na Watanzania wengi wanakusanya Kontena Nyingi sana kwa Mwezi na kupewa SPECIAL RATES na wenye MELI,Hivyo wanapata Faida kidogo kwa Kila kasha na kwakuwa Mizigo ni Mingi Hutengeneza Faida kubwa(NJE YA NCHI)
Wanatoa Misaada Mingi kwa Jamii Kuliko hao Wafanyabiashara Matycoon Wanaofyonza Nchi kwa Mabilioni na mmekaa Kuwatukuza,Maskini vijana hawa Wanashambuliwa ajili ya Mafanikio yao ya Muda mfupi,Tufanye Kazi na Kuacha Majungu
 
kumbe tunaonewa sisi wanyonge kuhusu kulipa kodi wakati wageni wanaididimiza nchi yetu jamani tunakwenda wapi je serikalli yetu haioni haya jamani
 

Ndo hao sasa doc.za container la nguo zimeandikwa toilet paper
 
Nchi hii SAMAKI mkubwa humla samaki mdogo....... Hapo kuna masilahi ya VIGOGO !! nawe tafuta kigogo wako mambo yako yaende vizuri... GOOD LUCK.
 
i am curious to know, hivi wewe @Mr Ethos na wewe @kipasta ni mtu mmoja multiple ID's? wote mnamtetea Home Shopping Center, wote mmejiunga JF siku Moja.....is that coincidence? Kama jamaa hawalipi kodi wacha wabanwe, misaada kitu gani mkuu?yaani watuibie matrilion ya pesa halafu waje warudishe vi-million ndo tuwasifu? Kulipa Kodi ni Jambo la kiungwana, walipe kodi, porojo waache.
 

mwana jamii forums tunashukuru kwa kuwa muwazi kwa nia ya kuweka jambo hili lieleweke kwetu.
Kumbe kuna wizi mkubwa namna hii jamani?. Hivi jamani kweli watu tumewapa dhamana watuongoze wanageuka kula mapato ya wanannchi wa tanzania?

Mimi nasema jamani tumwachie mungu maana kila neno na tendo litaletwa hukumuni
mungu atahukumu sawa sawa na matendo yao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…