Home Shopping Centre wazusha taharuki Kariakoo

Home Shopping Centre wazusha taharuki Kariakoo

Chezea biashara za wakubwa wewe?
 
Sasa hivi container lazima ikaguliwe ndio itoke. HSC na kampuni yake ya usafirishaji Silent road hauliers wamekuwa wakidanganya kodi na hata Tanroad kitengo cha mizani wanakula nao, wana overload sana na container za cement ya pakistan.
 
HSC wanakampuni kibao za Clearing bandarini pale, wafanyabiashara wanalazimika kuwatumia hawa jamaa kutokana na kuwa na mkono TRA na wakubwa wa wizara ya fedha. Ukijifanya unatumia kampuni nyingine kwa wafanyabiashara wa nguo, viatu, pazia na vinginevyo utapigwa ushuru wa kufa mtu. Ila ukitumia HSC container la nguo au kitenge unalipa mil.28 tunaambiwa jamaa yeye anacheza na wakubwa wa TRA anasema container lina Tooth pick au toilet paper yeye analipa TRA mil.7 dah kumbe zigo linathamani ya dola 170,000/= ishu ya Mwakyembe kuanza kukagua container imeanza kumuumbua bwana HSC na wakubwa wa TRA imesababisha taharuki kwa wafanya biashara k.koo mizigo imezuiliwa na biashara imesimama. Serikali imepoteza sana mapato juu ya hawa jamaa HSC wanakula pia na polisi wanasindikiza toilet paper kumbe nguo au vitenge au tv au friji.

Mkuu Mwakyembe anahusika vipi na TRA naomba ufafanuzi.
 
Mkuu Mwakyembe anahusika vipi na TRA naomba ufafanuzi.

Mkuu Ritz acha sihasa k.koo mizigo imekwama bandarini baada ya hawa jamaa kuhodhi biashara ya clearing otherwise una hisa na HSC kuna siku nakumbuka ulitamka unaganga njaa k.koo. Sasa hivi maduka hayana mali mpya. Mwakyembe amekomaa na TISCS wanao pakua mizigo kwenye meli HSC wanakwepa kulipa ushuru container la Nguo la thamani dola laki 4 linaandikwa toilet paper jamaa wa HSC analipa mil.7
 
Last edited by a moderator:
Wivu unaea sumbua enyi kizazi cha kitumwa

Ukweli upo wazi nenda k.koo kesho kaulize nani bingwa wa kutoa mizigo bandarini na kama uamini uliza clearing forwards mizigo ya k.koo kikubwa hawa HSC wanakwepa ushuru.
 
Wivu unaea sumbua enyi kizazi cha kitumwa

watumwa wa wayahudi
 
Mkuu, mbona wewe ni mkongwe humu jf, unashangaa? Tulishajadili kitambo kidogo ifisadi wa hawa hsc, tukaweka na ushahidi. Pekua thread, utaikuta

Hawa jamaa wanakwepa sana kodi canter za HSC hata polisi huwa hawasimamisha wanaelewa kilichomo na nani anakula escot money
 
Sio kweli huyu jamaa namjua wala HSC haina leseni ya uwakala wa mizigo yeye ana shipping agencies China na Dubai na sio dhambi mtu kufungua biahara nje ya nchi
 
Mkuu Mtoi ndivyo ilivyo hali ni mbaya bandarini baada ya container za HSC kukamatwa zikiwa wame declare
vyandarua na wayamesh wakati ndani kuna vitenge na makapeti,hata saa hii kuna mkutano kati ya waziri wa
fedha Mgimwa na madirector wa makampuni ya Clearing and forwarding kinaendelea kwenye ofisi za wizara ya
fedha.Na document zao zilikuwa zinapigwa direct Release zote hazikuwa zinakaguliwa,baada ya ofisa mmoja wa
TRA kushtuka akaamua kukagua ndio balaa lilipoanzia na container zao nyingi zimekuwa seized bandarini,na
kumekuwa na shinikizo toka kwa wakubwa serikalini kwamba container ziachiliwe,lakini hongera kwa commissioner
wa customs ndugu Masamaki amewagomea kuzitoa.Issue ndio kwanza iko hot'

Mimi ni mfanyabiashara na nimefanya biashara na maagent wengi na hawa maclering wanazingua sana mambo yangu hapa ni machache kama ifuatavyo...
1. Hapa tusichanganye mambo ya vita za madaraka ya ukamishna wa tra, vita ya maclearing na maisha ya maskini
2. Hakuna asiyejua masamaki alikuwa manager wa mafuta na alivyokuwa anapitisha mafuta bure! Leo mafuta yanapita na mzigo wote anahamishia kwenye makontena
3. Hakuna asiyejua ubabaishaji, wizi, utapeli na rushwa wa BAADHI ya maclearing, kama ametokea clearing mwaminifu lazma biashara itahamia kwake
4. Maclearing wengi ni mawakala wa rushwa za macustom officer ! Hawawezi kumpenda mtu straight.
Sasa vita zao wasiingize na sisi maskini watuache tufanye kazi vita zao wamalizane wao wenyewe ...
 
kwa kifup tu hawa jamaa mimi nimefanya nao kaz tangu mwaka 2007 wananisafirishia mizigo yangu toka china na dubai. ukwel kama alivyosema jamaa mmoja hapo juu ni kwamba kwa kias flan wanawasaidia Wtz masikin kupata hela na matajir pia ila njia anazotumia kuwapa utajir ni kwa kukwepa kodi kwa kusaidiana na baadhi ya watumish wa TRA wale wakubwa. wakat huo yeye kwa kuwaweka watu kati huko juu anapiga hela nyingi mno yaan unaibiwa mwenye mzigo na serikali hasa serikal. conteiner la nguo ni TshsMilion 17 kwa futi 20 lakn yeye anakuambia ni milion 19 au 20 lakn unatolewa on the sport ikifika. so kinachojitokeza serikalin wanabadilisha document wakishirikiana na watu wa TRA conteiner la nguo linabadilishwa linakuwa la cement so analipia milion 5 mpaka 7 za juu anawapa kidogo watumish nyingine zake. huu mchezo ameuanza cku akisaidiwa na Zakhia Megi kipindi akiwa wazir wa fedha. walichofanya wamemuuzia Riz 0ne hisa so wanaiba hela nyingi ni Mungu anajua. ingawaje ukwel mwingine mchungu ni kwamba kampun yake ndio inasuply karibu mizigo yote kkoo na posta so kumfungia ni kusababisha ombwe la mizigo sokon na pesa kupungua serikaln ushahd ni juz mwakiembe kakamata conteiner zake mia moja leo hii wamezuiliwa kutoa mizigo wk hiz mbili tu tayar imebid wazir wa fedha awaite wafanyabiashara aongee nao tatizo liko wapi. coz hazina haisomeki. na kwa kuwatonya nasikia hata mtoto wa mshua wakat anakamatwa china kama ni kweli hawa jamaa ofic yao ya china ndio iliratibu mazungumzo ya kuachiwa kwao.

HAPA TUNAJICHANGANYA SANA WATU WANAKAZANA HOME SHOPPING CENTRE HEMBU ONA HAPA
1.Tatizo hakuna kiongozi anayenunua nguo kariakoo, sio waziri,kitilya, kamishna wala wake zao wala watoto wao. Hapa bei ikipanda maskini ndio watatembea peku na uchi, sio mawaziri. Nchi hii tumeamini maskini hana haki. Viongozi wetu hawatuthamini.
2. Hapa wananunua maskini shati 2500 , yeboyebo 2000! Sasa tupige hesabu yeboyebo hata kama zinaingia 10000 ndani ya kontena inakuwa 20m, sasa kodi 45% mtu anakuambia ulipe 90m kodi unazitoa wapi. Waje hapa waziri na kamishna tupige hesabu.
3. Hela zetu za mikopo, tunalea wazee wetu vijijini, mnataka wafe?
 
Huu ni umbea mwingine HSC ilikuwapo kabla hata mkuu wa kaya unayemsema kuingia madarakani na walikuwa wapo vizuri ile mbaya jamaa wamejipanga wanapiga kazi na ndio mana wanasikikafanyeniresearch na muache kurukia habari nendeni TRA mkacheki wanalipa kodi zote VAT, MAPATO,PAYE,NSSF etc kwa muyjibu wa sheria acheni chukibinafsi watanzania tufanye kazi..
 
Hapa kuna issue nyeti...itaiva siku siyo nyingi. Hayo ya HSC na Ikulu yamesemwa mara nyingi sana, hata gazeti moja, bila shaka ni Mwanahalisi ilishaandika sana jinsi kampuni hii ilivyo na uhusiano wa karibu na Mama Salma na Riz...na jamaa huwa wanaingia Ikulu kama kwao na hakuwa wa kuwahoji..
- na huwa ma-container yao huwa hayaruhusiwi kuguswa na wakaguzi wa pale bandarini. na pia kuna wafanyabiashara wa mikoani walishakubali kusafirishiwa bidhaa zao kwa bei chee kupitia kampuni ya HSC ya clearing na Forwarding then bidhaa zao zilipofika Dar, huwa hawapewi BL na vibali vingine halisi, kwa kuwa hawakuwa na vibali toka kwa HSC waliishia kupoteza bidhaa zao kwa kukamatwa na ndio walikasirika na kupasua majipu na uozo wa hawa jamaa...wanaenda ikulu kila mara ndio wanaenda kujadili deals.
- Kkoo wameotesha nyumba kama upepo...mojawapo ni jumba linalotazamana na Ben Mkapa Sec
- wanamiliki Benki (Amana Bank) na wanafanya kila biashara sasa...!

WATU HAWAPENDI KUJUA UKWELI lakini hili halipingiki
1. Hapa issue ni makontena kukwama kwa kuongezwa bei na maafisa wa custom kwa sababu wanazojua wao. Aidha wanamrudisha nyuma Mhe. JK kwa kutaka achukiwe na maskini
2. Wenye makontena ni wafanyabiashara na si maagent
 
Mbona hii ishu ishaisha? Wafanyabiashara wa k.koo wameambiwa watapewa mizigo yao wasubir upepo upite tu kila kitu kiko sawa.
 
Mkuu Ritz acha sihasa k.koo mizigo imekwama bandarini baada ya hawa jamaa kuhodhi biashara ya clearing otherwise una hisa na HSC kuna siku nakumbuka ulitamka unaganga njaa k.koo. Sasa hivi maduka hayana mali mpya. Mwakyembe amekomaa na TISCS wanao pakua mizigo kwenye meli HSC wanakwepa kulipa ushuru container la Nguo la thamani dola laki 4 linaandikwa toilet paper jamaa wa HSC analipa mil.7

Nyunzo,

Wapi nimeleta siasa? Wewe kuongea siyo siasa? Usipende kuokota maneno mtaani ndugu yangu, mimi sigangi njaa kkoo, kama unachosema ni uhakika basi wasaidie serikali kuwaonyesha wanavyokwepa ushuru.

Mwakiyembe ahusuki usitake kudanganya watu issue ni maangent na kamishna wa TRA, Mwakyembe yeye kitengo chake kwenye kuifadhi makontena siyo kulipia mizigo.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom