Home Shopping Centre wazusha taharuki Kariakoo

Home Shopping Centre wazusha taharuki Kariakoo

Hivi hii noma inw connection yoyote na stanbic bank kariakoo branch?
 
Watanzania lazima tufikiri sana tunapoelekea na lazima tufikiri sana before we write our opinion or listen to rumours...
Haya ni maneno yanajengwa na wafanyabiashara wengine rivals wa Hawa vijana..
hawavijana wanajenga nchi na kuwapa Kazi watanzania wengi tuu faida zao za kibiashara zinatumiwa hapa hapa Tanzania which means they are business benefits/kuwanufaisha watanzania wote...
Mbona hatupigi makelele Kwenye machimbo ya gold,barrick ambapo Ndege Hutua uko uko shinyanga na ku chukka dhaabu zebu na kupelekwa marekani na nchi za europe...
point yangu ni tusiwakandamize watanzania wenzetu kibiashara.
 
Habari nilizopata toka kwa wafabiashara wa kariakoo ambao ndio waathirika wa makontena yalioko bandarini ni kuwa...
1.hsc ni bingwa wa kukwepa kodi Tanzania.
2.wafanyabiashara wakiagiza vitenge,tv,jenereta au hardware yeye kwenye kulipa bandarini anaandika tishu au net za msaada hivyo kulipa kidogo au kutolipa kabisa.
3.hsc ni Kampuni toka ikulu na vigogo wastaafu.
4.hsc haijakamatwa kwa bahati mbaya, na Mwakyembe kubadili utawala bandarini sio bahati mbaya Bali ni mpango maalumu.
Na kilichofanya hiyo Kampuni kuanikwa hadhani ni kitendo cha kuingilia tenda za vigogo wenzie akiwemo Zakaria na ishu ya betri za taiga.
Zaidi ni kitendo cha kutukanwa Mwakyembe na mkurugenzi wa hsc kwa kuambiwa Siwezi kuongea na wewe (Mwakyembe) naongea na mkubwa wako (jk)
Hivyo Mwakyembe nae akaamua liwalo na liwe kama uwaziri nifukuzwe tu Makotena hayatoki mpaka yalipe kodi halali.

Lakini mpaka sasa baada ya sakata la takribani miezi miwili juzi makotena yameanza kutolewa.!
 
idawa, yameanza kutolewa ndiyo. Lakini cha ajabu wakati ina hand in mzigo wako nje ya nchi wanakupa invoice kutokana na ukubwa wa mzigo. Sasa mizigo imepandishwa bei by 50% na zaidi. Ina maana hongo na faini za kukwepa ushuru wamebebeshwa wateja. Hii sio haki kabisa na hakuna pa kukimbilia. Na wanajibu jeuri ile mbaya, wanasema uache mzigo siku saba na baada ya siku 14 wanauuza!
 
Last edited by a moderator:
Mkuu King'asti unachoongea ni kweli, maana awali kupitia hsc wafanyabiashara walikua wanalipa 20-25 milioni kwa kontena lakini sasa imelipuka mpaka 65-90 milioni.

Hapa zaidi anaeumizwa ni mlaji wa mwisho ambaye ni mtanzania maskini.

Hatuungi mkono ukwepaji wa kodi, lakini TRA lazima wajue hawamkomoi mfanyabiashara Bali mtumiaji wa mwisho.!!
 
Last edited by a moderator:
Watanzania tunaumia sana,

we have one of the highest tax rate compare all over Africa serekali yetu wamefanya tax na bandari as a main income source.....tanga mji wameuua Kwaajili yakuongeza tax.....lazima serekali yetu waangalie sana au Wanaichi tutaumia
 
Habari nilizopata toka kwa wafabiashara wa kariakoo ambao ndio waathirika wa makontena yalioko bandarini ni kuwa...
1.hsc ni bingwa wa kukwepa kodi Tanzania.
2.wafanyabiashara wakiagiza vitenge,tv,jenereta au hardware yeye kwenye kulipa bandarini anaandika tishu au net za msaada hivyo kulipa kidogo au kutolipa kabisa.
3.hsc ni Kampuni toka ikulu na vigogo wastaafu.
4.hsc haijakamatwa kwa bahati mbaya, na Mwakyembe kubadili utawala bandarini sio bahati mbaya Bali ni mpango maalumu.
Na kilichofanya hiyo Kampuni kuanikwa hadhani ni kitendo cha kuingilia tenda za vigogo wenzie akiwemo Zakaria na ishu ya betri za taiga.
Zaidi ni kitendo cha kutukanwa Mwakyembe na mkurugenzi wa hsc kwa kuambiwa Siwezi kuongea na wewe (Mwakyembe) naongea na mkubwa wako (jk)
Hivyo Mwakyembe nae akaamua liwalo na liwe kama uwaziri nifukuzwe tu Makotena hayatoki mpaka yalipe kodi halali.

Lakini mpaka sasa baada ya sakata la takribani miezi miwili juzi makotena yameanza kutolewa.!

Sasa tunalalamika nini....

Kwanzatulikua tunatolewa kwa bei Nzuri na tunalalamika na kutoridhika....na bei sasa ndio hiyo imepanda manake tumesemaaa sana sasa serekali imepandisha tax kwa kweli mimi duka langu ninabidi nilifunge manake biashara inanishindwa....

serekali yetu inafanya tax ya bandari main income na kulisha nchi nzima this is impossible.....

we have the highest Tax compare na Africa nzima.....Vipi tutafanya biashara hivi,sisi wafanya biashara wadogo tunaumia kiss zakaria na tenda yake ya betri......wakati biashara ni competion
 
Tetesi zainasema kuwa Home Shopping Centre ni mali ya mkuu wa kaya (tz) na ndio sababu mara nyingi makontena yake yamekuwa yakipita bandarini bila kutozwa ushuru wakati watanzania wa hali ya chini ambao wamempa dhamana wanaumizwa kwa kucheleweshewa mizigo yao bandarini kisa hakuna hela hazina.
Tetesi zinaendelea kusema kuwa hivi sasa kuna container zipatazo 30 bandarini zilizofojiwa detail kuwa zina vyandarua na kumbe sio. na badala yake zimegudnulika kuwa zina vitenge. (no wonder they are the cheapest shopping centre in TZ)
Ingawa sisuport fujo za Mtwara lakini tafakarini kama wananchi wa tanzania wanaojulikana ni waoga au niseme (waerevu wa kijinga) leo wanadhubutu kupambana na polisi kweli ni kwasababu ya Gas tu. Wananchi wamesikia mengi wamechoka na wamechoka sasa.

Naomba mwenye detail zaidi juu ya hili ambalo linasememkana lina uhusiano mkubwa na kikao cha leo wizara ya fedha atuhabarishe zaidi.

Hapo kwenye RED = siyo kweli
 
Ilinipitaje hii!!!!!

CC MD25
 
Last edited by a moderator:
Huyu home shipping centre ni nani hasa na kwa maslahi ya nani guys wake up mulika mwiziiiiii
 
Back
Top Bottom