Hata hivyo, BoT mmeshindwa kabisa kusimamoa Sheria ya Huduma Ndogo za Fedha ya mwaka 2018 na kanuni zake za huku mitaani.
Mitaani biashara hii inafanyika kiholela kwa watu wasio na leseni huku wakitoza riba kubwa mpaka kufikia riba ya asilimia 40 kwa mwezi.
Taasisi za kifedha kukaa na kadi za benki za Watumishi huku na wao wakitoza riba kubwa kinyume Kabisa na sheria.
Taasisi hizi nyingi hazitumii utaratibu wa Reducing katika kutoza riba na baadhi hazitoa hata mkataba kwa wateja wao.
Kwa kifupi, mapungufu ni mengi na wahusika hawana hofu kwassbabu usimamizi wa sheria ni hafifu kwa kiasi kikubwa na hivyo wana-assume sheria haipo kwassbabu imekosa usimamizi.