Hongera Camilius Wambura kwa utulivu huu nchini

Huihui2

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2012
Posts
7,021
Reaction score
11,475
Takriban miezi 2 kufika leo media zote zilijaa mambo ya upotoshaji kutoka kwa akina Mwabukusi, Dr. Slaa, Mdude, Nshala, Lissu etc. Hawa walikuwa wanatumia lugha ya vitisho na matusi dhidi ya viongozi wa Serikali kuhusiana na Mkataba wa Bandari na DP World.

Wapo pia waliotumia fursa zao kukosoa bila matusi wala jazba baadhi ya vipengere kama Prof. Tibaijuka, Prof Shivji, Joseph Butiku, Jaji Warioba etc.

Hata mimi ninazo nyuzi zangu ambazo nimekosoa kwa staha tu vipengere ambavyo havina masilahi.

Kuanzia jana na leo tumetulia kusoma na kusikia clips za matusi toka kwa akina Mwabukusi, Mdude na Dr Slaa.

Nawapongeza Tanzania Police chini ya IGP Camilius Wambura na TISS kama imehusika kwa kuliheshimisha Taifa.

Bandari haijauzwa, tuachane na hii taharuki.
 
Wasiachiwe hao Hadi 2030
 
Unafiki unatutesa sana'' wa TZ, utasikia mama mi 5 tena!! Unajiuliza kwa lipo?
 
Kwahiyo mnavosambaziana hivi vikaratasi mitandaoni basi mnajiona washindi kweli [emoji1787]. Tanzania hii watu wa kufanya mnayoyaita mageuzi ya kuiondoa CCM bado hawajazaliwa sana sana mpo wajinga wajinga tu wakupiga porojo.
 
Mumeo anajua kapata mke mwenye akili kumbe hovyo kabisaaa
 
Mnajidanganya

Vita bado mbichi kabisa mnajifariji eeh

Na kwa taarifa yenu hao mliowakamata na kuwabambikizia kesi za uhaini ndio mnazidi kuchochea moto

Yajayo yanafurahisha
 
Takriban miezi 2 kufika leo media zote zilijaa mambo ya upotoshaji kutoka kwa akina Mwabukusi, Dr Slaa, Mdude, Nshala, Lissu etc. Hawa walikuwa wanatumia...
Waliokuwa wanatukana, kutisha watu na kuongea upuuzi ni wale waliohongwa na wakwepa kodi wa bandarini, ili watumie kila njia ikiwezekana hata matusi ili kuifanya serikali ishindwe au kusitisha mkataba.

Kuna watu humu mtandaoni walikuwa wakiandika kila kauli chafu iliyokuwa ikitolewa na mwanasiasa fulani, na walishangilia na kufurahia kauli zile.

Leo kibao kimegeuka watoa kauli wanafinywa, afu waliokuwa wanafurahia kauli zile wanalia na kulalamika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…