Hongera Diamond kwa release ya Utanipenda, umenishika Nifah!

Sasa moyo wangu na nifah unafanana kwani kila mtu na mapenzi yake mtu anabadilisha dini na inakuwa kawaida itakua kuhama team kiba

Mkuu kwema??? umemuona sepenga anavyoshusha mashairi #UTANIPENDA kama katunga yeye vilee

https://www.instagram.com/p/_TZEUPKU-x/
https://www.instagram.com/p/_TZEUPKU-x/
 

Diamond amekusikia nifah👡
 
Last edited by a moderator:
Sasa moyo wangu na nifah unafanana kwani kila mtu na mapenzi yake mtu anabadilisha dini na inakuwa kawaida itakua kuhama team kiba
Hajahama timu kapenda wimbo,sasa tatizo liko wapi ??????
 
Verse1.
Oh ghafla visenti sina nimerudi tandale,
nimeshindwa kulipa bima, nimeuza madale,
redio nyimbo wamezima tv ndio hatare,
umeneja umebaki jina,hanitaki ata tale,
oh shabiki zangu walionisifu kwa maneno matamu,
leo maadui zangu, ni mitusi tu kwa instagramu,
eeh kimwana si dadangu, ati naye hanifahamu,
ata harmonize nikimpigia,ananifokea kama salaamu,
na magazeti nyumbani kwa kukuza habari si unajuaga,
utasikia tafarani ati mondi kwa zari amemwagwa,
na venye nilivyo mnyonge tabia ya kuwajibu sinaga,
kama naiona michambo ya madem wa zamani,niliowapitiaga

verse2.
ooh ninayosema yana maana ,
sababu hakuna anayejua kesho,
anayepanga ni rabana,
ila ameficha ni confidential,
ukisali omba sana,
mumeo nisije kuwa kichekesho,
maana rafiki wa jana ,
ndio adui mkubwa kesho,

(chorus)
La x7
Oh Je utanipendaga,
La la la la la la la
Au nawe utanimwaga,
La la la la la la la
Ati utanipendaga,


Verse3.
Ooh bado nawaza sana
zile tuzo mashauzi airport
Je ntapofika tama,
utadiriki ata japo kunipost,
pindi show zimekwama ,
na nikipata sijazi ni mikosi,
oh jahazi limezama,
mola ninusuru baba,

verse 4.
kama namwona mwanangu roho yangu,
tiffah dangote ,anakwenda na mamangu,
kwa jakaya kikwete anafukuzwa atoke,
husilie sandra wangu,mboni yangu,
jikaze husichoke,uenda kesho zamu yangu,
nitavuma tena mambo yanyooke,

na magazeti nyumbani kwa kukuza habari si unajuaga,
utasikia tafarani ati mondi kwa zari amwagwa,
na venye nilivyo mnyonge tabia ya kuwajibu sinaga,
kama naiona michambo madem wa zamani,anikerage

la la la la la la la
la la la la la la la
la la la la la la la
la la la la la la la

verse 5.
kama namwona mwanangu roho yangu,
tiffah dangote ,anakwenda na mamangu,
kwa mkubwa fella anafukuzwa atoke,
husilie sandra wangu, mboni yangu,
jikaze husichoke,uenda kesho zamu yangu,
nitavuma tena mambo yanyooke

verse 6.
ooh ninayosema yana maana ,
sababu hakuna anayejua kesho,
anyepanga ni rabana,
ila ameficha ni confidential,
ukisali omba sana,
mumeo nisije kuwa kichekesho,
maana rafiki wa jana ,
ndio adui mkubwa kesho
 
Sasa moyo wangu na nifah unafanana kwani kila mtu na mapenzi yake mtu anabadilisha dini na inakuwa kawaida itakua kuhama team kiba
pwilo my dear, relax....
Nisome vizuri tena,wala sijaedit hii post tokea nilivyoipost.
Jifunze kusoma post yote kabla ya kucomment.
 
Last edited by a moderator:
pwilo my dear, relax....
Nisome vizuri tena,wala sijaedit hii post tokea nilivyoipost.
Jifunze kusoma post yote kabla ya kucomment.

Afu mbona kawaida tu, kama wakina swiz beats wenyewe wanacheza nyimbo za Diamond, sembuse mtoto wa Magufuli?
 
Last edited by a moderator:

Wimbo wenyewe mbona mbaya tuuh...! We nifah smd bado una mapenzi na diamond siyo wimbo...!
 
Last edited by a moderator:

Asubir video bora utunzi ni Barnaba na kiba mwisho
 
Last edited by a moderator:
Wimbo wenyewe mbona mbaya tuuh...! We nifah smd bado una mapenzi na diamond siyo wimbo...!
Nachelea kusema hujui mziki mzuri,huu wimbo nimeukubali sanaaaa.
Diamond simpendi na hata katika post yangu nimesisitiza hilo.
Baniani mbaya,kiatu chake dawa....
Sifa zake tumpe tu jamani,hatutopungukiwa na chochote kwa kusema ukweli.
 
Last edited by a moderator:
huu wimbo sio kwamba amejiimbia yeye bali hata sisi unatugusa... Wapo wanaotusifia kwa sasa, je tutakapoanguka Wataendelea kutusifia na kutusapoti kwa Hali na Mali? Jiulize na Uanze kuusikiliza huu wimbo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…