Hongera ITV kumhoji Tundu Lissu. Hongera sana Tundu Lissu kuzungumza kistaarabu kwa lugha za staha. Ruksa kuhisi chochote, sio fair kutaja majina!

Hongera ITV kumhoji Tundu Lissu. Hongera sana Tundu Lissu kuzungumza kistaarabu kwa lugha za staha. Ruksa kuhisi chochote, sio fair kutaja majina!

Bw Mayalla mara nyingi hauko huru kifikra tena ni mtu una hofu.Kwanini unamsemea lissu.eti hana ushahidi.kwanini ukaweza kujua kwamba alietajwa anasingiziwa wewe na mtajwa mnafanya kazi kitengo kimoja?
Kwasasa wewe ni mwandishi kanjanja mwanaccm.Lissu unamchukulia kwamba hajui anachoongea.Aisee pole sana.
 
Kama kuna mdau anaweza kutuwekea ningefurahi sana.Wengine hizi local channel huu ni mwaka wa nne sijathubutu kutazama wala kusikiliza.
 
Bado bado sjakuelewa unasmamia hoja gani? Maana umesema mtu ukiongea kitu na ukashindwa kuthibitisha, utaitwa muongo, then mwisho umemalizia kwa kusema katika kipindi hiki cha kampeni za kutafta kura ni ruksa kwa wagombea kuongea uwongo! Je Lissu sio mgombea? Je hatuko kipindi cha uchaguzi?

After all nondo alizoporomosha Lissu hata wewe umemkiri kuwa ni jembe, Hivyo basi hakuna haja ya kujaribu kujenga na kukuza hoja mpya, wewe uliyemuelewa vema Lissu waeleweshe na jamaa zako wa Lumumba wanaojaribu kuziba macho yao huku masikio yao bado yanamsikiliza Lissu wamuunge tu mkono hakuna jinsi!
 
Kwa hiyo unaamani angalao pachimbike.Fikiri kwanza.
Siamini kwenye kuchimbika,na sio mimi tu hata watanzania hawaamini kwenye kuchimbika.
sababu zenu za kuchimbika hazina mantiki kabisa ndo maana watanzania hawana mpango na kichimbika.

Amani kwanza,changamoto zingine zitatuliwa taratibu pakiwa na amani na utulivu mpaka tutafika Ishallah.
 
Pascal Mayalla,

Unasema kazi ya Rais ni kuteua lkn si kutengua, unamaanisha Rais Huyu wa akina Le Mutuz au Rais yupi?

Alimtengua Mangu, hadi Jeshi limemuaga Last week baada ya kustaafu rasmi

Alimtengua Prof Benno Ndulu, baada ya Ndulu kukataa Ujinga ujinga kwenye uendeshaji wa Uchumi wa nchi

Alimtengua Prof Assad, baada ya Prof kukataa Wizi kwenye Fedha za Umma

Na wengine kwa maelfu...amebaki na praise singers tu wa kutoka majalalani wasiokuwa na akili wala maarifa yoyote!
 
Kwani kura zishaibiwa marangapi na hapakuchimbika shimo?
Mbona mlipigwa pini kufanya siasa miaka mitano na hapakuchimbika?
Hamasa tu za kwenye mitandao hamna lolote ni ushuzi tu.
Duh! Hivi kumbe ni kweli huwa mnaiba kura?! Sikuwa na uhakika.
 
Pascal Mayalla,

Mzee wa kuandika UTOPOLO, naona umekuja kivingine sasa. Lissu hakamatiki kwasasa, nafasi pekee mliyoipoteza ni ile ya kutaka kumkata asigombee.
 
Freedom of speech/expression maana yake nini? Vipi kuhusu transparency? Unataka afichefiche nini?

Bora aanike tu wote tufahamu.
 
Pascal Mayalla,

Umecharanga sana labda tulijadili hili neno KUHISI ninavyojua mm ukimuhisi mtu huwezi kumtaja na ukimtaja mtu una uhakika.

Sikusikia eneo lolote lissu alisema ana hisi ila alitaja direct na ukisha taja direct unaushahidi la muhimu ungemuuliza akupe ushahidi na kwa kuwa ni mwansheria angekutosheleza.

Pia umesema uhuru wa kuongea kwamba si kila kitu utaonge mbona hilo linajulikana? Yy kamaananisha uhuru wa kuongea mambo ya kweli.
 
Hivi na wewe Mayalla hv ukiwa mwanaccm akili zinakuruka????Hv kusema jiwe ndio alieamuru lisu apigwe risasi ni uongo???KWANI WEWE JPM HUMJUI?ALIVYO NA SIFA NA HATAKI KUKOSOLEWA SASA UKIFANYA TOFAUTI NA MATAKWA YAKE NINI KITAKUTOKEA???HUYO ASSAD HUJAONA ALIVYOSONGWA????TUACHE UNAFIKI AISEEH KWENYE UKWELI!!
 
Nimesha subscribe ITV online. Kumbe ina mtangazaji kichwa namna hii. Yule Dada yupo Bright sana. Very cool and focused. Hongera ITV

Kiukweli huu ni mwaka wa tatu tangu niiangalie itv. Nimeipenda bureeee
Hata mimi aisee na ngoja nika isubscribe na mimi.
 
Wanabodi,

Hili ni bandiko la pongezi kwa ITV kuwa ndio the first mainstream TV Station kumhoji Tundu Lissu. Huu ni mwanzo mzuri, TV nyingine zifuate.

Pia nampongeza Mhe. Tundu Lissu kuzungumza kistaarabu, ametumia lugha za staha, amemwaga sera.

Kati ya freedom zote, freedom ambayo ni absolute freedom is the freedom to think, uhuru wa kufikiri ndio uhuru pekee ambao hauna mipaka, mtu unaruhusiwa kufikiri lolote, lakini sio uhuru wa kuongea lolote.

Nimemsikiliza Tundu Lissu katika
mahojiano haya, amezungumzia sera nzuri za Chadema, generally kipindi hiki ni kizuri, kimeijenga ITV na kimemjenga Tundu Lissu, but...
Naomba hapo kwenye but nisiseme kitu kwasababu siku hizi, mimi ni kada.

Kitu pekee Lissu alichoharibu, ni kutaja majina ya watu, anaowahisi wanafanya mambo fulani ndivyo sivyo!. Nimesema kuhisi ni sawa lakini usitaje hadharani majina ya hao unawahisi, ukiambiwa thibitisha, ukashindwa utahesabika ni muongo!.

Kumhisi mtu yoyote au kumshuku mtu yoyote is your right, lakini kumtaja hadharani kwa majina huyo unayemhisi, is not right unless una ushahidi usiotia shaka, na ukiitwa kuthibitisha, utathibitisha pasipo kubabaika wala kujiuma umma.

Katika kipindi cha leo, kuna jina la mtu, Tundu Lissu amemtaja, na kumsingizia kuwa kabla hajafanya maamuzi yoyote ni lazima kwanza amuulize aliyemteua!.

This is not right, ofisi ile ni independent, kumsingizia yule aliyemsingizia, tena kwa kumtaja jina kuwa hawezi kufanya maamuzi yoyote hadi amuulize aliye mteua kama uamuzi huo utamfurahisha, is not right.

Kwa mujibu wa katiba yetu, wakuu wa Taasisi zote za umma wanateuliwa na rais. Kati ya taarifa hizo, kuna Taasisi ni independent, rais anaweza kukuteu tuu lakini hawezi kukutengua, Taasisi hizo ni pamoja na Mahakama, Ofisi ya CAG, Gavana wa Benki Kuu, Tume ya Haki za Binaadam na Utawala Bora, na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, nafasi zao zinalindwa na kitu kinaitwa security of tenure. Rais anaweza kumteua tuu mtu kama Jaji Mkuu, CAG, Msajili wa Vyama, lakini hawezi kumtengua. Hivyo kitendo cha Tundu Lissu kumsema mteule fulani hawezi kufanya maamuzi mpaka amuulize aliyemteua, sio kumtendea haki mteule huyo!.

Alichosema Lissu is as if, kwa vile wakuu fulani wameteuliwa na rais, hivyo kazi yao ni kufanya maamuzi ya kumfurahisha rais, kitu ambacho sii kweli.

Mfano ni mimi mwenyewe, baada ya Mkuu fulani kusema hadharani kuwa fulani alimpigia simu kumuuliza aumteue nani kwenye issue fulani. Mimi nikauliza, kitu fulani, niliitwa Dodoma kuhojiwa na Kamati fulani kwa swali langu hilo!. Sasa leo Tundu Lissu amesema mtu fulani hawezi kufanya maamuzi hadi amuulize aliyemteua!, jee akiitwa kuthibitisha, ataweza?.

My Take.
Natoa wito kwa wanasiasa, japo kwenye kampeni uongo unaruhusiwa na propaganda za kisiasa rukhsa katika kutafuta kura, mnapo nadi sera zenu, epukeni kutaja majina ya watu katika vitu ambavyo ni hisia tuu!.

Namalizia kwa kutoa hongera kwa ITV, hongereni sana, mmetusaidia kumsikia Tundu Lissu na kumsililiza bila kukereka.
Pia nampongeza Tundu Lissu kuzungumza kwa utulivu katika mahojiano hayo, bila kusahau kumpongeza Mtangazaji Farhia Middle, kwa maswali mazuri kwa Tundu Lissu, hiki ni kipaji kingine kizuri katika utangazaji, ITV imekiibua, na hongera kwa menejimenti ya ITV, kumwalika Tundu Lissu na kumpatia Airtime ya kutosha, katika zama hizi za Tanzania ya sasa, it's a bold decision!, mimi niliulizaga tuu swali mahali, kilichofuata..., only God knows, hadi ilibidi...

Pia nasisitiza the freedom to expression, ruksa kuhisi lolote, rukhsa kumhisi yoyote, lakini sio fair kutaja majina ya watu kwa jambo la hisia tuu kwa kumhisi. Niliwahi kushauri humu kuwa sio lazima mtu kuusema kila ukweli unaoisikia au kuujua!. Kwa mfano kuna member mwenzetu humu, anamjua kiongozi fulani kuwa sio..., akanitajia, na mimi nikajiridhisha kuwa alichokisema ni kweli lakini ukweli huo hauhitaji kusemwa!.
Swali la Morality: Je ni lazima kuusema kila ukweli unaousikia au tutangulize mbele maslahi ya Taifa?

I wish him, Tundu Lissu, all the best katika ugombea wake, maana mimi ni miongoni mwa watu tuliomchagiza Lissu kugombea ili kuuchangamsha uchaguzi wa urais.

Uchaguzi 2020 - Tundu Lissu ndiye asimame na Magufuli 2020? Ameonyesha uwezo zaidi ya Magufuli!

Paskali
Tobo ni kichaa anayejua kuoga tu
 
Back
Top Bottom