Hongera JF kwa Whistleblow, JF tubadilike, tusichafue majina ya Watu kwa tuhuma za Hearsay zisizo na Uthibitisho, Ukituhumu, Weka Uthibitisho

Kuna kundi la VIJANA walioibuka kufanya siasa za kishabiki (siasa za kimakundi-makundi).

 
Binafsi naona kama hakumtendea haki ingawa inawezekana akawa na uhakika kwa alicho kiandika.
Mkuu Mmawia , uko right ndio maana nimeshauri, ukituhumu kama una uhakika, leta na ushahidi, au uthibitisho, vinginevyo leta tuu tuhuma as a Whistleblowing lakini usitaje majina ya mtuhimiwa.
P
 
kuchafuana ndio imekuwa tabia ya Watanzania walio wengi, na Tabia hii imeeenea kila mahali, sio tu kwa mawaziri bali tabia hiyo imeshamiri maofisini hasa ktk ofisi za umma.

watu wanachafuana sana huko, yaani ni mwendo wa kuangushana ili mwengine apande.

Jambo la msingi ni kwa viongozi wenye dhamana wawe waangalifu ktk kuchukua hatua, wasi sikilize majungu.

majungu yanaharibu na kuwapoteza watendaji wazuri na waadilifu.
 
Unathibitishaje wizi, hapa sio mahakamani tuhuma wana_whistleblow TAKUKURU watathibitisha.


Nani alijua kuwa Ole Sabaya ni jambazi, namuhujumu uchumi?


Acha watu WAPULIZE FILIMBI Mgambo watafanya kazi yao.

Ana conflict of interest madini maana tunasikia yeye pia anafanya biashara ya madini.
 
Umeeleweka Mkuu,nakubaliana na wewe,tuhuma ziwe na vivid evidence na sio tu mtu anatuhumu kwa hisia tu au anayetuhumu nae hizo tuhuma amezisikia sehemu na akawahi kuja kuanzisha Thd JF ili aonekane nae anajua,
 
Pascal Mayalla
Inamaana alichosema waziri Mchengerwa ni uongo?
Mkuu Babu Ochu , it's very unfortunately sijasikia Waziri Mchengerwa amesema nini, inaweza kuwa ni kweli au ni uongo, kama ile issue ya kuumwa kwa JPM, viongozi wetu wakubwa tuu, walitangaza uongo mkubwa wa wazi hadharani mchana kweupe, hadi kifo kilipo waumbua, what do you expect to the rest?. Please share alichosema ili tuki scrunize tujue ni kweli au uongo.
P
 
Uzalendo unapimwa kwa kusikiliza? Mpiga mbiu kadai madini kusafirishwa kwa njia ya panya hili nalo linahitaji detail zaidi? Maana njia za panya ni mipakani na kutouza kupitia masoko ya madini. Sasa haya hayajulikani? Kama hayajulikani mbona Waziri ofisi ya mkuu wa nchi kasema kuna wizi unafanyika?
 
Nanyinyi wafuasi wa Dikteta muache kumchafua waziri wa Nishati, kutwa mnamchafua bila uthibitisho wowote,kisa tu ndugu yenu katolewa hiyo wizara
 
Kama unaamini viongozi walitangaza uongo hadharani kuumwa kwa JPM kwanini unamuamini "kiongozi" Biteko?

Don't try to take him off the hook
 
we Ni mpuuzi,"eti nawasubiri wamtoe halafu nione watamuweka wapi"

hivi nyie misukule Ya dikteta mmerogwa au, Sasa mama atapiga chini masalia yote ya mwendazake,
 
Mkuu Mmawia , uko right ndio maana nimeshauri, ukituhumu kama una uhakika, leta na ushahidi, au uthibitisho, vinginevyo leta tuu tuhuma as a Whistleblowing lakini usitaje majina ya mtuhimiwa.
P

Naungana na wewe kwa hili.

Lkn Pascally kwa jinsi upepo wa kisiasa hapa nchini kwetu hasa kutoka ndani ya ccm kuna makundi yamezuka hasa baada ya kifo cha marehemu magufuli.

Kuna makundi yanaendeleza malumbano kwa kuiona awamu ya 5 ilikuwa mzuri na imara kuliko awamu ya 6 na watu wanaongea bila ya uoga.

Binafsi naona mh Biteko anaingizwa kwenye hizo tuhuma kisa asili yake ya alipo pata huo uwaziri na wapi alipo zaliwa .

Siamini kama utanielewa ila hayo ni mawazo yangu binafsi.
 
Mkuu denooJ , thanks for this, ila sijapata bahati kumsikia waziri mkwe kasema nini!, please share links.
P
 
Ni kweli tuache Majungu ila huyo Waziri wa Fedha ang'oke hali ni mbaya sana Mtaani.
 
Umenikumbusha 2015 wakati Lissu anampigia kampeni Lowassa, alisema kama hivyo kwamba kama Lowassa fisadi mbona hajapelekwa mahakamani.
 
Tutangulize maslahi ya taifa kwanza, makundi, siasa za chuki Ni laana kwa taifa letu. Dotto Ni MTU sahihi alipo ana maono na tafsiri Bora Sera yetu madini. Apewe ushirikiano Karibuni sector madini inachangia Sehemu kubwa GDP, miaka michache ijayo tutaachana na adha hisani Kama hii ya 1.3T ya uviko.
Zipo fursa ndogo kuambatana na wizara husika Ni motisha kwake tuache wivu wa kijinga.
 
Mkuu Mmawia , nakuelewa sana kuliko unavyodhani. Kwanza ni kweli awamu ya 5 hawakuwa malaika, na ni kweli kuna watu waliteuliwa kwasababu zile za kanda pendwa, ni kosa kufanya nepotism, kwa kuwateua watu wa kabila lako, lakini sio wateuliwa wote wa kabila hilo wameteuliwa kwa nepotism, walioteuliwa kwa kubebwa tuu, halafu can't perfom, can't deliver, ni right kutumbuliwa, lakini hii witch hunt kuwa target wote wa kanda pendwa , hata wale the clean ones who delivers, kwa kuwapikia majungu, kuwazushia tuhuma za uzushi, uongo, fitna na majungu, halafu wakasikilizwa, karma haitakubali, karma hainaga mswalie Mtume. Watu watuhumiwe kwa haki na waadhibiwe kwa haki na sio kimajungu majungu. Mimi ni muumini number 1, kuwa hakuna kitu kinachoitwa the "Sukuma Gang".
P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…