Hongera JF kwa Whistleblow, JF tubadilike, tusichafue majina ya Watu kwa tuhuma za Hearsay zisizo na Uthibitisho, Ukituhumu, Weka Uthibitisho

Yes ataondoka na kila mtu ataondoka, hakuna atakayeishi milele. Hoja yangu hapa ni watu watuhumiwe kwa tuhuma za haki, na ikibidi waondolewe, then, waondolewe kwa haki kwa tuhuma za ukweli na sio waondolewe kwa kupikiwa majungu.
P
Mwendazake zake wakati anaondoa watu bila hata sababu za msingi, mlikuwa mnademka mitandaoni kumsifia na kumuabudu,,
We ndio ulikuwa mmoja wanaodemka kufurahia watu wakitumbuliwa enzi za mwendazake, wakati Nape anapigwa chini ulikuwa mmoja wa watu waliofurahia Sana
 
Kwa hiyo tukiambiwa Watu8 ni fisadi jambo la kwanza ni kuamini uambiwaji / maelezo huo/hayo bila hata ushahidi.

Kama msimamo ndiyo huo kama taifa, basi tufute dhana ya ushahidi.

Mkuu anza kwanza kusoma mstari wa kwanza kwamba katika nchi zetu hizi za kiafrika kuna mstari mwembamba mno kati ya mtu fisadi na mtu safi...

Kwa mantiki hiyo, ndipo mimi binafsi maamuzi yangu huegemea kuamini mtuhumiwa wa ufisadi kwa asilimia kubwa kama zote huwa ni kweli...

Hii mifumo ya kisheria haiathiri maamuzi yangu kwa kuwa sheria zipo, mahakama zipo na bado tunaendelea kufisadiwa huku tukiendelea kukusanya ushahidi...

Hizi nchi zetu kuna tabaka la watu lipo juu ya sheria, na jambo hili hatuwezi kulibadilisha katu, labda tubadilike na tusiwe Waafrika...
 
Ndiyo umepewa kazi ya kumsafisha?

Wangapi humu wametuhumiwa kwa namna hii hii aliyotuhumiwa Doto Biteko, mbona hukuwahi kuweka bandiko?

Ukisikia unafiki, ndiyo huu uliouweka hapa.

January anawekewa tuhuma humu kila siku. Mara sijui anataka mafisadi wauze majenereta, kuna uthibitisho?

Tundu Lisu, mara amehongwa na Acacia, kuna uthibitisho?

Rais Samia, mara amehongwa na mabeberu, kuna uthibitisho?

Zito mara amehongwa, kuna uthibitisho?

Dr. Slaa alihongwa na Serikali, kuna uthibitisho?

Lipumba anatumiwa na Serikali, kuna uthibitisho.

Mbowe ni wakala wa mabeberu, kuna uthibitisho?

Mabeberu wanatuibia, kuna uthibitisho?

Tupo kwenye vita vya kiuchumi, kuna uthibitisho?

Hak wote hatujawahi kumsikia mnafika Pascal Mayala akikemea ila tu tuhuma dhidi ya Biteko, tena kwa kiasi kikubwa ni tuhuma ambazo zina maelezo yanayojitosheleza namna uovu anavyoutenda.

Wewe ukiamua kumsafisha, kumpamba au kumtetea, endelea, lakini usiwapangie wanaomtuhumu. Ukweli ni kuwa hakuna kitakachofanywa dhidi ya Doto kwa vile tu watu wametuhumu. Kama kutakuwa na hatua, ujue ni baada ya wanaomchukulia kujiridhisha na tuhuma hizo.¹
 
Very affordable adhabu. Mtu wakati huo keshajinufaisha na mabilioni yaliyotakiwa yakafanye maendeleo yanayogusa maisha ya watu.
 
Nadhani zile story kuwa kuna chuki imepandikizwa- hii ndiyo maana yake.
Kwani kama si chuki ni nini basi?

Sad kwamba hakuna anayejaribu kuangalia kama kuna ukweli katika hili isipokuwa kuna ubishi juu ya hizi chuki zinazosemekana kuwa zimepandwa.

Pengine imeachwa ijisolve naturally.
Hivyo tusubiri.
 
BITEKO siyo mtu safi hata kidogo.

Nenda kafanye utafiti kwa kuongea na wafanyabiashara wakubwa wa migodi wakueleze namna Dotto anavyokusanya bongo bila aibu kutoka kwao.

Vilevile, upendeleo wa wazi na tuhuma zilizo bayana kuwa ana maslahi na kampuni ya usafirishaji mafuta ya mitambo katika mgodi wa GGM ni uchafu kwake na inamuondolea kabisa heshima yake kwa jamii.[/QUOTE]Mimi binafsi, siyo kwa kusikia kwa watu wa pembeni, bali wahusika wenyewe waliolazimika kutoa pesa kwa Biteko ili wapate eneo la kuchimba ambalo lilikiwa ni eneo la kampuni moja. Walimpa akichotaka na leo wanachimba. Mwenye eneo anaendelea kupambana kuona kama atarudishiwa, sijui kama atarudishiwa. Ninao mfano mwingine vivyo hivyo, wahusika wenyewe wanaeleza walivyolazimika kutoa pesa ili wapate maeneo ambayo hayakuwa yao.

Uthibitisho hauwezi kupatikana hapa, huwezi kuweka majina ya watu waliotoa pesa hapa, ila vyombo vinavyohusika vifanye kazi, vimchunguze Waziri Biteko. Kwa hakika, bila chuki wala nia ya kisasi chochote, Biteko siyo msafi. Kwenye vyombo vya uchunguzi, watu waliolazimika kutoa pesa, wataweka wazi. Uchunguzi ufanyike.
 
Umeongea la maana sana sijui kwa sababu home boy ndio anasakamwa?

Kuna video clip ya sekunde chache tu inasambazwa, watu wenye akili timamu kila ukiitazama video hiyo ni vigumu kumtambuwa muhusika, lakini kuna kundi la watu wanatulazimisha tuamini huyo ni Kabwili ya Yanga anatuhumiwa ushoga, hivi kwa ushahidi kama huo ni haki kweli kumpa mtu tuhuma nzito? Au ndio bullying?
 
Kumtetea Doto na kumtangaza kuwa ni mzalendo, hukustahili kufanya. Aheri ungenyamaza tu, kwa vile hujui kama ni msafi au corrupt. Lakini nakuhakikishia ukifanyika uchunguzi, utajilaani kumtetea mtu wa namna hiyo. Hujui hata anavyotoa pesa kwa watu mbalimbali ili wamsafishe kutokana tuhuma nyingi nzito, na nyingine hazijawahi kuandikwa hata humu? Sasa hivi anahangaika sana, kwa kuwatumia watu mbalimbali kutoka kwenye ofisi kubwa za uongozi, ili wamsafishe dhidi ya uchafu ambao amekuwa akiufanya.
 
"Mifano mirahisi kabisa, kuna nyumba ilikamatwa ikiwa imejiunganishia bomba la mafuta hapa Dar, waziri mkuu na IGP wakasema ndani ya siku 7 watatoa ripoti ya jambo lile, lakini mpaka leo kimya"


Hivi hii habari iliishia wapi? Iliishaje?
 
Wewe tuambie ni mfanyabiashara yupi na yupi kaombwa pesa ili tumface direct.otherwise haya uliyoandika bado ni majungu.[/QUOTE]Upo sahihi sana. Jana tu niipata nafasi ya kuongea na mwanafamiia wa huyu aliyepewa tenda ya kupeleka mafuta GGM kwa msaada wa Biteko. Mimi mwenyewe nilikuwa siamini. Nilishangaa huyu mwanafamiia alipotamka kuwa ni kweli.

Kukifanyika uchunguzi na taarifa ikawekwa wazi, wengi watashangaa jinsi huyu bwana alivyofanya tangu kifo cha Magufuli. Anatafuta pesa kwa namna isivyo halali kwa kiwango cha ajabu na kushangaza.
 
Yes ataondoka na kila mtu ataondoka, hakuna atakayeishi milele. Hoja yangu hapa ni watu watuhumiwe kwa tuhuma za haki, na ikibidi waondolewe, then, waondolewe kwa haki kwa tuhuma za ukweli na sio waondolewe kwa kupikiwa majungu.
P
Ebu eleza, ni tuhuma ipi dhidi ya Biteko ni majungu? Kukosekana kwa kielelezo cha kuthibitisha hapa JF, haimaanishi taarifa hiyo ni majungu, sawa na ilivyo kama mtu akaleta tuhuma hapa, si lazima tuhuma hiyo iwe ni jambo la kweli. Ndiyo maana inaitwa tuhuma.
 
"Mifano mirahisi kabisa, kuna nyumba ilikamatwa ikiwa imejiunganishia bomba la mafuta hapa Dar, waziri mkuu na IGP wakasema ndani ya siku 7 watatoa ripoti ya jambo lile, lakini mpaka leo kimya"


Hivi hii habari iliishia wapi? Iliishaje?
Limepotezewa tayari wakiamini tumesahau.
 
Ila Mkuu,kwamba vyanzo vyangu vimeniambia kwamba kijana wangu anakwapua mazao na kuuza shambani nikae kimia mpaka kudhibitisha, na KAZI ya vyombo wa uchunguzi kuoji KAZI yao ni ipi?

Binafsi nitatoa malalamiko ,na vyombo husika vinisaidie kudhibitisha Kama kweli au la,
 
Huyu ni mtusi pandikizi, na wamejana huko Geita,Mwanza, Kagera, Ukerewe, na sehemu za mkoa wa Mara.
 
Ukiniambia kuwa Magufuli alijitahidi kuwabana wanaotorosha madini, nakubaliana na wewe kwa 100%. Inaonekana Biteko alilisimamia hilo, siyo kwa sababu ndicho alichokiamini, bali ni kwa sababu ndicho kilichomhakikishia kuendelea kuwa Waziri. Kama ingekuwa hicho ndicho alichokuwa akikiamini, asingebadilika kwa kiwango hiki cha sasa, mara tu baada ya marehemu Magufuli kuondoka Duniani.

Hii inaonesha mawaziri na watendaji wengi wa marehemu, waliyokuwa wanayafanya ni kwa sababu ya kumwogopa marehemu, lakini kiasili kwenye mioyo yao, wengi ni corrupt kupindukia, Biteko ni miongoni. Nazungumza nikiwa na uthibitisho wangu moyoni. Ukihitajika panapostahili na palipo salama, tutapeleka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…