Hongera Kinana, CCM tunayoifahamu imerudi!

Hongera Kinana, CCM tunayoifahamu imerudi!

Hauko siriaz wewe,Kinana huyu tunaemjua yakuwa ndie kinara wa sisi ndio Ccm wenywe,ambao wapo kupora rasilimali za Taifa tu,sio kuwakomboa wananchi,timu yao ni hii hapa,
JK
NAPE
MZEE MAKAMBA
JANUARY
MEMBE
LOWASA
na washirika wao,hawa ndo tabu,shida kwa Taifa letu
Tatizo lako unaona CCM ya ndugu yako chini ya wale wasijulikana ya unyang'anyi wa wafanya biashara watesi wa akina Lissu, Zacharia na wengine wengi haitowi kasoro kwa vile na wewe mwenyewe labda ulikuwa unanufaika.

Leo akina Musiba wamebaki kulia lia tu akina Makonda hali ni mbaya Sabaya na wenzake wanajijua wenyewe, hawa walikuwa mawazo ya kijinga kabisa, walijua kuwa Magufuli atakuwa wa milele.
 
Ndio ni kweli, zile ndizo zilikuwa harufu za ubabe, udikteta usikuma na ushamba wa kusukuma. Maana haikuishia hapo tu mwendazaka pia aliweza kuthubutu kusema serikali ya Magufuli kitu ambacho hata Hon Mkapa alikikemea kwa nguvu sana.

Alichokuwa anatakiwa akifanye ni kuandika chagua CCM chagua Magufuli.

Kiukweli tangu aondoke mwendazake wasiojulikana wametoweka.
Wale vijana wa5 wambao mamazao wanalia walichukuliwa na wasiojulikana unawajua walipo?

Nakukumbusha tu kuwa ile kazi ya kuprint mabango 2015 hakuifanya Magufuli mwenyewe, ila mwenyekiti wa chama JK na timu yake ndo wakijua wakaprint wapi mabanngo na waandikaje!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nyie wenyewe CCM ndio mlikiri kuwa hamna budi kwenda na mwendazake ili kuokoa chama. Na mabango 2015 mlibadilisha ikawa sio chagua CCM Bali chagua Magufuli[emoji1787]
Lakini pia nyie si mlizomeana ukumbini huko Dodoma? Mkasema hamna Imani na mwenyekiti?
Mwendazake wala asingepita hakuwa na issue.Tangu akiwa Waziri alikuwa na vi elements vya udikteta dikteta.
Sema kosa la kumkata Lowasa kwa kumuonea ikapelekea wafuasi wake (wajumbe) kulipiza kisasi kwa kumnyima kura the next most competent candidate ambae waliona anabebwa na wenye MAMLAKA.
 
Kwa hakika sie CCM, hasa tuliokuwa wanachama waasisi, tumefurahi sana kurudi kwa Kinana uongozini CCM.

CCM ya hoja,
CCM ya mshikamano
CCM ya umoja
CCM ya kutetea haki na misingi ya ubinadamu.
CCM ambayo hata kumpinga kiongozi kwa hoja huna wasiwasi wa kutembelewa na wasiojulikana.
CCM ya kuheshimu kila binadamu
CCM iliyoondoa ukanila
CCM ya kudumisha muungano

Hii ndiyo CCM tunayoifahamu.

Karibu tena Omrade Kinana.
Ndiyo maana hujui hata kuandika neno Comradi. Akili finyu tu
 
Kwa hakika sie CCM, hasa tuliokuwa wanachama waasisi, tumefurahi sana kurudi kwa Kinana uongozini CCM.

CCM ya hoja,
CCM ya mshikamano
CCM ya umoja
CCM ya kutetea haki na misingi ya ubinadamu.
CCM ambayo hata kumpinga kiongozi kwa hoja huna wasiwasi wa kutembelewa na wasiojulikana.
CCM ya kuheshimu kila binadamu
CCM iliyoondoa ukanila
CCM ya kudumisha muungano

Hii ndiyo CCM tunayoifahamu.

Karibu tena Omrade Kinana.
Ni Wakati wa CCM ya kinana, Kama Taifa tuliposhuhudia mauaji ya Kinyama ya Mwangosi, Machinga Moro, Mabom Olasit, Kumwagiwa tindikali kwa Saidi Kubenea wa Mwanahalisi halisi acha hii iliyochakachuliwa na kuumizwa kwa Absalom Kibanda.
Ni demokrasia ya Wakati huo iliyosababisha kuvamiwa kwa Mikutano ya hadhara ya CDM Songea, Morogoro na Arusha na kusababisha mauaji na maumivu kwa wapigania demokrasia ya kweli .
 
Sasa ni mwendo wa kutetema tu.
Maana timu sasa imeeenea kasoro kipa tu labda.
 
Mwendazake wala asingepita hakuwa na issue.Tangu akiwa Waziri alikuwa na vi elements vya udikteta dikteta.
Sema kosa la kumkata Lowasa kwa kumuonea ikapelekea wafuasi wake (wajumbe) kulipiza kisasi kwa kumnyima kura the next most competent candidate ambae waliona anabebwa na wenye MAMLAKA.
Hapo unajichanganya sasa, watu walikuambia hao chama kilitaka kuwafia. Ukasema sio kweli, ndio nikakukumbusha kuwa walienda kwa mwendazake ili kukiokoa.

Unahisi kwa nini wasingeenda na huyo most competent? Walihofu nini ikiwa walikua wanakubalika?
 
Uzuri ni kwamba kumbukumbu ya maovu ya chama chako unayo vizuri. Ila mwendazake alivunja rekodi, aliua hata ndama anayenyonya kisa tu ameshindwa kutaja jina lake vizuri.
Kwani Kinana alipokuwa katibu mkuu wa CCM kipindi cha JK hakukuwa na hivo vitu? Dkt Mvungi kauawa kipindi Kinana hayupo CCM? Je! Dkt Ulimboka alitekwa na kunyofolewa meno kipindi gani? Pinda anatoa agizo kuwa na wapigwe tu kipindi gani? Je! Yuke Mwandishi wa Habari wa Chanel Teni Marehumu Daudi Mwangosi aliuawa Iringa? Dkt Slaa alivunjwa mkono kipindi cha Bashiru eeh? Jaman mbon wasaulifu hivo? Mnaweka wapi akili zenu? Ayah matukio yapo miaka na miaka sema safari ile yaliwakuta wenyewe ambao wanajua kutengeneza maneno na kuandika stori zao kwenye vyombo vya habari!

Yani Leo ushasahau kuwa JAKAYA alitoa amri ya kufutwa kwa uchaguzi wa Zanzibar 2015 kinana akiwa ndiye katibu mkuu wa chama na Nape Katibu mwenezi! Serious leo unatarajia ushindani serious kweli! Nakushangaa sana ndugu yangu!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uzuri ni kwamba kumbukumbu ya maovu ya chama chako unayo vizuri. Ila mwendazake alivunja rekodi, aliua hata ndama anayenyonya kisa tu ameshindwa kutaja jina lake vizuri.
Sijawahi kumiliki kadi ya chama chochote ila nishatumikia chama kimoja tu kabla ya 2015, ni Chadema chini ya Makene baada ya hapo sikuitumikia CCM japo nilimkubali Magufuli.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watanzania 2025 tuna kazi ya kuirudisha tz kwa watz maana kifuatacho kinafurahisha
 
EeeenHeee Heeee!

Wewe 'jamaa' sikujua kuwa uko hivi!

Watu wa ajabu sana ndani ya nchi hii.

Kidogo unitie ngeu, shauri ya kumsema Magufuli kuwa laghai..., unakumbuka?

Mara nikakusikia na 'contractors' mnavyoneemeka, lakini hapo hapo husemi neema hizo zinapatikana chini ya Waziri yule yule uliyetaka afutiliwe mbali!

Siku hizi simsikii sana pacha wako 'Masopyakindi', kuna jambo linamsibu?

Jameni, tuweni wakweli kwa nafsi zetu, namna hii wanasiasa watakuwa wanatucheza kama mpira.

Nimeona nikujadili, badala ya mada yako, kwa sababu sijui ukweli wako upo wapi hasa na hizi mada.
@Masopyakindi
 
Ni Wakati wa CCM ya kinana, Kama Taifa tuliposhuhudia mauaji ya Kinyama ya Mwangosi, Machinga Moro, Mabom Olasit, Kumwagiwa tindikali kwa Saidi Kubenea wa Mwanahalisi halisi acha hii iliyochakachuliwa na kuumizwa kwa Absalom Kibanda.
Ni demokrasia ya Wakati huo iliyosababisha kuvamiwa kwa Mikutano ya hadhara ya CDM Songea, Morogoro na Arusha na kusababisha mauaji na maumivu kwa wapigania demokrasia ya kweli .
Pole sana kama ulimwagiwa tindikali, at least you lived to tell the tale.
Tutafutie na Ben Saanane alikopotelea kabisa.
 
Back
Top Bottom