MAAJABU YA CHUMVI
Stori kuhusu chumvi
Tunapata chumvi nyingi kwenye vyakula vyetu siku hizi.
Chumvi nyingi itasababisha shinikizo la damu, uvimbe, matatizo kwenye kibofu cha mkojo, matatizo ya moyo na orodha inaendelea.
Tunaambiwa chakula chenye chumvi kidogo au kisicho na chumvi kabisa ndicho bora kwa afya zetu.
Ukweli kuhusu chumvi:
Mpaka zama za pili za mawe (middle stone ages), hakuna chumvi iliyokuwa mbaya.
Waharifu waliuliwa gerezani kwa kupewa chakula bila chumvi, iliwasababishia kifo cha taratibu.
Miaka 2000 iliyopita, chumvi ilitumika kama hela.
Dhahabu na Chumvi vyote vilikuwa na thamani sawa.
Neno 'salary' (mshahara) linatokana na neno 'salt' (chumvi).
Hapa kwetu Tanzania, watu hutumia msemo, 'Nimekula chumvi nyingi' kumaanisha kuishi miaka mingi.
Katika siku hizo za kale, chumvi ilitumika pia kuhifadhia vyakula.
Siku hizi tunatumia rifrijereta, kwa hiyo chumvi chache inahitajiwa isipokuwa kwa matumizi machache ya kusokotea nyama.
Wanyama wote wenye damu moto, lazima wawe na chumvi ili kuishi. Ubongo wa binadamu pamoja na uti wa mgongo, vimo katika mfuko wa maji chumvi uitwao 'cerebrospinal fluid (csf)'.
Umajimaji huu huzunguka sehemu zote za ubongo na uti wa mgongo.
Sote tulitumia miezi tisa kuishi katika mifuko ya uzazi ya mama zetu inayoelea kwenye maji chumvi (amniotic fluid).
Machozi yetu ni chumvi na tunatokwa na jasho ambalo pia ni chumvi.
Mifupa yetu ina uwazi katikati yake (uboho) ambamo seli za damu hutengenezwa.
Uboho huu umefunikwa na tabaka nyingi za chumvi kalisiamu kama vile kamba inavyoshikizwa pamoja.
Kowa chumvi (salt crystals) zinashikizwa pamoja na kalisiamu, na kowa hizi ndizo zinazoifanya mifupa yetu kuwa imara, na siyo kalisiamu pekee.
Mifupa inamiliki asilimia 27 ya chumvi yote mwilini. Wakati mwili unahitaji chumvi zaidi, huikopa toka mifupani, jambo hili likitokea, kalisiamu huondolewa pamoja na chumvi na kuifanya mifupa kuwa miembamba, laini na midhaifu.