Hongera kwa walioleta uzi wa Chumvi ya Mawe

Hongera kwa walioleta uzi wa Chumvi ya Mawe

Ndiyo ni imani lakini pia chumvi hasa ya mawe ya baharini inao uwezo wa kufukuza Nguvu mbaya yaani bad energy, hata miti ukiipanda kuzunguka nyumba yako inasaidia kufukuza Nguvu mbaya (bad energy)

Ni kweli maji ya Baraka ni mchanganyiko wa maji ya mvua na chumvi ya mawe
Sawa ,amini kama unavyoamini.
 
Mungu mnamuona kwenye upande mmoja tuu? Upande mwingine daily mnasema uongo, madhulumu, mnalewa pombe, mnafanya zinaa, mnatamani wake/waume za wenzenu, mnaiba vya wenzenu nk nk...
Mkuu fafanua hapo kwenye point ya MNALEWA POMBE,

Fafanua hii hoja kwaio kama mtu atatenda wema na kufanya yampendezayo Mungu..

Akinywa mvinyo ndio ticket ya kuukosa ufalme wa MUNGU

Itapendeza zaid ukifafanua
 
Mi haya mambo yananishinda mwenzenu. Kwanza nikiwaza kufanya hivyo naogopa sana!

Ila nini, kila mtu na maisha yake na siwadharau wanaoamini tofauti na mimi.
Hupasulii wanaume nazi ili wakupende wewe? Au hauko Dar? Nasema hivi kwa sababu ndiyo mtindo wa wanawake wengi wa Dar siku hizi.
 
Hawa ni sikio la kufa kama yule mwenzao wa kansa.

Wakawaulize bibi zao chumvi ina kazi gani wataambiwa kinagaubaga.

Kamtu kamesoma shule ya kata kameishia FOM FOO kanajifanya kasomi uchwara, atii ooohh chumvi ni uchawi! Like serious, ati chumvi ni uchawii!!! 😲

Chumvi ni utakaso, inaondoa mauchafu yote ya kichawii na ya kiroho. Unakuwa msafi haswaa ndio maana hela zinatiririkaaa kama maji zinakufuata.

Hizo shule za kata zimulikwe, zinatengeneza mazuzu wanaodhani wao ni wasomi. FOM FOO uchwaraa.
I'm soleee to ask zis...je? Tufanye zile shule za feza, St Joseph, Francis, kemebos, St Mary's zinafundisha masuala ya chumvi? Unajua matumizi ya chumvi kuondoa bad energies ktk mwili wako na maisha yako kiujumla iko kiimani zaidi, sie wakristo tunaamini na iko kwenye biblia nafikiri ni wafalme wa pili sikumbuki namba ngapi nabii elisha aliondoa mapooza ktk mji ule waliokuwa wakizaa mapooza na maji yamebadilika kuwa damu, akawaambia leteni chumvi na kibeseni sjui skumbuki jina la chombo akaiweka mle na akaimwaga juu ya ile ardhi na mapooza yakakoma.....hivo chumvi ni imani zaidi
 
Back
Top Bottom