Ndugu yangu lazima tukubali kuwa Mbowe ana akili kubwa sana kuliko Lissu. Chadema halikuwa chama kikuu nchini kwa bahati mbaya; ni akili ya Mbowe. Kwani vyama vingine si vipo kwanini ni vidogodogo TU.
Hii no reform no election ni upuuzi mtupu kwangu. Issues kubwa ni kujenga hoja juu ya nini unakwenda kufanya Ikulu kama utashika dola. Uwaambie watu mpaka wakuamini ili wawe tayari kufanya lolote kama wataibiwa kura. Mama Samia anasambaza maji, umeme, pembejeo, hospital, shule, barabara, ajira, madawati, nishati safi, na masoko Kila mahali nchini, chadema itakwenda kufanya nini kama itashinda?
Lissu asifikirie kuwa watu wengi kwa maelufu na mamilioni wataandamana kudai katiba na tume huru ya uchaguzi TU bila kujua watapata nini tangible kama katiba ikibadilishwa na chadema ikishinda. Inabidi Lissu atumie muda mwingi kujenga hoja zinazowalenga wananchi wengi Moja kwa Moja badala ya kuja na hoja za kejeli, matusi, bandari, wamasai, na katiba mpya. Hakuna atamwelewa.
Trump alimshinda Biden kwa hoja zinazowalenga wamarekani wengi kama mfumko, wahamiaji, vita ya Ukraine, kupunguza kodi, kujenga viwanda, kuondoa kodi kwenye tips, kupiga vita ushoga, kuzuia kutoa mimba nk. Biden muda wote alikuwa akisema Ukraine, Ukraine, Ukraine TU. Lissu muda wote itakuwa katiba, katiba, katiba.......
.