Aaa!! CCM imeunganishwa kwa kamba dhaifu sana za majani ya migomba, ni swala la muda TU. Wanaishi kwa nguvu za dola, loopholes za katiba, uchanga wa vyama vya upinzani na uzembe wa wananchi wenyewe (hasa wasomi wetu).Kwahiyo unasemaje?
Heri chadema waliofanya uchaguzi
CCM ni mwendo wa udikteta tu hakuna hata uchaguzi
Kwahiyo wewe tulia
Kikubwa ni ushindi.
Ndugu yangu lazima tukubali kuwa Mbowe ana akili kubwa sana kuliko Lissu. Chadema halikuwa chama kikuu nchini kwa bahati mbaya; ni akili ya Mbowe. Kwani vyama vingine si vipo kwanini ni vidogodogo TU.Hyo asilimia ni wale ambao mbowe anawadai ela alzowapa
Mzee Mtei is a smart old man! Hukusema kabla ya uchaguzi na hata baada ya uchaguzi. Anaheshimu uamuzi wa wanachama. Chadema sio succos kama Mbowe alitaka watu waamini😳😳Kwani Mzee Mtei ameshasema lolote kuhusu matokeo ya uchaguzi?
Maono ya hao walioshinda ni tofauti na hao walioeashinda!! Wakina Mbowe ni mamluki wa Samia, wanakubali Samia na ccm waendeleze kuwanyanyasa wananchi milele suala ambalo halikubaliki na vijana wengi sasa!!Sio hivyo kaka, hawa 48.9% wako upande "noble", ni rahisi sana kwao kupata,10% ya watu kutoka upande wa 51.2% uliojaa "viasaka". Lengo langu ni kuwatahadharisha 51.2% waendeshe siasa jumuishi bila kusahau kuwa waliwashinda kwa kura 1.2% TU.
Hakuna chama kitaishinda ccm na Katiba hii !! Ndio maana ni muhimu kuibadilisha hii Katiba na mambo mengine yatafuata baadae! Bila hivyo tutakuwa tunatwanga maji kwenye kinu.Ndugu yangu lazima tukubali kuwa Mbowe ana akili kubwa sana kuliko Lissu. Chadema halikuwa chama kikuu nchini kwa bahati mbaya; ni akili ya Mbowe. Kwani vyama vingine si vipo kwanini ni vidogodogo TU.
Hii no reform no election ni upuuzi mtupu kwangu. Issues kubwa ni kujenga hoja juu ya nini unakwenda kufanya Ikulu kama utashika dola. Uwaambie watu mpaka wakuamini ili wawe tayari kufanya lolote kama wataibiwa kura. Mama Samia anasambaza maji, umeme, pembejeo, hospital, shule, barabara, ajira, madawati, nishati safi, na masoko Kila mahali nchini, chadema itakwenda kufanya nini kama itashinda?
Lissu asifikirie kuwa watu wengi kwa maelufu na mamilioni wataandamana kudai katiba na tume huru ya uchaguzi TU bila kujua watapata nini tangible kama katiba ikibadilishwa na chadema ikishinda. Inabidi Lissu atumie muda mwingi kujenga hoja zinazowalenga wananchi wengi Moja kwa Moja badala ya kuja na hoja za kejeli, matusi, bandari, wamasai, na katiba mpya. Hakuna atamwelewa.
Trump alimshinda Biden kwa hoja zinazowalenga wamarekani wengi kama mfumko, wahamiaji, vita ya Ukraine, kupunguza kodi, kujenga viwanda, kuondoa kodi kwenye tips, kupiga vita ushoga, kuzuia kutoa mimba nk. Biden muda wote alikuwa akisema Ukraine, Ukraine, Ukraine TU. Lissu muda wote itakuwa katiba, katiba, katiba.......
.
Ni kwanini tunataka kuishinda CCM? Tupishe na wengine wale au Kuna kitu mbadala wanataka kukifanya kwa ubora zaidi kuliko CCM?Hakuna chama kitaishinda ccm na Katiba hii !! Ndio maana ni muhimu kuibadilisha hii Katiba na mambo mengine yatafuata baadae! Bila hivyo tutakuwa tunatwanga maji kwenye kinu.