Hongera Mtaka: Ni heshima kubwa kwako kuwa Mkuu wa Mkoa Dodoma

Hongera Mtaka: Ni heshima kubwa kwako kuwa Mkuu wa Mkoa Dodoma

Mtaka alitakiwa awe na cheo kikubwa sana either Waziri mkuu au waziri tamisemi

Jamaa kichwani yupo vizuri sana halafu hana mihemuko kufanya maamuzi ana utulivu jamaa ukienda ofisini kwake anatoa ushirikiano wa hali ya juu sana


Kama ningekuwa mimi Ndiye rais alitakiwa kuteuliwa mapema kuwa mbunge then Waziri tamisemi Jamaa namkubali sana

Kama nchi inataka watu wa kusadia nchi basi ni kutafuta vijana aina ya Mtaka.

Na idara ya usalama wa Taifa kuwalinda juu ya kuchafuka.

Hawa ndio type ya viongozi taifa sasa linawahitaji.
[emoji106][emoji106][emoji106][emoji106]
 
Mnavyomsifia sijui kafanya kitu gani special ambacho wengine wameshindwa,too much hadi kero
Hata wewe ukifanya mambo mazuri, utasifiwa tu. Na kama unaumia sana, basi kunywa maji mengi ili upunguze shinikizo la damu mwilini!
 
ukiwa mtendaji mzuri huwa hakuna ubishi....hakuna anayemzungumza Mtaka vibaya, hii ni sifa nzuri kwake na malipo ya utendaji wake mzuri....
 
Nakumbuka wakati ule wakuu wa wilaya wanatia watu ndani huku wengine wakicharaza wananchi bakora ili kumfurahisha jiwe, mtaka yeye alipiga marufuku kwa wakuu wa wilaya kufanya hivyo ktk mkoa wake.Tatizo la nchi hii ni kwamba waimbaji wazuri wa mapambio na wapepesa midomo kama chalamila ndo wanaoonekana viongozi bora.
 
Ni mtu anayependa sana kusoma na kujielimisha. Na anatumia elimu yake ili kufanikisha kazi zake. Mtu kama Mtaka ndio hazina za nchi hii. Tunahitaji kusonga mbele. Tuache kubeba wasiobebeka. Tumeshafanya majaribio inatosha.
 
Kifupi Dr. Bilinith Mahenge, alikuwa yupo yupo tu! Hakuwa na ubunifu wowote ule!

Mlitaka Dr. Mahenge afanye ubunifu gani zaidi ya kusimamia hiyo ilani ya chama Tawala? Tuone kama Mtaka atakuja na ilaní yake tofauti!! Ajitahidi kama anaweza abuni mbinu ya kukomesha wagogo kuwa ombaomba!!!
 
Mtihani wa kwanza wa Mtaka Dodoma kuhusu haki ,uhuru wa kujieleza na democrasia ni wanawake wa Chadema ná Maandamano Yao kuhusu wabunge 19 wa CDM.Tafakari maneno RPC Dodoma kuhusu hayo Maandamano na Misimamo ya Mtaka
 
Ndugu Anthony Mtaka,

Dhamana ya kupelekwa Dodoma ni kubwa sana kuliko kama ungepelekwa Dar.

Umepelekwa Makao Makuu Rais ameonesha Imani kwako na uwezo wako kuwa juu ya siasa.

Nakutakia Kila la kheri kujenga Makao Makuu.
Mkuu wewe vipi , mbona hujakumbukwa ? nakuombea sana mkuu ili ule shavu
 
Mlitaka Dr. Mahenge afanye ubunifu gani zaidi ya kusimamia hiyo ilani ya chama Tawala? Tuone kama Mtaka atakuja na ilaní yake tofauti!! Ajitahidi kama anaweza abuni mbinu ya kukomesha wagogo kuwa ombaomba!!!
Umewatukana wagogo lakini kwa mimi Dar ni jii kubwa na hakuna watu wanaojinasibu wajanja kama wazaramo wanaongea sana, na Dar ndio nyumbani kwao walikuwa na nyumba za babu zao Dar nzima lakini hakuna watu maskini kama wazaramo pamoja na fusra zilizokuwa mbele yao hata nyumba za babu zao wameshauza wamesogea kisarawe huko na maneno yao mengi sijawahi kusikia hata wametoa RC na sijui hata mbunge tu Dar wacha uwaziri.
 
Back
Top Bottom