Hongera na pole Balozi Siwa. Je, utaiweza TISS au TISS itakuweza?

Je Unafikiri uteuzi DG MPYA TISS kila wakati una maslahi kwa USALAMA wa TAIFA?

  • Ndio

    Votes: 46 22.1%
  • Hapana

    Votes: 162 77.9%

  • Total voters
    208
K
Aiseee kuna uteuzi mpya huko?
Huyu aliyeondoka amekaa muda gani madarakani?
Amepwaya wapi?
Je hakuwa team Jk na vipi huyo mpya ni team Jk?
 
maslahi ya chama zaidi, maslahi ya watu binafsi zaidi ndio shida ya yote haya.

Hakuna tena wanaowaza kiundani maslahi ya Taifa na watu wake wapo wanaotetea matumbo yao, yamichepuko yao, yafamilia zao na ndugu zao nk.

Taifa linahitaji watu kadhaa watakaojitoa kwa maslahi ya Taifa na vizazi vingi karne nyingi mbele.
 
Watanzania tunasahau mapema na tunapelekwa na matukio. Ukweli ni kwamba kabla ya Dr Kipilimba kukalia kuti kavu, aliyekuwa wa kwanza kukutwa alikuwa ni Robert Masalika Makungu (Deputy Director TISS). Baada ya ripoti ya CAG kutoka na Trilioni 1.5 kupototelea kusikojulikana, bwana yule akashikwa na hasira akamtoa TISS hadi RAS Njombe.

Tatizo siyo watu, tatizo ni mfumo na mtu aliyeko ofisi ya juu kabisa. Jinsi mambo yalivyoharibika hapa Tanzania, leo hii hata Mkurugenzi TISS awe ni mtu aina ya Imran Kombe, Augustino Mahiga au Apson Mwang'onda yatawashinda tu. Uozo wa leo hii ni mkubwa, pia ni matokeo ya uzembe (COMPLACENCY) wa miaka mingi sana ulioelelewe na watu kama Mzee Mkapa na Mzee Kikwete.

Mama atatafuta mchawi lakini yeye mwenyewe na mfumo alioamua kuulea ndiyo chanzo.
 
Tujiunge na wachambuzi wenzetu kutoka pale George Bush Center For Intelligence, Langley, Virginia yalipo Makao Makuu ya CIA.

Mpaka sasa Lucas Mwashambwa hajawasili katika uzi huu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…