Hongera na pole Balozi Siwa. Je, utaiweza TISS au TISS itakuweza?

Hongera na pole Balozi Siwa. Je, utaiweza TISS au TISS itakuweza?

Je Unafikiri uteuzi DG MPYA TISS kila wakati una maslahi kwa USALAMA wa TAIFA?

  • Ndio

    Votes: 46 22.1%
  • Hapana

    Votes: 162 77.9%

  • Total voters
    208
Presidential decree....

Mama anafanya vile anavyoona inapaswa....

Mama ana "sources" nyingi za info zaidi ya hao anaowateua.....

Kubwa zaidi ni usalama wa rais wetu kipenzi na kubwa zaidi ni muendelezo wa utulivu wa taifa hili bora barani afrika [emoji120]

#Mwenyezi Mungu umlinde Rais wetu kipenzi SSH ,amen [emoji120]

#SiempreJMT amen[emoji120]
 
Naandika andiko hili nikiwa ndani ya Ofisi yangu ya mpya ya Centre for Strategic Intelligence and Clandestine Operation hapa ndani ya kijiji chetu hiki kdogo.

Rais wangu Samia Suluhu, najua kazi ya Urais ni Ngumu Sana, ila TRUST me kwamba ni kazi rahisi sana. Tatizo wanoko ni wengi na wanaoitaka pia ni wengi.

Hata hivyo leo sizungmzii cheo chako cha URAIS bali nazungumzia Uteuzi wako wa Mkurugenzi wa TISS. Kwa uelewa na uzoefu wangu. TISS ni kama Serikali ndani ya serikali. Kwa lugha nyingine Unapoteua Mkurugenzi wa TISS ni sawa na Umeteua Alternative Preseident au Rais mbadala kwani nyenzo alizo nazo ni sawa na nyenzo ulizo nazo isipokuwa yeye anakuwa hana Political Accoutability na wakti huo huo anakuwa na njia za kutengeneza Mazingira ya Plausible Deniability.

Sasa hili ni somo ambalo unahitaji muda na utulivu ili ulielewe. Ila nataka ufahamu kwamba Mkurugenzi wa TISS kwa chini huwa anakuwa na mamlaka sawa na uliyo nayo wewe. Kama ambavyo wewe unaweza kumtengua wakati wowote basi hata yeye ana uwezo na resources za kufanya hivyo.

Sasa nimesikia umetengua na kuteua mwingine. Unachosahau ni kwamba "Once a spy, always a spy"Ukishateua Mkuu wa TISS anapata clearance kubwa sana katika masuala ya taarifa na usalama wa nchi. Anakuwa na access ya resources zote za nchi. Zaidi mwaka huu mmewatungia sheria ya kuwapa kinga ya kutowajibika kisheria which means matendo yao hata kama yatakuwa ya kihalifu bado wanaweza kuepuka wajibikaji wa kisheria.

Sasa iko hivi, kwa sasa TISS ina spy masters watatu ambao wako around na wako nje na ndani ya Mfumo, Kipilimba, Diwani, na Masoro na sasa huyu bwana Siwa.

Iko hivi hawa wote ni Spy masters whether wako nje au ndani ya mfumo.

Ndio maana unapowatoa uhakikishe kwamba unaweza kuundoa Uspy master wao na hilo unajua kwamba huwezi.

Ndio maana huwa unapotaka kumtoa usimtoe kwasababu ya Makosa ya kiusalama au kwa sababu ya umbea au kwa sababu ya kukosa uvumilivu.

Spy masters hawajibishwi kama anavyo wajibishwa waziri au DC,Spy Craft ni mchezo tofauti sana.Ukitaka kufahamu hilo JIULIZE kilichofanya Imran Kombe akauwawa kama JAMBAZI ilihali wengine waliowahi kuwa wakuu wa kitengo waliendelea kuwepo ingawa baada ya wao na kujaribu ku activate mitandao yao walipigwa na kitu kizito.

Sasa umeteua DG mpya ambaye bila shaka unalo file lake na huenda linakuvutia hasa ukizngatia kwamba alishakaa kwa PAKA so anaweza kuwa na ka cv kazuri ila TRUST me huenda kwenye MEZA yako kuna mafili ambayo bado hujayasoma na kuyapitia vizuri na ukija kuyafikia unaweza kushawishika kufanya uteuzi mwingine tena ambalo nalo litakiwa kosa la KIMKAKATI.

Hawa jamaa wote wanaweza wa "Kagang UP" against you na hakuna unachoweza kufanya kwa sababa wanayo access ya taarifa na resources ambazo ww unajua uwezo wake.

Sasa lengo sio kuleta hofu bali kuchokoza mjadala tu kuhusu tatizo lililoko katika IDARA yetu ya USALAMA wa TAIFA.

Ila uelewe vizuri nitakukumbusha hadithi ya bwana Mdogo Ole Sabaya ambaye aliwahi hata kufoji kitambulisho ka cha TISS na kujiita Afisa Kipenyo wakati akiwa mwenyekiti wa UVCCM Arusha na wapo wengi kama yeye, So unapobadili Wakurugenzi Jiulize iwapo Tatizo ni TISS au ni Wakurgenzi wa TISS?

Madam President, Fahamu kwamba TISS sio CID wala sio Military Intelligence UNIT ingawa kimajukumu, TISS anaweza kuingia katika hayo maeneo yote ila sio CID wal MIU wanaweza kuingia katika maeneo ya TISS so ni muhimu tukajiuliza iwapo TISS imevamiwa na KIRUSI na inahitaji kupigwa Immune Booster nani ataipiga immune booster?

Kuna kipindi mm binafsi niliona au kuhisi kwamba Utawala wako uliamua kutumia JU(Jeshi la kupambana na Ujangili kama TISS mpya so nikafikiri umegundua TATIZO na unalitafutia Suluhu kama Ulivyo wewe.

Tatizo kwa sisi wenye macho ya Rohoni tuliingia katika Sala, maombi na kufunga na tukagundua kwamba kulikuwa tu na mambo fulani ya wajomba zako ulikuwa unawatumia jamaa wa juu kuyaweka Sawa. Anyway hiyo issue kila mtu atakuwa ameshaijua hasa tukisikia stori za Loliondo

Sasa fahamu hili, huwezi kupata TISS bora kwa kutumia TISS katika muundo na utaratibu wake wa Sasa. TISS ambayo ilifanya kazi enzi za Mwalimu sio Sawa na TISS ambayo inafanya kazi enzi hizi. Imagine mimi hapa nilipo nawez kuona patern of errors unazofanya bila hata kuwa na taarifa za jikoni unadhani hao ambao wana access ya taarifa za jikoni wanaona nini kama sio zaidi ya haya.

Sasa nataka ujilulize. Je unafikiri TISS ni kama wizara ambapo unaweza kubadili katibu mkuu na kazi ikaendelea? Hapana.SPIES are trained not TRUST.

So kadiri unavyoleta na kubadili wakuu wa TISS ndivyo idadi ya MOLES inaongezeka ndani ya IDARA na Badala ya kuwa idara ya Usalama wa Taifa na inakuwa ni Idara ya Kupika Majungu, vijembe, fitna na kukomoana. TRUST me ikiendelea kuwa hivyo hata wewe utapewa Majungu, utapigwa vijembe utafanyiwa Fitna na hata kukomolewa mwishoni Utakumbuka Kamsemo "WHo will Watch the Watchers"

Nimechokoza mjadili, hayo mengine sijui kama ni ya kweli niko hapa pembeni ninaendelea kupata Madini wala sijajificha.

Ukiona nchi ni Maskini jua "wavaa miwani myeusi" hawana uwezo!
 
Mimi sijui lolote kuhusu masuala ya TISS, lakini simple reasoning, kama taasisi za umma zimejaa uzembe, fitina, majungu, kukosa umakini kutokana na RUSHWA, USWAHIBA, UPENDELEO NA UKADA, deductively hata TISS haina exception. So, nadhani tatizo ni mfumo uliooza uliojengeka kwa miaka mingi!
 
Watanzania tunasahau mapema na tunapelekwa na matukio. Ukweli ni kwamba kabla ya Dr Kipilimba kukalia kuti kavu, aliyekuwa wa kwanza kukutwa alikuwa ni Robert Masalika Makungu (Deputy Director TISS). Baada ya ripoti ya CAG kutoka na Trilioni 1.5 kupototelea kusikojulikana, bwana yule akashikwa na hasira akamtoa TISS hadi RAS Njombe.

Tatizo siyo watu, tatizo ni mfumo na mtu aliyeko ofisi ya juu kabisa. Jinsi mambo yalivyoharibika hata Tanzania, leo hii hata Mkurugenzi TISS awe ni mtu aina ya Imran Kombe, Augustino Mahiga au Apson Mwang'onda yatawashinda tu. Uozo wa leo hii ni mkubwa, pia ni matokeo ya uzembe (COMPLACENCY) wa miaka mingi sana ulioelelewe na watu kama Mzee Mkapa na Mzee Kikwete.

Mama atatafuta mchawi lakini yeye mwenyewe na mfumo alioamua kuulea ndiyo chanzo.
Hii idara imeharibia kipindi kundi la Wana mtandao walipoanza kuusaka urais 1995 Baada ya Kikwete kushindwa ndani ya CCM akapita MKAPA ,

Hapo ndipo Mkakati ukaanza kusukwa ili kuweza kumuingiza Msoga Ikulu na Moja ya Sehemu ambayo kutokana na Mkakati wao ili waingie Ikulu ni kuifanya TISS iwe yao na walifanikiwa maana waliweka watu wao wengi sana na wengine wakongwe kubadilishwa na PESA

Kwa hiyo ili Mama afanikiwe Ila kama ni kwa maslahi ya Taifa , hii idara ifumuliwe upya

Ila kama ni kwa maslahi ya wajomba zake (Waarabu) Niko begabega na TISS hii
 
Hawa uliowataja ni panya road wa mtandaoni. Hapa nimepata jambo moja. Loliondo tatizo lake ni Samia akiwakingia kifua wajomba zake.
Ujinga mweupe huo....

Umeamua kumchafua Rais kwa kuamini maneno ya watu ?!!! [emoji15][emoji15][emoji15]

Wa kizimkazi ,wa mwakakogwa-kuoga mwaka hawana mahusiano na WAARABU waliowaita babu zao WAHADIMU....

Unaujua uhadimu wewe?!!!

Makunduchi ndio "epicenter" ya WAZALENDO wa Zanzibar wanaoutukuza MUUNGANO na wasioutaka uvunjike....

Karibu wanzuki[emoji120]
 
Ko mkuu mtu kateuliwa, halafu hafanyi vizuri tumuache? Akizingua hata huyu atolewe tu, hakuna mtu mkubwa kuliko taifa kwamba una chance hata ukizingua tusikutoe kisa ni spy master
Kwanini ateuliwe mtu ambae hafanyi vizuri? Unahisi mtu anaefanya vizuri home works zake anaweza kumteua mtu ambae hafanyi vizuri?

Hizi nafasi ni nyeti Sana, tuache ushabiki wa 'anatoka dini gani au anatoka mkoa gani' tufuate kanuni na viwango vya Tiss
 
Back
Top Bottom