Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 28,722
- 20,610
Ndugu zangu Ni wachache wenye kuona na kutambua kazi kubwa inayofanywa na hivi vyombo vyetu katika kuilinda na kuipigania nchi yetu usiku na mchana na hatimaye kufanya watanzania tuishi kwa amani bila hofu Wala mashaka
Msingi wa maendeleo katika nchi yoyote Ile Ni uwepo wa amani na utulivu, msingi wa watu kufanya kazi za kimaendeleo ni uwepo wa usalama katika nchi, msingi wa kushamiri kwa biashara na wafanyabiashara Ni usalama katika nchi, chambo kuu ya kuwavuta wawekezaji au watalii au wafanyabiashara wakubwa toka mataifa mbalimbali ni uwepo wa usalama madhubuti ndani ya nchi
Tanzania imeendelea kuwa kisiwa Cha Amani kwa kuwa Asikari wetu wanapambana muda wote kuzuia uhalifu na kuwakamata wahalifu, Ndio maana Inafika hatua watu wanashangaa inakuwaje kwa wakati mmoja viongozi wakubwa wa juu wawili au wote watatu hawapo nchini? Wanauliza haya kwa kuwa wanajuwa kwa nchi za wenzetu hasa Afrika Jambo Hilo Ni gumu, kwetu linawezekana kwa kuwa tunavyombo imara na madhubuti Sanaaaa vilivyojidhatiti kulinda na kuipigania nchi yetu
Rai yangu kwa vyombo vyetu Ni kuwa natambua kazi ya ulinzi ilivyo ngumu kwa kuwa baba yangu amewahi kuwa mwanajeshi aliyepigana Vita vya Tanzania na Uganda 1978-1979 Tena akiwa mstari wa mbele kabisa na kufanikiwa kukanyaga Aridhi ya Uganda na kurudi mzima Hadi Leo Ni mzima pia, Na hata matunda yake yapo mpaka Sasa maana aliporejea alipewa ardhi kubwa Sana na serikali ya Kijiji Kama zawadi ambayo imenisaidia katika kusoma, Ndio maana naipenda nchi yangu na kuwa mzalendo kwa kuwa Baba yangu alitoa jasho kuilinda na kuipigania Tanzania hii
Hivyo nawaomba Asikari na wanajeshi wetu Kuendelea na moyo huo wa uzalendo kwa nchi yetu Katika kuilinda na kuipigania. msikatishwe Tamaa na maneno ya wachache wanaokuwa wanaongeaa maneno ya kuwakatisha Tamaa, Msijari maneno yao, piganieni Taifa letu, ilindeni mipaka yetu kwa nguvu zenu zote, mamilioni ya watanzania Tupo nanyi na tunawaombea ili Mwenyezi Mungu awalinde muwapo katika majukumu yenu
Tangulizeni moyo wa uzalendo hata pale inapotokea Kuna baadhi ya madai au Mahitaji hamja pewa kwa wakati ,Nawaombeni muwe na Subira uvumilivu utiifu na moyo wa Kuendelea kuilinda nchi yetu kwa uzalendo kwa kuwa serikali yetu imeonyesha muda wote kuwajari na kuwasikiliza, mlipo na malalamiko Tumieni njia nzuri na za kizalendo kufikisha madai yenu
Ushauri kwa Rais wetu mpendwa kipenzi Cha watanzania mama Samia Namuomba aendelee kuwajari na kuwaongezea bajeti kila Hali ya uchumi inaporuhusu ili waweze kufanya kazi kwa urahisi hasa kwa kuwa na vitendea kazi Bora na vya kisasa zaidi, lakini pia kuwapa faraja na kuwatia moyo wakati wote,
Kazi iendeleee,Mungu ibariki Tanzania, Mungu mbariki Rais wetu,Mungu vibariki vyombo vyetu vya ulinzi na usalama, Mungu Tubariki watanzania na utusamehe pale miongoni mwetu wanapotokea kukufuru na kukukosea, usituadhibu wote Kama Taifa, Tunaomba utuhurumie na utusamehe,
Lucas Mwashambwa ,kijana mzalendo na mpenda nchi yangu, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na sauti