Hongera Rais kwa usajili wa alama za vidole, ila tambua kwamba haupo salama!

Hongera Rais kwa usajili wa alama za vidole, ila tambua kwamba haupo salama!

Line moja siyo ufumbuzi kwani mtu anayesajiliwa kwa jina lako huwa kwenye line moja pia na ni kampuni hiyo hiyo unayotumia wewe, kumbuka kampuni za Simu ni nyingi na zote zinalipa kodi na si kila kampuni inapatikana kote Nchini ndiyo maana watu huwa na Line za kampuni zingine kulinda mawasiliano pindi wakiwa wilayani vijijini kwenye Tatizo la Network
Hebu fafanua vizuri. Itawezekanaje mtu atumie taarifa zako endapo haitaruhusiwa kwa mtu mmoja kusajili line (mtandao) zaidi ya moja?

Nielewavyo mimi kwa mujibu wa mtoa taarifa ni kwamba kwa vile hakujaweka kikomo cha idadi ya simu za kumiliki, mtu mwingine anaweza kutumia taarifa mwenzie aliyekwisha sajili ili kujipatia line yenye namba mpya.

Kumbuka line (namba) moja haiwezi kutumiwa na mtu zaidi ya mmoja.
 
JAMANI TUWE WAKWELI HIVI TANZANIA INA MAADUI WA NJE KWA UMASKINI TULIONAO???

KAMA VYOO VYA MADARASA TU TUNASHINDWA KUJENGA HAO MAADUI WATAFUATA NINI HAPA??? WATU WANATUJENGEA HADI VYOO HALAFU TUNAWAITA MAADUI KWELI???

Sent using Jamii Forums mobile app
Tanzania hatuna maadui Nchi jirani zote tunaishi nazo kwa Amani, Uadui uliopo ni wa ndani tu CCM ya awamu ya Tano kuwachukua upinzani na cyprian Musiba kutumika kuwakoroga wasaka nia huko CCM, zaidi ya hapo hakuna Uadui mwingine zaidi.
 
Wanacho kifanya wale ma-freelancer (wasajiri) wanakwambia weka alama za vidole kisha utaweka zaidi ya mara moja ,akijadi kukwambia mtandao unasumbua rudia tena huku akisajili linw usizo zijua,mwisho anakwambia imekubali kisha unakuwa umesajiri line yako na zawengine kwa taarifa zako

Sent using Jamii Forums mobile app
Kama zimesajiliwa laini zaidi ya moja kwa taarifa zako basi ujue siku zoezi la kufungwa likifanyika lazima utatakiwa kwenda kuzitolea maelezo laini hizo, kwa hiyo kuhusu usajili wa laini zaidi ya moja hautakuwa changamoto sana. Ila yote kwa yote naunga mkono hoja hili zoezi ni hatari kuwakabidhi freelancers wazunguke mtaani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hebu fafanua vizuri. Itawezekanaje mtu atumie taarifa zako endapo haitaruhusiwa kwa mtu mmoja kusajili line (mtandao) zaidi ya moja?
ile ile line moja uliyosajili anasajiliwa mtu mwingine pasipo wewe kujua na Mbinu inayotumika huwa ni kusingizia hakuna network ili wapate kisingizio cha kumwambia mtu arudie kuweka Alama ya vidole kwa mara ya pili, pia Tambua kuwa siyo kila kampuni ya Simu imesambaa Nchini kote, ndiyo maana huhijika line za kampuni zingine ili pindi ukisafiri uwe hewani popote unapokuwa Nchini, line moja ukienda kijijini kusiko na Network ya hiyo Line yako moja utafanyeje?
 
Usichoke endelea kunipa darasa. Ikiwa mtu mwingine atapewa namba yako je line yako itaendelea kutumika? Yaani namba moja itaweza kutumiwa na watu wawili kwa wakati mmoja?
 
Watu wanaandika tu bila kufanya research... Fanyeni research kwanza... Hayo mnayoyawaza sasa yalishafikiriwa hata kabla huu mfumo haujaanza kufanya kazi... Kuna taratibu za kufuata ili upate laini ya pili within the same network.
 
Kama zimesajiliwa laini zaidi ya moja kwa taarifa zako basi ujue siku zoezi la kufungwa likifanyika lazima utatakiwa kwenda kuzitolea maelezo laini hizo, kwa hiyo kuhusu usajili wa laini zaidi ya moja hautakuwa changamoto sana. Ila yote kwa yote naunga mkono hoja hili zoezi ni hatari kuwakabidhi freelancers wazunguke mtaani.

Sent using Jamii Forums mobile app
Na sababu kuu serikali kuomba mtu awe na laini moja kutoka mtandao mmoja ni kwamba kila number ya simu na fingerprint zake zinahifadhiwa kwenye database ya mtandao husika na TCRA. Kwa kuwa fingerprint huwa hazifanani kama unasajili line ya pili kwa fingerprint zile zile kwa mtandao huo huo line ya pili itagoma kukubali usajili kwa kua fingerprint unazotumia kusajili line 2 zinakuwa zimeishasajiliwa kwenye database mpaka line 1 na taarifa zake walinganishe na kitambulisho chako unachotaka kusajilia line 2 hivyo watajua mmiliki halali wa line 1 ni nani tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
iwe zuga iwe kweli kwenye usajili wa Line tayari upo ujanja ujanja mwingi watume vyombo vya uchunguzi kupenya huko ikibidi uwepo mfumo wa kumtumia msg mtu endapo line yako ingine ipo hewani na hauitumii wewe
Nafikiri taarifa hizi zinafikirisha kweli ingawa mimi siamini kuwa TCRA wameiacha system porous kiasi cha kufanyiwa ujanja na wanaosajili hizi laini. Ukweli ni kwamba hii haraka ya kuwatambua raia na kuwapa namba naitilia shaka kiasi kwamba ni rahisi kuwapa uraia watu wasiostahili. Pale mwanzo kulikuwa na mchakato bora sana wa kumfanyia vetting mlengwa uliohusisha watu wa uhamiaji, lakini kinachoendelea sasa huku mitaani yaelekea ni kwa ajili ya kusajili laini za simu tu na si kutambua yupi ni raia anayestahili ID na yupi sio.
Hata hivyo ni wajibu wa NIDA kuutolea maelezo kitaalamu kila wasi wasi wa wadau juu ya uwezekano wa mfumo kuingiliwa na kusajili line nyingi kwa taarifa za mtu mmoja, kwani kama hii inaweza kutokea basi itakuwa hatari sana na zoezi zima likawa halina maana. Yawezekana ni wasi wasi tu wa wadau lakini ni vizuri TCRA na NIDA wakatuhakikishia raia sisi mambumbu wa taaluma ya Tehama usalama wa mfumo wetu. Huku mitaani ni vululu vululu kwani kuna maeneo watu wanalipisha kusajili line kama mdau alivyodai line iliyosajiliwa inauzwa elfu tatu.
 
JAMANI TUWE WAKWELI HIVI TANZANIA INA MAADUI WA NJE KWA UMASKINI TULIONAO???

KAMA VYOO VYA MADARASA TU TUNASHINDWA KUJENGA HAO MAADUI WATAFUATA NINI HAPA??? WATU WANATUJENGEA HADI VYOO HALAFU TUNAWAITA MAADUI KWELI???

Sent using Jamii Forums mobile app
Zinduka ndugu! Tanzania siyo nchi masikini kwa vile imejaaliwa rasilimali nyingi, bali watu wake ndio masikini kwa maana tumekosa maarifa ya kuzitumia rasilimali zilizopo. Wenye akili (maadui) wanatamani rasilimali amba tunazikalia ili ziwanufaishe.
 
Kaka
Nafikiri taarifa hizi zinafikirisha kweli ingawa mimi siamini kuwa TCRA wameiacha system porous kiasi cha kufanyiwa ujanja na wanaosajili hizi laini. Ukweli ni kwamba hii haraka ya kuwatambua raia na kuwapa namba naitilia shaka kiasi kwamba ni rahisi kuwapa uraia watu wasiostahili. Pale mwanzo kulikuwa na mchakato bora sana wa kumfanyia vetting mlengwa uliohusisha watu wa uhamiaji, lakini kinachoendelea sasa huku mitaani yaelekea ni kwa ajili ya kusajili laini za simu tu na si kutambua yupi ni raia anayestahili ID na yupi sio.
Hata hivyo ni wajibu wa NIDA kuutolea maelezo kitaalamu kila wasi wasi wa wadau juu ya uwezekano wa mfumo kuingiliwa na kusajili line nyingi kwa taarifa za mtu mmoja, kwani kama hii inaweza kutokea basi itakuwa hatari sana na zoezi zima likawa halina maana. Yawezekana ni wasi wasi tu wa wadau lakini ni vizuri TCRA na NIDA wakatuhakikishia raia sisi mambumbu wa taaluma ya Tehama usalama wa mfumo wetu. Huku mitaani ni vululu vululu kwani kuna maeneo watu wanalipisha kusajili line kama mdau alivyodai line iliyosajiliwa inauzwa elfu tatu.
Huku ninakoandikia uzi huu line zinapatikana fresh kabisa.
 
Line mbili namba tofauti watumiaji wawili wasiojuana taarifa na fingerprints za mtu mmoja. Elewa.Mtanao mmoja zinasajiliwa line zaidi ya tatu
 
Back
Top Bottom