Hongera Rais Magufuli kuipendezesha Ikulu yetu kuliko enzi za Nyerere, Ikulu iwe kivutio cha utalii, restrictions ziondolewe watalii wafurike

Hongera Rais Magufuli kuipendezesha Ikulu yetu kuliko enzi za Nyerere, Ikulu iwe kivutio cha utalii, restrictions ziondolewe watalii wafurike

Mkuu ukweli kama umekulia Dar au umeishi miaka mingi utajua Ikulu kuna wanyama miaka mingi kabla ya magufuli kuwa raisi au pengine kabla ya kuwa Mbunge.

Sema raisi waliomtangulia hatukuwaona wakiwa ktk picha wanahudumia wanyama au wana watazama kama kujifurahisha wakiwa pale Ikulu.
Zebra walikuwepo pia ?
 
Boss Pascal Mayalla Cheo cha Msemaji wa Serikali aka Jamhuri kipo wazi ... Mbona unaharibu tena? Unasifia kupita maelezo, Mimi siungi mkono hoja kuhusu Ikulu ziwe open kwa ajili ya Utalii, Hell no. Kuna Mdau humu alikupigia debe, wakupe wewe hicho Cheo.

Usalama wa Ikulu zetu ziendelee kuwa imara, tulisikia juzi, Beberu alisema 1978 alitumwa kuipiga Ikulu ya Dar aka Magogoni. Ukisharuhusu tu haujui Mtu mzuri ni yupi na adui ni yupi.
 
Ni muhimu sana rais Magufuli afanye safari muhimu za nje ili kupata exposure, akaone Ikulu ya South inavyofurika, pia aende Ikulu ya White House tena akiandamana na Makonda ili kumkomoa beberu Pompeo!, akaone jinsi wageni wanavyo jivinjari kwenye Ikulu ya White houseya Marekani. Hao wanyama na all the beauty ni bure kama watu hawatembelea na kuchangia upkeep cost.
Unataka Rais wetu aharibu pesa kwa kwenda kuangalia ikulu za watu tu?

Acha utani
 
Ila tushukuru sana Mungu watu kama nyie hamkuwepo kipindi Mwalimu Nyerere anapambania uhuru wetu, yani tungechelewa SANA kupata uhuru kwa hizi tabia za uchumia tumbo, [emoji114][emoji1751]

Sent using Jamii Forums mobile app
Hakika umesema vema, yaani ukiwa na kundi la watu wa aina ya pascal kutegemea mabadiliko ni ndoto, sasa naelewa kwanini kwenye orodha ya wapigania Uhuru kwanini hakuna wasukuma
 
Paschal punguza njaa ya kitoto na kujipendekeza. Kauli ya "ONGERA MAGUFULI KWA KUIPENDEZESHA IKULU KULIKO ENZI ZA NYERERE" wakati wa Nyerere anaipokea hiyo IKULU kutoka kwa wakoloni ulikuwepo?

Na ni kipimo kipi unakitumia kulinganisha miaka ya 60 ya mwalimu na ya sas ya Magu? Magu anaendeleza iweje ubeze mwanzilishi. Nyerere hana mfano katika uhifadhi wa wanyamapori Ikulu.

TATIZO unawinda nafas ya Dr. Abbas usemaji wa serikali, wee tulia kama imepangwa utapata acha kujipendekeza una boa bro.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa uandishi huu kweli kesho CNN, BBC and the like watakutaka uende kuwafanyia kazi kweli? Jeff koinange alijaribu! Mayalla, avoid such kind of posttings kwa level yako please! Yaani Ikulu iwe free to enter place!
 
Its very unfortunate, kumsikia Pascal akizungumza ama kuandika hivi.

Unapoona mtu aliyekuwa mbele kwa mengi ya maana na mara anafanya vinginevyo, basi kuba tatizo, ni vizuri kufuatilia kilichompata na pia kumpeleka kwa Madaktari wajuuzi wa Saikologia afanyiwe medical evaluation, lazima kutakuwa kuna kitu ama VIRUS imempata.

Tumuombee ndugu na kaka yetu Pascal afya, uzima na Mola Amrejeshe kwenye hali yake timamu ya awali.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Brother kaa nyumbani cheza na wajukuu kama mjini mishe zimekuwa ngumu maana sasa hivi unandika madudu tupu unajishushia heshima yako, tulikutetea sana kipindi wanakutuhumu umemuuza Kabendera tulibisha humu mapovu yakatutoka lakini kwa rangi unayotuonyesha sasa ni wazi kabisa sasa una ukasuku

Hatukatai kumsifia mh Rais wetu kwa mambo mazuri tunachokataa ni huu ujinga ulioandika huu hapa

(Kiukweli hadi raha! Mimi napendekeza Rais Magufuli akae Ikulu hadi pale Mungu atakapoamua!)

Takataka gani umeandika hapo tena mtu mwenye taaluma ya sheria unaijua katiba vizuri, kiumri unajua mengi umeona mengi sasa umeanza andika utoto kwa uandishi huu tegemea kuikimbia JF maana member wakikuchoka humu utashangaa kila andiko wana wewe mwisho wa siku utaishia kusoma tu yaliyoandikwa na kuichukia JF kama kina musiba na wengineyo
 
Hilo swala la ulinzi twahisi they are taking it over the top. Eti hata ukipita tu nje upande wa ukuta wanakukoromea?! Nahisi ni ubabe wa kishamba na uzushi tu. Ikulu ni patakataifu sawa kwa nchi yetu lakini isiwe shida kwa raia kukatazwa kupita hata nje ukichukulia barabara zetu nyingi almost 99% hazina pedestrian crossing or walks ...
 
Yani Magufuli kurudisha wanyama Ikulu inakuwa guarantee ya yeye kutawala hadi kufa...Nyarere aliyewaweka hao wanyama hakutawala hadi kifo Magufuli atawale hadi kifo kisa tu karudisha wanyamapori...ofkoz Magufuli anachotafuta ni sifa binafs sio sifa ya kitaasis.

Kwamba nae amefanya jambo jipya ..Magufuli hajawahi na hatowahi kufanya jambo jipya hata siku moja ...Aliwarudisha kimya kimya sasa anatupigia vi-clip tumuone...Kuna watu walifanya mazuri lakini hawakupenda kuonekana public ila matendo yao yaliwaonyesha.

Ila na wewe unekuwa mtu mzima zaid naona umekuwa addicted na Magufuli sababu kubwa ni ama kutafuta uteuzi ama kujikomba tu ukijua Magufuli n msukuma mwenzio kumbe Magu n mzinza.

Siku ukipata uteuzi utavua hadi nguo.
 
Back
Top Bottom