Wanabodi,
Leo kuna video clip ya Ikulu yetu ya Magogoni imepandisha humu, kiukweli nimekuwa very impressed na ile zoo ya Ikulu na jinsi wanyama walivyopendezea.
Kwenye mazuri wajameni tupongeze:
Wanyama pori waipamba Ikulu, Hongera sana Rais Magufuli
Kiukweli hadi raha! Mimi napendekeza Rais Magufuli akae Ikulu hadi pale Mungu atakapoamua!
Sasa tuifanye Ikulu yetu kuwa kivutio cha utalii, vile vizuizi viondolewe, waweke
nominal fee watalii hadi wa ndani tutafurika.
Ni muhimu sana rais Magufuli afanye safari muhimu za nje ili kupata
exposure, akaone Ikulu ya South inavyofurika, pia aende Ikulu ya White House tena akiandamana na Makonda ili kumkomoa beberu Pompeo!, akaone jinsi wageni wanavyo jivinjari kwenye Ikulu ya White houseya Marekani. Hao wanyama na all the beauty ni bure kama watu hawatembelea na kuchangia upkeep cost.
Na kama hoja ya
restrictions ni usalama wa rais, maana naona ulizi wake unakaribia wa Mu7, then Ikulu Zoo iwe open to public zile siku rais yuko Dodoma ambapo pia I hope kutakuwa na Chamwino Zoo. Kiukweli ita-make hata kuliko Chato!
Hongera sana Rais Magufuli kwa kuendelea kumuishi Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere kwa maneno na matendo, pia tunakuombea utawale kwa muda kama wa Nyerere au kwa kukaribiana tu japo vipindi viwili vya miaka 10/10.
P