Hongera Rais Mwinyi, Rais Samia Uko Wapi?

Hongera Rais Mwinyi, Rais Samia Uko Wapi?

MtuHabari

JF-Expert Member
Joined
Oct 16, 2020
Posts
321
Reaction score
1,019
Katika hotuba zenu za Mei Mosi jana kuna suala sugu sana ambalo Rais Mwinyi amelikumbuka lakini mama Samia hakuligusia hata kidogo.

Ni Suala la PENSION ZA WAZEE WASTAAFU WALIPWAO NA HAZINA.

Serikali ya Mapinduzi imetangaza bila chenga kupandisha viwango vya pension kwa 100% lakini huku kwetu hakuna lolote limetajwa.

Ni jambo la kusikitisha hawa wazee wengi walipwao na hazina ambao kwa uzee wao unaweza kukuta nchi nzima pengine hawafiki hata elfu 10 bado wanalipwa laki moja kwa mwezi na hao unakuta ni wanajeshi (wengine wamepigana vita kwa nchi hii), wahandisi, madaktari waalimu nk lakini kwa vile wengi wao ni wastaafu miaka kabla ya mwaka 2000 uadilifu ukiwa mkubwa ni maskini tuu.

Tunajua Rais hatengenezi Budget ya nchi bali watumishi viongozi waliopo hivyo tunadhani mama hakuliona hilo lakini BADO ANAWEZA KULIONA NA KUAGIZA KUFANYWA AMMENDMENT.

Wazee hawa ukitaka kuwaona na kuwahurumia uwakute wakifanyiwa uhakiki kisha ukiambiwa mafanikio ya sasa ya nchi ni mchango wao basi waweza kutokwa machozi na pengine hali yao ndio inachangia watumishi wa sasa kufanya ufisadi kwani wanaogopa hali hii kuwakuta uzeeni.

Kama nchi zilizoendelea wana nyumba za kutunza wazee na sisi hatuwezi hilo basi Mama Samia wakumbuke hata kuwaongeza Pension ili hata DUA WAKUOMBEE.
 
Sidhani kama Budget inayoandaliwa na watu aina ya Mwigulu inaweza kukumbuka wazee waadilifu wa zamani ili hali kura zao hazina impact kubwa kwenye uchaguzi, wao kila kitu wanawaza uchaguzi tu.

Ila wenye kufikisha ujumbe kwa Rais wamfikishie ujumbe huu kuwa awakumbuke hawa wazee wachache walio baki apate baraka zao.

Wengi waliipigania nchi hii kwa uzalendo wa kweli.
 
Wevi na vibaka ndo wanakumbatiwa na CCM siku zote,watu mlio na tumaini kubwa kwa rais Samia honorable causa kuhusu maslahi ya wafanyakazi mnaota ndoto ya mchana Mweupe.

Endelea kuvaa nguo za Mei mosi na kuimbishwa mapambio ya "2025 tuna kwenda na Mama"
 
HAO HAO NDO WALIYO IWEKA SISIEM MADARAKANI MIAKA YOTE

ACHA WALE JASHO LAO

WATAISOMA NAMBA

SISI MPAKA TUSTAAFU HII SISIEM ITAKUWA HISTORIA KAMA TANU
 
Kodi za watanganyika zinagharamia neema kwa wazanzibari
 
HAO HAO NDO WALIYO IWEKA SISIEM MADARAKANI MIAKA YOTE

ACHA WALE JASHO LAO

WATAISOMA NAMBA

SISI MPAKA TUSTAAFU HII SISIEM ITAKUWA HISTORIA KAMA TANU
Lakini si tunakubaliana kuwa CCM toka uchaguzi wa vyama vingi uanze hata kama inashinda lakini kwa kiwango cha kutisha ilikuwa inaiba uchaguzi?
Why tuwabebeshe watumishi wetu wachache waliotumikia kwa uadilifu?
Nimekaa siku moja na nwanajeshi mmoja alikuwa na cheo cha Luteni na kapigana Msumbiji na Uganda lakini ukiona maisha yake ya sasa utamhurumia.
Hana watoto wa kumuangalia na maradhi ya uzee yanamsumbua huku akisubiri hiyo laki yake kila mwezi.
Kumbuka hawa ni wale walistaafu kabla ya mifumo ya mifuko ya jamii hivyo wanalipwa na Hazina. Sio huyo tuu wapo nadaktari, wauguzi na waalimu hali inatisha na ingekuwa ulaya ndio wanawekwa nyumba za wazee.
Ni utu wema kuwakumbuka wazee!
 
Back
Top Bottom