MtuHabari
JF-Expert Member
- Oct 16, 2020
- 321
- 1,019
Katika hotuba zenu za Mei Mosi jana kuna suala sugu sana ambalo Rais Mwinyi amelikumbuka lakini mama Samia hakuligusia hata kidogo.
Ni Suala la PENSION ZA WAZEE WASTAAFU WALIPWAO NA HAZINA.
Serikali ya Mapinduzi imetangaza bila chenga kupandisha viwango vya pension kwa 100% lakini huku kwetu hakuna lolote limetajwa.
Ni jambo la kusikitisha hawa wazee wengi walipwao na hazina ambao kwa uzee wao unaweza kukuta nchi nzima pengine hawafiki hata elfu 10 bado wanalipwa laki moja kwa mwezi na hao unakuta ni wanajeshi (wengine wamepigana vita kwa nchi hii), wahandisi, madaktari waalimu nk lakini kwa vile wengi wao ni wastaafu miaka kabla ya mwaka 2000 uadilifu ukiwa mkubwa ni maskini tuu.
Tunajua Rais hatengenezi Budget ya nchi bali watumishi viongozi waliopo hivyo tunadhani mama hakuliona hilo lakini BADO ANAWEZA KULIONA NA KUAGIZA KUFANYWA AMMENDMENT.
Wazee hawa ukitaka kuwaona na kuwahurumia uwakute wakifanyiwa uhakiki kisha ukiambiwa mafanikio ya sasa ya nchi ni mchango wao basi waweza kutokwa machozi na pengine hali yao ndio inachangia watumishi wa sasa kufanya ufisadi kwani wanaogopa hali hii kuwakuta uzeeni.
Kama nchi zilizoendelea wana nyumba za kutunza wazee na sisi hatuwezi hilo basi Mama Samia wakumbuke hata kuwaongeza Pension ili hata DUA WAKUOMBEE.