Kanda ya kusini kuchele Ndanda kuchele.
CCM kwani imekuwaje? Hela izunguke mikoa yote Madalali wa korosho waondoke.
Kusini tumeona
#MAMA SAMIA KAUPIGA MWINGI KAMA ALIVYOUPIGA UNCLE 2017/2018
kiufupi kila mkulima na kangomba afurahi.
Mnada wa kwanza 4,090 kwa newala na tandahimba
Hii bei ni kubwa sana kwa jinsi watu walivyokuwa wamekata tamaa hata YA kulima na kulizia lorosho zao.
Kumbe miaka ya nyuma mlikuwa mnatuhujumu kwa kiwango kikubwa namna hii .Mwaka jana minada ilifika hadi 1600 ila mwaka huu bei imepaa zaidi.
Kangomba tulio nunua chache kwa kuogopa bei itakuwa chini tumehuzunika sana.
Walio jilipua kwa 1500 wameona matunda yake..
Korosho ni dhahabu yakusini korosho inaweza kukutoa mchana kweupe korosho ni utajiri.
TUNAWASHUKURU CCM KWA KUWAONDOA MADALALI WENU WA KOROSHO.
Soma Pia: Rais Samia umetuteIekeza Wakulima wa Korosho?
======
Leo Oktoba 11, 2024, historia imeandikwa katika mikoa ya kusini baada ya kufanyika mnada wa kwanza wa korosho ulioandaliwa na Chama Kikuu cha Ushirika Tandahimba na Newala (TANECU).
Katika mnada huo, jumla ya tani 3,857 za korosho zimeuzwa kwa bei ya juu ya shilingi 4,120 kwa kilo, huku bei ya chini ikiwa shilingi 4,035. Haya ni mafanikio makubwa kwa wakulima wa korosho ambao wamekuwa wakisubiri kwa hamu bei nzuri ya zao hili muhimu.
Wakulima wa Tandahimba na Newala wameonyesha furaha kubwa kwa hatua hii, huku wakimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, kwa jitihada zake katika kuhakikisha bei za korosho zinapanda na kuwa na tija kwa wakulima. Wamesema kuwa mnada huu wa kwanza umewapa matumaini makubwa kwamba kilimo chao sasa kinaleta faida zaidi, na maisha yao yataboreka kutokana na ongezeko hili la kipato.
Akizungumza mara baada ya mnada huo uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Mji wa Newala, mmoja wa wakulima wa korosho,alisema:
"Tunamshukuru sana Rais Samia kwa juhudi zake za kuhakikisha tunapata bei nzuri kwa mazao yetu. Hii ni hatua kubwa kwa wakulima wa korosho, na tunaamini kwamba serikali itaendelea kutusaidia ili tuendelee kuuza kwa bei nzuri kama hii."
Aidha, wakulima hao wameiomba serikali kuendelea kusimamia bei hizi kwenye minada ijayo, huku wakionyesha imani kwamba chini ya uongozi wa Rais Samia, sekta ya kilimo cha korosho itaendelea kuimarika na kutoa tija kwa wananchi wa mikoa ya kusini.
Mnada huu umeleta nuru mpya kwa wakulima ambao wamekuwa wakitegemea korosho kama chanzo kikuu cha mapato. Serikali imeonyesha dhamira thabiti ya kuimarisha bei za mazao ya kilimo, na hatua ya leo ni ishara tosha kwamba wakulima wanapewa kipaumbele ili kuinua uchumi wa mikoa ya kusini.