Hongera Rais Samia kilo 1 ya Korosho yafika shilingi 4120

Lione hili Kwahiyo korosho za samia? wakulima waliotoa jasho lao kuzilima huwajui?
Tehe tehe tehe teheeeeee! Chadema hawaamini kama wamepigwa kanzu, kidali na tobo kabisa!! Poleni, siku nyingine muwe na adabu na watu wanaotunukiwa u-dr
 
Lione hili Kwahiyo korosho za samia? wakulima waliotoa jasho lao kuzilima huwajui?
Hata wewe wa Samia.
. Au una Rais mwengine Tanzania?

Wakulima wa korosho wa mama Samia wanafaidika kwa bei nzuri mwaka huu.
 
Hakikisha 2025 kura yako inaenda kwa Samia
 
SAafi sasa wananchi wafanye uwekezaji mzuri, mkoa unyanyuke kiuchumi
 
Una Rais wako mwengine Tanzania hii, ukipenda usipenda wewe Rais wako ni mama Samia Suluhu Hassan.

Au kuna kondoo mwenzako Rais?
 
Una Rais wako mwengine Tanzania hii, ukipenda usipenda wewe Rais wako ni mama Samia Suluhu Hassan.

Au kuna kondoo mwenzako Rais?
 
Wakazi wa Mkoa wa Mtwara wanasherehekea kwa furaha kubwa hatua ya kihistoria ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kupandisha bei ya korosho hadi shilingi 4,120 kwa kilo.

Haya sio tu mabadiliko ya bei, bali ni ushahidi wa dhamira ya Rais Samia ya kuwainua wakulima na kuleta mabadiliko chanya katika maisha yao.

Wakulima wanasherehekea kwa kusema, “Mama Samia ni rafiki wa wakulima, ni kiongozi anayejali!”

Katika sanduku la kura, wakulima hawawezi kuficha shukrani zao, wakitangaza kwa sauti moja: “Tutampa Mama Samia VEMA, TIKI ni ndogo mno, haimtoshi kwa wema aliotutendea Mtwara.”

Hii inadhihirisha jinsi Rais Samia alivyoweza kuungana na wakulima, kuleta matumaini na mabadiliko ya kweli katika kilimo chao.

Wakulima wanasema kwa ujasiri, “Mama Samia ametuwezesha kuona mwanga wa maendeleo, na kwa kupitia uongozi wake, tumejifunza kuwa na matumaini.”

Hakika, Mama Samia ni kiongozi anayeonesha mfano wa jinsi ya kuleta maendeleo ya kweli katika jamii.

Wakulima wa Mtwara wakiwa na dhamira thabiti, wanajipanga kutetea maendeleo yao kwa kumchagua Mama Samia katika uchaguzi ujao.

Huu ni wakati wa kuimarisha uongozi wa Mama Samia, ambaye si tu mkombozi wa wakulima, bali pia ni chaguo sahihi kwa mustakabali wa Taifa letu.

Tumaini letu liko mikononi mwa Rais Samia.

View: https://www.instagram.com/reel/DBHCq_9qMT4/?igsh=MWdycDE2b2ZkbDJ0Yw==
 

Attachments

  • VID-20241014-WA0037.mp4
    5.8 MB
Yeeeerrrrreeeeh!

Baada ya bei ya korosho kupaa na kuchanganya mwaka huu mbuzi kuanza kunyweshwa soda tena kama ilivyokuwa awali.

Nyau de adriz member mwenzetu yuko huko Lindi anabangua na kulangua korosho. Toka mwezi wa sita ananiringia kafanya mtihani sasa anajishughulisha na kilimo nikaja kugundua kumbe korosho.

Halafu kuna reply flani kwenye comment yangu humu aliniringishia ataoa mwarabu.

Yani huyu dogo ndo wale watanywesha mbusii soda za kutosha.

Mashirika ya kutetea haki za wanyama ingilieni kati mbusii wasinyanyasike kwa kunyweshwa sumu (soda) na hawa matajiri uchwara watarajiwa.

Nyau de adriz
 
Rais amefanya mambo mengi sana kwenye Kilimo.

Bei zimevunjwa na kuweka rekodi kwenye mazao ya Kakao,korosho,tumbaku,ufuta.

Hii bei ya koroshi ingekuwepo mwakanizkusini kulikuwa hakuna haja ya kampeni hope pia utakuwepo.

Mwisho kina Bashe futeni Yale makato wanayolalamikia pamoja na kuwapa pembejeo za Bure Kwa wakati.
 
Nyie matahira mbona nyama ilivyopanda bei hamkumpongeza huyo Samia?
Dola ilivyoshuka thamani hamkumpongeza?
Mafuta yalivyopanda bei hamkumpongeza?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…