Hongera Rais Samia kwa kujitahidi kuondoa ukakasi wa uadui wa kisiasa nchini

Hongera Rais Samia kwa kujitahidi kuondoa ukakasi wa uadui wa kisiasa nchini

Jidu La Mabambasi

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2014
Posts
16,419
Reaction score
26,594
Makamba na Kinana wamerudishiwa heshima zao.

Membe karudi CCM alikofukuzwa.

Mashitaka ya Mbowe yakafutwa.

Waliokuwa lupango kwa kesi za kubambikwa wameachiwa.

Mikutano ya kisiasa imerudi upya.

Polisi wameanza kuwaheshimu wananchi wa itikadi tofauti na chama tawala

Tundu Lissu alionana na Rais huko Ubelgiji, na sasa twasikia kalipwa stahiki zake.

Hata Sugu, ameenziwa kwa muziki wake na Birthday yake ya miaka 50.

Kwa kweli ukiona picha kubwa-The Bigger Picture- inasoma MSHIKAMANO, na SIASA SI UADUI.

Na hapo namkumbuka marehemu Mzee Rashid Mfaume Kawawa na Matembezi yake ya Mshikamano.

Hongera sana mama Samia, hata Mungu aliye juu amesema mpatanishi atarithi mbingu na nchi.
 
Hivyo vinasaidia nini kundi kubwa la wananchi???

Hatma ya tozo?bei ya mafuta?mbolea?Ni ipi

Acheneni na hoja za kijinga? Tujadili maisha na sio wanasiasa
 
Heshima kubwa sana kwake mhe. Rais Samia.

Hili ni jambo kubwa sana amelifanikisha.

Sivutiwi na Ccm lakini ni muhmu sana kuwa na siasa za kuheshimiana na kuthaminiana vyama vyote
 
Makamba na Kinana wamerudishiwa heshima zao.

Membe karudi CCM alikofukuzwa.

Mashitaka ya Mbowe yakafutwa.

Waliokuwa lupango kwa kesi za kubambikwa wameachiwa.

Mikutano ya kisiasa imerudi upya.

Polisi wameanza kuwaheshimu wananchi wa itikadi tofauti na chama tawala

Tundu Lissu alionana na Rais huko Ubelgiji, na sasa twasikia kalipwa stahiki zake.

Hata Sugu, ameenziwa kwa muziki wake na Birthday yake ya miaka 50.

Kwa kweli ukiona picha kubwa-The Bigger Picture- inasoma MSHIKAMANO, na SIASA SI UADUI.

Na hapo namkumbuka marehemu Mzee Rashid Mfaume Kawawa na Matembezi yake ya Mshikamano.

Hongera sana mama Samia, hata Mungu aliye juu amesema mpatanishi atarithi mbingu na nchi.
Kwa hili tunampongeza sn
 
Samia Suluhu angekuwa Rais mzuri Sana shida kachukua nchi iliyokuwa shimoni.Kila sehemu ni shida tupu pamoja na hayo yote kidogo mwanga upo na Mungu ampe nguvu asikate tamaa apige kazi.
 
Back
Top Bottom