Hongera Rais Samia, Kwenda US, Kuhutubia UN, Safari ya Kuzindua Filamu Yako ya Royal Tour, Tunaomba Tukusindikize, Dreamliner Yetu Itue New York

Utalii unajitangaza wenyewe kupitia watalii waliotembelea sehemu hizo na media binafsi. Mfano Serengeti nani anaitangaza kwanguvu? Tanzania kinachojulikana ni Serengeti na Mt K'njaro.
 
Wanabodi,

Kila nipatapo fursa, huwaletea mfufululizo wa makala zangu za "Kwa Maslahi ya Taifa" Makala ya leo ni bandiko la pongezi na ombi. Pongezi ni kwa Rais Samia, kusafiri kwa kukwea pipa la watu, kwenda nchini Marekani, na kuhutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, UNGA. Ombi ni kwa Safari ijayo ya Rais Samia kwenda Marekani ni mwanzoni mwa mwaka ujao, kwenda kuzindua ile filamu yako, ya Royal Tour, tunakuomba safari hiyo, usipande ndege za watu, panda ndege yetu ya Dreamliner, tena tunaomba safari hiyo itangazwe kikamilifu kabla, ili Watanzania wenye uwezo, wakiwemo wasanii, wanamichezo, wafanyabiasha na waandishi wa habari, tukusindikize kuitangaza Tanzania, na tangazo la Dreamliner yetu kutua New York, Marekani ni tangazo tosha la utalii, kuvutia Wamarekani kutembelea Tanzania. Hongera sana, Mama Samia kwenda Marekani na kuhutubia UN.

Declaration of Interest
Humu jf kuna kikundi fulani kidogo, cha watu fulani wajinga wajinga, wambea wambea na wenye wivu wa kike, ukiandika chochote kuipongeza serikali yetu au kiongozi yoyote wa serikali, wao wivu huwaka moto ndani yao , hivyo hununa, na kuanza kubeza, au hata kutukana na badala ya kujadili mada iliyo mezani, huleta viroja vya kumjadili mtoa mada kuwa pongezi hizo ni za kujipendekeza kusaka uteuzi. Naomba kama na wewe ni mmoja wa kundi hili, nakushauri uishie hapa, bandiko hatutaki umbea wa kumjadili mtoa mada, wala wivu wa kike, kuumia mtu mwingine anaposifiwa. Na declare interest openly, mimi Pasco Mayalla, huwa naandika kusifia vitu vinavyostahili sifa, sio kwa lengo la kusaka uteuzi wowote na kama kuna makosa, huwa nakosoa. Msifiaji mtafuta uteuzi, kazi yake itakuwa ni kusifu tuu, hawezi kukosoa.

Kwa Vile JPM Hakuvuka Bahari, Kitendo Cha Rais Samia Kuvuka Bahari, Kuhutubia UN, Kinastahili Pongezi za Dhati.
Kwa vile kipindi chote cha JPM, hakuwahi kuvuka bahari, na rais wa Tanzania hakuwahi kuhutubia UN kwa miaka yote mitano ya JPM, kitendo cha Samia kuvuka bahari, kwenda nchini Marekani na kuhutubia UNGA, kinastahili pongezi za dhati. Hongera sana Rais Samia.

Rais Akisafiri Media Huwa Inaonyesha Akikwea na Akitua, Hii Safari ya UN Vipi?.
Kwa kawaida rais akisafiri, huwa tunaonyeshwa picha na video za eapoti, siku akiondoka huku akionekana akipanda ndege, na siku akirudi pia tunaonyeshwa akishuka kwenye ndege, na kuandaliwa press briefing ya rais pale eapoti kutujuza kilichojiri huko. Lakini safari hii ya Mama Samia kwenda UN, hatukuonyeshwa akipanda ndege, wala akishuka kupokelewa bali tumeelezwa tuu kuwa rais atakwenda Marekani, hatukuonyeshwa akiondoka, wala akipokelewa, tukaja kuonyeshwa tayari ameishafika Marekani akijichanganya na Watanzania, akiwemo Mtanzania mwenzetu maarufu sana aishie Marekani Da Mange ndio tukajua kumbe rais keshafika.

Hakuna chombo cha habari kinachojiuliza kwanini rais asafiri kimya kimya, apokelewe kimya kimya na kuibuka tuu. Sababu ni moja, rais kasafiri kwa ndege za mashirika ya nje hivyo sio busara kumpiga picha rais wetu akikwea pipa la watu, wenyewe hawapendi na usumbufu kwa abiria wengine.

Kama Tanzania Tuna Ndege Zenye Uwezo wa Kufanya Direct Flights to US, Kwanini Rais Wetu Apande Commercial Flights?.
Enzi za Mkapa na JK, mimi nikiwa mwandishi wa habari wa kujitegemea, wakati wa safari za mbali za rais wetu, vyombo vya habari tulialikwa kumsindikiza rais wetu, na alikuwa anaandamana na kundi kubwa la wafanyabiashara. Enzi hizo pia rais wetu alipanda ndege za mashirika mengine kwasababu wakati huo, Tanzania tulikuwa hatuna ndege zenye uwezo huo.

Lakini kipindi cha JPM, Tanzania imejenga uwezo, sasa Tanzania tuna ndege kubwa za abiria za masafa marefu, kwanini rais wetu aendelee kusafiri na ndege za mashirika mengine, wakati sisi tunalo shirika letu, ATC, tunazo ndege za masafa marefu, Boeng na Airbus “The Dreamliner”?. Why?!. Hii ni aibu!. Ile siku sisi waandishi tulipopata fursa ya kumuuliza maswali JPM, pale Ikulu, nilipopata nafasi, kabla ya kuuliza swali, nilitoa hoja ya waandishi tushirikishwe kwenye mambo ya kuitangaza vizuri nchi yetu, na mimi nikasema waandishi tutajitegemea, kwa usafir chakula na malazi. Nimesafiri sana na Mkapa na JK, hivyo hii sasa ni zamu ya Samia, akisafiri safari za kimataifa, itolewe fursa kwa vyombo binafsi na wafanyabiashara kuandamana na rais.

Bila hata kusubiri majibu ya serikali au ya ATC, sababu pekee iliyomfanya rais Samia kusafiri kwenda Marekani kwa ndege za abiria za mashirika mengine, ni kwasababu kwanza ATC haina route ya Marekani, pili kupeleka mdege mkubwa, kama Dreamliner Marekani ni gharama, mafuta na landing charges ambazo zinalipwa kwa saa, hivyo huo mdege umpeleke rais Marekani, umsubiri kwa siku atakazokazokaa huko, na kumrudisha, ukilinganisha na kama akipanda ndege ya abiria kama wasafiri wengine, usafiri wa ndege za abiria ni nafuu kuliko kuipeleka Dreamliner Marekani.

Kutangaza Utalii Kimataifa ni Ghali, Hakuna Kitu Kinaongoza Kutangaza Utalii Kama Usafiri wa Ndege
Kama ilivyo katika kutangaza utalii, kuandaa filamu ya utalii na kuitangaza katika vyombo vya kimataifa, ni ghali, lakini kama tunataka kukuza utalii, hatuwezi kuepuka gharama, ndio maana tumekubali rais wetu kurekodi filamu ya Royal Tour kuutangaza utalii wetu. Hakuna kitu kinachoongoza kuvutia utalii, kama usafiri wa direct flights. Hakuna kitu kingeitangaza Tanzania nchini Marekani, kama ndege ya ATC kutua uwanja wa ndege wa New York, nchini Marekani huku imembeba rais wa Tanzania.

Rais wa Tanzani kwenda nchini yoyote ikiwemo Marekani kwa ndege ya watu wengine, wakati ATC inazo hizo ndege ni aibu, ni kosa, kosa sio kufanya kosa, kosa ni kurudia kosa, muda wowote mwakani, kuanzia miezi ya mwanzoni, rais Samia atakuwa na ziara rasmi ya kutembelea Marekani, ambapo katika ziara hiyo pia rais Samia ndio ataizindua rasmi ile filamu yake ya Royal Tour, naomba sana, tusifanye tena kosa la rais wetu kusafiri kwa ndege za watu, tusirudie kosa kwa rais wetu kutua Marekani kwa ndege za watu wakati sisi wenyewe tunazo hizo ndege na uwezo wa kulirusha li Dreamliner letu likiwa full board kwenda Marekani, tunao.

Kitu cha kufanyika ni kabla rais hajafanya ziara nchi yoyote, zille taasisi zote zinazohusika na shughuli mbalimbali ziarifiwe rasmi, ili ziandae trips. Mfano baada tuu ya kujua filamu ya Royal Tour inayo muonyesha movie Star wa Tanzania, Chief Hangai, itazinduliwa lini, nchini Marekani. Na tunajua Dreamliner inabeba abiria 300, ukiondoa rais na ujumbe wake wa kiserikali, say ni watu 30, kwanza serikali inatangaza fursa kwa taasisi zote za umma, wenye issues zozote za kufanya Marekani, wapange hizo issues zao zifanyike kipindi hicho. Waserikali hao, wafanye booking ATC. Then ATC inatangaza excursion trip ya Marekani kwa nafasi zote zilizobakia, hivyo trip ina correspond na siku za ziara ya rais kwenye nchi hiyo, lets say ni ziara inakayodumu siku 7. Inauza hizo nafasi zilizobakia kwa wafanyabiashara wa sekta binafsi, au Watanzania wengine wowote wenye uwezo, tukiwemo sisi waandishi wa habari.

Dreamliner Yetu ikitua JFK, Utaungaza Vizuri Utalii Wetu Kuliko Tangazo Jingine Lolote!.
Hivyo Taarifa tuu kuwa rais wa Tanzania, ametua Marekani na dege la Dreamliner la Tanzania, akiandamana na ujumbe wa watu 300!. Hili ni tangazo tosha la utalii kimataifa, kwasababu hakuna ndege yoyote ya direct kutoka Marekani hadi Tanzania, hivyo ATC pia itapata fursa ya kuanzisha route ya Marekani na nawahikishia ndege itajaa!.

Paskali
Rais kaenda na wafanyabiashara Sasa shida yako nini?👇

Screenshot_20210920-151938.png

Screenshot_20210920-151722.png

2938478_9C54C963-C05D-4860-8CFA-0279A8FBAB82.jpeg

2938479_07CE890F-0FCD-48FB-B22A-08EE1605E32F.jpeg
 
Pascal wewe ni mwanasheria kutumia neno la wivu wa kike ni uzalilishaji wa kimamama au wanawake .umenisonesha sanaa. Omba msamaha.
 
Mzururaji tu uyo

Ila Paskal nimekusoma vizur na kama ile kamati ya bunge ikikusoma vizuri basi 77 na 88 ijayo kampuni yako haitopewa tenda na utarudi kwenye njaaa kali kama ulivyokuwa katika awamu 5
 
Mama Samia kaamua kufanya suprise, video ya kwanza ni selfie ya Dada Mange kule USA. Mama hakutaka publicity iambatane na safari yake tena ndefu.

Kuongoza hizi nchi za afrika ni kazi ngumu sana. Mama sasa anachimbwa ili watu wajiridhishe kama kaenda kaenda US na kundi la wafanyabiashara au la. Nongwa ni nyingi mno.

Kwenda US ni kelele kutokwenda kama JPM na kwenyewe ni kelele nyingi tu.

Kwani mkuu SSH au JPM wafanye lipi linaloweza kukufanya wewe kupiga kelele?

Wewe si ni wale ambao hata mkifanywa vipi - hamkatai?
 
Nimeishia kusoma pale uliposema wenye wivu tuishie hapa kwa sababu hata mimi nilidhani unasaka uteuzi.

Ila kwa vile umeshasema husaki uteuzi, nitakuwa nasoma mada zako zote kwa sababu najua uteuzi ni kitu kidogo kwako, hata ukipata unajikatalia.
 
Tusaidiane ndugu zangu kwani ni kipi kinasababisha utalii Tanzania kususua ,Je ni Boing kutokutua USA ikiwa na Chifu Hangaya? Na kama angetua nayo basi watalii wangemwagika kama mafuliko.Tusidanganyane sekta ya utalii Ina matatizo makubwa sana hasa Kodi na matazo ya ajabuajabu kama haya mambo yasipolekebishwa hiyo Loyal Tour itakua ni bule tu.
Ushauri wangu Serikali kupitia Wizara ya utalii kaeni na wadau wa utalii Wana mengi ya kuwaeleza ili mfikie Sulihisho na hatimae sekta ikue.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Utalii unajitangaza wenyewe kupitia watalii waliotembelea sehemu hizo na media binafsi. Mfano Serengeti nani anaitangaza kwanguvu? Tanzania kinachojulikana ni Serengeti na Mt K'njaro.
Waambie ukweli mchungu.Wizara ya utalii wake na wadau wa utalii Wana matatizo yao Tena makubwa hasa makodi makubwa .naamini hizo shida zikitatuliwa basi watalii watakuja wengi Sana na Nchi itapata faida ingawa ni kweli pia sekalta ya anga nayo ni mhimu Sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom