Hongera Rais Samia, Kwenda US, Kuhutubia UN, Safari ya Kuzindua Filamu Yako ya Royal Tour, Tunaomba Tukusindikize, Dreamliner Yetu Itue New York

Extremely rubbish print from you! Kwamba kwakuwa JPM hakwenda huko na huyu kaenda ndio kafanya jambo kubwa? Now I don't wonder why most of JF Jukwaa la Siasa contributors make a lot of fun of you!
 
Pascalli unamsifia mtu anayedanganya watu yaani wewe Mzee umekuwa mchawi unatuaminisha sisi watanzania namnagani elimu zetu zilivyombovu yaani kizazi cha KINAFIKI
 

Paskali unafahamu vigezo na masharti ya USFAA kwa Shirika la ndege la nje kupewa clearance ya kuanzisha direct flights kwenda Marekani ? Hebu fuatilia kwanza ujue Kenya Airways ilichukua miaka mingapi application yao kukubaliwa mkuu ? Hawaangalii upya wa ndege zako tu ,fuatilia utupe majibu.

In 2013, Kenya applied to the US Federal Aviation Administration (FAA) to be considered for Category One but the application was rejected. In 2014, the rejection was upheld following an audit of Jomo Kenyatta International Airport (JKIA) which indicated the airport was not fenced, there was no separation between arriving and departing passengers and that there were houses built too close to the airport. The airport administration took several steps that saw JKIA qualify for accreditation of Category One in February 2017. Read more: List of African countries with direct flights to the United States of America
 
Mkuu Bravo Mike, kwanza asante kutuletea vigezo vya USFAA, ila sisi Tanzania tuna mkataba wa Anga Huria na Marekani, hatuhitaji kuomba kibali kingine chochote zaidi ya notification for landing clearance.
P
 
Tatizo waafrika wengi wanaweka mbela hisia zao badala ya Tafiti za kisayansi.
Hivi kwenye Mkutano mkubwa wa marais wa nchi zaidi ya mia moja nani atapoteza muda kutangaza ndege kutoka Tanzania? Na je, tukio hilo litarudiwa Mara ngapi kwenye vyombo vya habari vya Magharibi ?

Kosa kubwa la serikali kutumia zaidi ya Tril.1 kununua ndege ni jambo lililoisababishia nchi hasara kubwa sana. Akina Paskali wanaona aibu kuweka waza misimamo yao juu ya hasara kubwa iliyosababishwa na awamu ya tano na sasa inaendelezwa na awamu ya sita.

Hivi MTU mwenye nia njema kabisa na watu wake anaweza kutumia tril. 1 kununa chombo cha usafiri wakati vijana wanajenga mabanda ya mbao kwenye barabara kwa kukosa maeneo ya kufanyia biashara. Kwa kukosa mipango wanageuka na kuwaita wamachinga wakati wamejenga fremu na hawafanyi biashara ya kutembea Bali ni maeneo waliyojijengea na kila mmoja ana miliki kibanda chake juu ya mtaro na wengine wanauza mpaka bia sehemu isiyo na choo.

Tril. 1 ingeweza kujenga Nyumba za watumishi wa umma zenye thamani ya sh. Mil 1 kwa kila nyumba ,zaidi ya nyumba elfu kumi. Jiji la Dodoma lingekua halina tatizo tena la nyumba bora za kuishi watumishi wa umma. Na kwa kutumia NHC nyumba hizo zingekua zinalipiwa pango kwa bei nafuu au zingekospeshwa kwa kwa kulipa kidogokidogo ili hatimaye watanzania wawe wanaishi kwenye nyumba bora zenye huduma muhimu zilizojengwa kwa kuzingatia ramani ya jiji.
Wizi mkubwa na rushwa serikalini na hata kwenye mashirika ya umma na binafsi unatokana na ukweli kuwa kila mfanyabishara au mfanyakazi anawazi kujenga aondokane na adha ya wenye nyumba. Matokeo yake ni ujenzi usiozingatia ramani za mipango miji.
Ujenzi usiozingatia mipango miji sio maendeleo endelevu kwani miaka ijayo miji iliyojengwa hovyo itabidi ivunjwe ili pafanyike ujenzi wa majengo marefu kama Yale ya magomeni ili kupunguza uwezekano wa ardhi yote ya nchi kuwa makazi. Kwa maana kwamba watu let say mil. 150 wenye Sera za ujamaa na kujitegemea wanaowaza kila mmoja kumiliki nyumba kuepukana na kodi kubwa inayoongezela bila udhibiti ,hii ina maana kuwa nchi nzima itakua ni makazi ya watu. Wakati huo huo kuna vyanzo vya maji na hifadhi kwa ajili ya wanyama na misitu. Uharibifu wa mazingira n.k. litakua ni taifa la ajabu. Hili Watawala hawalioni wala vyama vya siasa na hata NCCR Mageuzi waliokua na Sera nzuri ya makazi hawalizungumzii tena.

Serikali ziwekeze kwenye makazi ya watu. Ndege zipo tu na hakuna MTU aliyeshindwa kuja Tanzania au kwenda Nje kwa sababu ya kukosa usafiri. Ndege zipo nyingi sana zinakosa mpaka abiria tatizo ni kukosa mbinu za kuitangaza nchi na sio ndege.

Hivi yale matshrt ya Vyama yangechomwa moto na kutengeneza T-shirt zenye maandishi ya kutangaza mlima Kilimanjaro ,Tanzania ,Zanzibar, Ngorongoro. Mikumi ,Pangani, Bagamoyo, Kilwa Masoko. Liwale n.k ikawa ni kama jadi yetu kuzivaa na kwenye makongamano mbalimbali badala ya matsht ya vyama. Na iwe kila mtalii anayeingia Tanzania anapokua ameliingizia Taifa zaidi ya sh.500000 awe anapewa zawadi ya Tshrt , mbili au tatu ili akawape marafiki zake huko Ulaya . Tungekua tumeitangaza nchi kwa kiwango cha juu sana.

Sent from my TECNO L8 Lite using JamiiForums mobile app
 
Huu ni mwendelezo wa bandiko hili
P.
 
Nimetoa mchango wangu wa mabandiko mawili kuhusu uzinduzi wa filamu ya Royal Tour.
Bandiko la kwanza ni hili

Na bandiko la pili ni hili

Nautakia uzinduzi mwema wa Royal Tour siku ya Jumatatu ya Pasaka.
Paskali
 
HBD Rais Samia!.
P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…