sammosses
JF-Expert Member
- Jan 24, 2011
- 1,687
- 1,111
Hongera mh. Rais Samia kwa mtazamo na maono yako kuzingatia misingi na falsafa za maridhiano. Safari hii ni ndefu sana ambayo bado naviona visiki kwenye msamaha wa mikutano ya hadhara ambayo ilizuiwa kwa upande mmoja ili kudhoofisha upande wa pili.
Nakupongeza kwa kuwa umezingatia misingi niliyoitaja hapo juu,japokuwa misingi hiyo haikujengwa kwa mamlaka ya sheria,kama ilivyo ilivyoadhibiwa bila kufuata mamlaka na msingi wa kisheria.
Pamoja na uhuru huu bado umewapa nguvu unao waita chawa wako kujibu mashambulizi bila kuainisha aina ya ujibuji mashambulizi hayo,hii maanake umefungua wigo mpana wa kuendeleza siasa za kushugulikiana bila kujali msingi wa sheria za vyama vingi nchini.
Kuwanyima wananchi haki yao ya kupata habari kupitia mikutano ya hadhara kwa kipindi chote,kumeendelea kudhoofisha demokrasia kwa takribani miaka sita,haki ambayo ni msingi wa haki za binadamu.
Lakini pia hakufungua wigo mpana wa kudhoofisha tasnia ya habari kutoa habari zao kwa uhuru badala ya habari hizo kuhaririwa kwanza. Na bila kuzingatia msingi wa sheria ya uhuru wa habari kikatiba,hakuna agizo lolote linaloelekeza kuzitazama sheria kandamizi zinazo ondoa uhuru wa vyombo hivi.
Huenda ndiyo mwanzo mzuri wa kufungua wigo mpana na utokomezaji wa sheria kandamizi,lakini jambo hili limeviathiri sana vyombo vya habari na kuondoa haki ya wananchi kupata habari za kiuchunguzi toka vyombo hii ambavyo ni mhimili wa nne wa dola usio rasmi.
Pia watunga sheria niwakumbushe kuwa iko siku sheria hizi wanazo tumia kuwabana wapinzani wa kisiasa,ambazo zimetungwa na ninyi kwa majority yenu iko siku zitageuka verse versal kwa kuwa sheria ni msumeno ila kwa kuwa kuna upendeleo mkubwa wa vyombo vya dola unakuta inaumiza upande mmoja.
Kuna haja sasa ya kuliangalia suala hili kwa mapana sana hasa katika kipindi hiki cha kuondoa zuio batili la mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa. Maanake nini,Bunge lifanye mabadiliko ya sheria ya vyama vya siasa kuhusiana na agizo la vibali ambalo limekuwa likitumiwa vibaya na vyombo vya dola kuvidhoofisha vyama vya upinzani.
Jambo hili litazama kwa mapana yake kuondoa chuki,dhuluma na matumizi mabaya ya rasilimali muda dhidi ya rasilimali watu.
Mwisho kwa hoja hii niwatakie maendeleo mema kwa mijadala ya maridhiano,lakini kuviasa vyama vya siasa kujikita zaidi katika utatuzi wa matatizo ya wananchi na ugatuaji wa madaraka unapelekea kuhuisha ufisadi uliotamalaki.