Hongera RC Makalla, hakika vibanda vya Machinga ulikuwa ni uchafu

Hongera RC Makalla, hakika vibanda vya Machinga ulikuwa ni uchafu

Hongera RC........................tujitahiidi isiwe nguvu ya soda,maana hawa jamaa huwa wanaanza kutejea taratibu tukisha sahau
 
Poleni sana wadogo zangu wa CBE,DIT na IFM hao wauza mihogo,chips na mama ntilie walikuwa wana saidia sana kupunguza Ugumu wa maisha
Yaani nimewawaza sana hawa madogo,kula yao sasa inarudi kuwa ya shida sana
 
Yule mzee mtu anaemuongelea utumbo najiskia kutapika yani😅!!! Jamaa amefanya vitu vinavyoonekana sikazi ingalikuwa kiongozi wa Calibre ya JK miradi ingechukua miaka hata 30 kukamilika
Akili mingi sana we jamaa.
Chuma bana huhitaji darubini kuona alichokifanya.Mtu na nusu
 
Everton walikuja Dar waliletwa na SportPesa basi gazeti moja la uingereza likaandika kuhusu hiyo mechi...wakasema "in a fishing village of Dar es Salaam"....niliona jamaa wanatudharau sana yaani jiji letu wanaliita kijiji cha wavuvi....ila nikitizama mabanda ya wamachinga yalivyo kila mahali naona walikuwa sahihi...kuita kijiji cha wavuvi.....
Utaratibu ni muhimu, hivi kuna mtalii gani atakuja kutazama mabanda kona labda wapenda slums...
 
Dar ilikua inachukiza sana aisee lakini pamoja na hayo yote ilikua inahesabika miongoni mwa majiji masafi Africa kwenye kumi bora. Saizi Dar itakimbiza vizuri sasa labda watatuzidi Kigali na Capetown tu hahahahaaa

Jiji likisafishwa na vibanda kutokomezwa hata kigali hawatufikii
 
Lakini tukumbuke ktk shida ya ajira hao machinga ambao Leo mnafurahia kuwa wamefukuzwa mjini ni vijana graduates ambao wamekosa ajira hawajapenda kupanga vitu barabarani ila ni maisha ....mpango mzima wa hili swala sijaona ukizungumza ni jinsi watawasaidia Hawa machinga warudi ktk hali yao ya kawaida.....Sasa wanaugulia maumivu makali ya kiuchumi na tukumbuke wengine wanafamilia.....na hapo hapo wanasiasa wanazungumza watu wajiajiri .....nyinyi ambao mnafurahia mji kuwa msafi pengine mna ajira zenu maofisini lakn hamuangalii maumivu wanayopitia wenzenu ...jadirini ni kivipi serikari itapunguza tatizo la ajira...kwani magufuri alikuwa ajui kuwa mji ni mchafu alikuwa anajiuliza wanaenda wapi...mnafurahia lakn hamjui impact yake inaweza kuongeza ualifu.....
Jiwe ndiyo chanzo cha haya yote. Jiji haliwezi kuwa kama wanaishi ng'ombe au mashetani kama alivyokuwa anataka.
 
Lakini tukumbuke ktk shida ya ajira hao machinga ambao Leo mnafurahia kuwa wamefukuzwa mjini ni vijana graduates ambao wamekosa ajira hawajapenda kupanga vitu barabarani ila ni maisha ....mpango mzima wa hili swala sijaona ukizungumza ni jinsi watawasaidia Hawa machinga warudi ktk hali yao ya kawaida.....Sasa wanaugulia maumivu makali ya kiuchumi na tukumbuke wengine wanafamilia.....na hapo hapo wanasiasa wanazungumza watu wajiajiri .....nyinyi ambao mnafurahia mji kuwa msafi pengine mna ajira zenu maofisini lakn hamuangalii maumivu wanayopitia wenzenu ...jadirini ni kivipi serikari itapunguza tatizo la ajira...kwani magufuri alikuwa ajui kuwa mji ni mchafu alikuwa anajiuliza wanaenda wapi...mnafurahia lakn hamjui impact yake inaweza kuongeza ualifu.....
Kwani si wamesema waende maeneo rasmi yaliyotengwa au ni sound tu?
 
Amos Makalla anaupiga mwingi haswa.......

Kitu kimoja wengi wasichokijua ni kuwa mh.Mkuu wa mkoa ana hulka ya "USIKIVU SANA"...KUJISHUSHA SANA....na UTEKELEZAJI MKUBWA na si "pang'ang'a"

Kongole kwake [emoji123][emoji106]

Siempre JMT
"Pang'ang'a", hiki ni kimatumbi chetu au.....hapa umeniacha njani Jumbe.
 
Back
Top Bottom