Hongera Samia kwa kumfanya Majaliwa kuwa Waziri Mkuu

Hongera Samia kwa kumfanya Majaliwa kuwa Waziri Mkuu

NIMEONA

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2019
Posts
3,862
Reaction score
5,693
Kwa jina la JMT, nawasalimu sana!

binafsi, nafasi ya waziri mkuu ni moja ya nafasi ninayoiheshimu sana na kuiogopa.......tangu nilipopata akili ya kufuatilia mambo ya siasa, mpaka sasa! nikisikia 'Waziri Mkuu', basi picha inayonijia akilini ni;
  • Ukali (kwa wazembe),
  • Uwajibishaji (kwa wakosefu),
  • Amri (yenye mamlaka tele),
  • kujiamini,
  • kauli thabiti na yakini (zisizo na chembe ya uongo)
  • utii
  • ufuatiliaji n.k

Hayo yote, kwa kiasi fulani niliyashuhudia katika awamu nilizobahatika kuziona....mh sumaye, mh lowassa (hata kama ilikuwa kwa kipindi kifupi sana) na mh pinda.

katika awamu ya kwanza ya uwaziri mkuu wake, mh majaliwa, kiukweli (kwa mtazamo wangu), alikuwa kama mtu mwenye wasiwasi mno asiyejiamni sana. sina uhakika kama kauli, 'nitapiga mpaka shangazi zako' nayo ilichangia kwa kiasi fulani au la. hebu tupitie viashiria vichache vifuatavyo, kwa mtazamo wangu, vinavyoonyesha kuwa hakuwa ni mtu wa kujiamini n.k.

1. aliwaambia wananchi wake wa kusini, 'limeni kwa wingi sana mbaazi soko lipo'!
hii kauli kiukweli inawatesa watu wa kusini hadi kesho wakiikumbuka. wananchi, wakiwa wamejawa na matumaini tele juu ya kauli hii iliyotolewa na mtoto wao, tena akiwa ametoka kuteuliwa kuwa waziri mkuu. ajabu ni kuwa bei ilishuka kutoka 3000 aliyoikuta hadi 150 na bado wateja walikosekana. walipolalamikia hali hiyo kwa mheshimiwa raisi (r.i.p), alitokea waziri mmoja mdogo na kuwajibu, 'mbaazi ni chakula kizuri chenye protini, kuleni!'. wananchi waliishia kuziacha tu huko mashambani na kupoteza nguvu kweli kweli.

cha kujiuliza hapa ni kwamba hakuwa na taarifa au ilikuaje? jibu pekee niwezalo kulifikiria hapa ni kuwa hakushirikishwa katika 'maamuzi mengine' yaliyokuwepo kichwani kwa mkubwa wake......zigo likamwangukia na naamini kama mtu mzima, atakuwa alijisikia vibaya sana kutotimia kwa kauli yake. pm aseme kisichotimia?

2. kutangaza sukari iuzwe tshs.1,800/= nchi nzima

hata sielewi hapa ilikuaje, lakini ninahisi kama alilazimishwa tu na mkubwa wake atangaze hivyo. nilikuwa namuangalia siku ile ya kutangaza hivyo na kiukweli sura yake na lile agizo vilikuwa vitu viwili tofauti. sukari haikushuka kamwe!!!

3. kulitangazia taifa kuwa, 'raisi ni mzima, anachapa kazi na anawasalimu sana' ilhali alikuwa mgonjwa!

hili kila mtu analikumbuka vizuri, sina haja ya kusema sana.
huu unaweza kuwa ni ushahidi mwingine kuwa mheshimiwa kipindi kile alikuwa hajiamini kabisaaa. ninachokiona katika kuongea kwake vile ni hofu iliyomjaa juu ya mh raisi (r.i.p) aliyekuwepo. ni kama vile alikuwa anaijua hali halisi na alitamani kusema ukweli lakini alikuwa anajiuliza, 'akiamka itakuaje?!!', mwishowe akajikuta anasema alichosema.

Majaliwa wa sasa!

  • Anajiamini hadi ananawiri katika nafasi yake,
  • Ana kauli thabiti zisizoteteleka,
  • Anaheshimika na kuogopeka kama pm (kitu ambacho ni kizuri kabisa)
  • Haongei kwa kuzidisha wala kupunguza (hana hofu) n.k

Hata ukipitia mitandaoni utaona jinsi watu wanavyomuelewa sasa, wanachosahau tu (au kufanya makusudi kwa sababu za chuki, wivu, husda au chochote kile) ni kuwa kuna mtu anayemfanya awe hivyo, na huyo ni MAMA SAMIA SULUHU HASSAN.

ahsante sana mama samia suluhu hassan kwa kumfanya mh. kassimu majaliwa kassimu kuwa pm wa ukweli.

Mungu ibariki Tanzania,
Mungu ibariki serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan
 
Kama benchi lina misumari, busara ni kuinuka kutolikalia. Bahati mbaya pamoja na kuambiwa atapigiwa hao mashangazi wake aliufyata ili kikombe chake kisijae ‘nzi’ badala ya uji
 
Majaliwa kaona "gap" kule juu ndio analitumia, kamuacha aendelee kuimba yeye mwanamke.
Tunaendelea kuheshimu mtazamo wako. Nafikiri huo ndo utakuwa wimbo wa haters kwa sasa, katika kujaribu kujipoza na maumivu ya upigaji mwingi wa mama!
 
Sijasikia kiongozi!
Ila ya JPM yote ulitega masikio na kuyasikia,ila ya juzi hapa wizara ya fedha hukuyasikia.

Inaelekea yule mzee alikukuna sana au we ni mjane wake wa siri??
 
Kuna mambo mengine yanakela basi tu

Hizo sifa unazotoa umefikilia kabla ya kuazisha uzi?

Waziri yupo tu kabaki anapiga kerere wateule wanamuangalia tu wala hawshituki

Twambie mabasi ya mwendo kasi nini kiliendelea, bank kuu, na baadhi ya sehemu anazo pita na kuacha maelekezo.?
 
Back
Top Bottom