HONGERA SANA AFISA MTENDAJI WA MTAA WA NYERERE HALMASHAURI YA MJI WA BUNDA

HONGERA SANA AFISA MTENDAJI WA MTAA WA NYERERE HALMASHAURI YA MJI WA BUNDA

Mjukuu wa kigogo

JF-Expert Member
Joined
Sep 19, 2023
Posts
445
Reaction score
1,094
Sasa unaingia mkoa wa Mara!Utakutana na maandishi yakiwa kwenye hiki kibao mara tu unapoiacha Simiyu na kuingia mkoa wa Mara.Jina la mkoa halijulikani sana ukilinganisha na jina la makao makuu ya mkoa,Musoma.Ndio maana wengi wanajua jina la mkoa ni Musoma!Huu ni mkoa ambao mfumo dume ni mahali pake.
Sasa tuje Bunda hii Inajulikana zaidi kama wilaya ya "kazi".Za chini ya kapeti hii wilaya ina zaidi ya Guest House 600.Ndio zaidi ya 600!Yaani hata ukiwa na 1500/=unapata chumba!Sasa ukiwa halmashauri ya mji wa Bunda kuna mtaa mmoja unaitwa Nyerere.Huu mtaa upo katikati ya mji ukiwa umezungukwa na soko kuu,uwanja wa mpira na stand kuu ya magari.Lakini pia ni mtaa ulio karibu na Barabara kuu ya Musoma-Mwanza.Hili ni eneo ambalo familia nyingi hazikufanikiwa kuwekeza kwenye elimu Wala shughuli rasmi mfano kilimo nk Asilimia kubwa ya wakazi wake wanaishi kiujanja ujanja tu.Kuanzia watoto,vijana mpaka wazee ni ujanja ujanja tu.Wale mliowahi kuishi manzese kule dar es salaam,mabatini Mwanza au Sakina Arusha nature ya hayo maeneo ni copyright ya mtaa wa Nyerere .Yaani huu mtaa akili kumkichwa yaani kipindi cha nyuma ulikuwa ukiingia kiboya boya utauziwa dhahabu feki hata na mtoto wa darasa la pili C..It's not a joke!!
Binafsi kwa leo nimejisikia kutumia jukwaa hili kumpongeza Afisa mtendaji wa huu mtaa kwa kuweza kuumudu vizuri kuanzia mawasiliano yake mazuri na raia wake.Kwa kuanzia tu hata akialika mkutano mwitikio wa raia ni mkubwa, kafanikiwa kwa kiwango kikubwa kudhibiti vitendo vya kihalifu ambapo mbali ya kushirikisha vyombo vya usalama katumia weledi wake kushauri kundi kubwa la jobless ambao sasa utawakuta wapo car wash centres wakijishughulisha,kafanikiwa kuongeza ushawishi wake kwa anaowatawala lakini kubwa zaidi ni bidii na nidhamu katika majukumu yake.
Ni aina ya kiongozi ambaye mbali ya uchapakazi wake mzuri,mbali ya heshima yake kwa wanajamii kafanikiwa kuwaunganisha vizuri wakazi wa eneo hili pasipo kujali utofauti wa itikadi zao za kivyama.
Huyu ni binti ambaye wengi walitegemea atafeli na kutawala Kwa mihemko pengine kutokana na kuwa mdogo kiumri.
Kiuhalisia nimempongeza sana huyu binti kutokana na nature ya ugumu wa eneo husika,watangulizi wake wengi walifeli yeye kaonyesha njia nzuri.

Imani inanituma kuamini kabisa anafaa kushika nyadhifa za juu zaidi za kiongozi na kuleta maendeleo kwa Taifa kama mamlaka za uteuzi zitamuamini.Na tuombe tu mamlaka zimuamini Kwa faida ya wengi!
Binti anaweza sana kikubwa wananyerere msimuangushe💪
 
Back
Top Bottom