Hongera sana Jeshi la Polisi kwa kutumia busara kubwa badala ya nguvu

Angalizo.

Kuna mfano hai wa mtu aliyewahi kushabikiwa na watu hapa Tz. Askari wakawa wanazuia hata jambo dogo kama kubebwa kwake, Nyerere akaagiza askari waachane naye wafanye watakavyo ila wasivunje sheria.

Hakubebwa tena na umaarufu ukakata.

Askari wakiendelea na approach hii CDM na Lisu umaarufu wao utakufa natural death.

Nahisi hivyo.
CDM, wala LISU, umaarufu wao hauwezi kufa kwani wafuasi wao bado watakuwa na itikadi zao mioyoni!! Unaweza kuua vyama au mtu lakini huwezi kuua itikadi!! Sema kuna umaarufu mwingine unampatia mtu bila wewe kujua, ukidhania kuwa una mkomoa!!! Lisu licha ya kuwa mwanasiasa ni mwanaharakati kindakindaki hasa!! Akisimama jukwaani kwa siasa zetu hizi, ni vigumu sana kwa mlengo mwingine kuvumilia, kwani mala nyingi anaongea facts ambazo kuzijibu lazima utulie, sasa upande ule mwingine lazima tu watauita UCHOCHEZI!! Na hapo sasa ndio mvulugano na polisi utaanza, itaonekana anaonewa!! Kuna lundo la kesi linalomsubilia mahakamani!! NI MUDA AMBAO BUSARA ZAIDI INATAKIWA. au waamue tu kumuacha kwanza uchaguzi uishe ndio hayo mambo mengine yafuate tena kwa kuonyesha haki inatendeka. Kwani kwenye kampeni ni muda wa mambo mengi
 
Ukielewa vyombo vya dola vinavyofanya kazi, huwezi kuvipa lawama zozote.

Jeshi la polisi ambalo leo linazuia hata vikao vya watu 10, ndio lile lile lililosimamia usalama wa operation Sangara ya CHADEMA nchi nzima.

Majeshi siku zote yanaimba nyimbo za watawala, ukiona wanaimba Reggae ujue watawala ndio wanaomba mchakamchaka, ukiona wanaiba RnB ujue wameambiwa twendeni taratibu.
 
Asubuhi nilitoa mada yenye kichwa "Tunasubiri kuona busara ya jeshi la polisi wakati wa kurejea kwa Lissu"

Niseme wazi kwa mara ya kwanza jeshi la polisi limetumia busara kubwa kutozuia na kuingilia mapokezi ya Tundu Lissu.

Hiki ndicho wengi tulikuwa tuna kitaka. Polisi wakijiweka kando katika shughuli za kisiasa na kijamii huwa hakuna vurugu wala madhara mpaka pale wao wanapofika na mabomu yao, virungu na bunduki kuanza kutumia nguvu kwenye dhughuli zisizo kuwa na vurugu.

Kwakweli kuna haja ya jeshi kuendelea na utamaduni huu. Waacheni watu wafanye shughuli zao za kulia na kucheka bila kuwaingilia kwa kisingizio cha mikusanyiko.

Kwa muda mrefu polisi na CDM wamekuwa kama wake wenza wanao gombea mume kila siku vitisho na ugomvi polisi wakiwa ndio chanzo. Polisi kwa leo mmeonesha busara kwa mara ya kwanza.

Namsifu pia mkuu mpya wa mkoa wa Dar es Salaam kwa busara kubwa aliyo ionesha kama mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa. Ingekuwa ni yule bwana masifuri leo ingekuwa ni vilio na kusaga meno. Well done!
Kabisa naunga mkono hoja,mkuu wa mkoa ameonesha alivyo kuwa anajielewa
 
Asubuhi nilitoa mada yenye kichwa "Tunasubiri kuona busara ya jeshi la polisi wakati wa kurejea kwa Lissu"

Niseme wazi kwa mara ya kwanza jeshi la polisi limetumia busara kubwa kutozuia na kuingilia mapokezi ya Tundu Lissu.

Hiki ndicho wengi tulikuwa tuna kitaka. Polisi wakijiweka kando katika shughuli za kisiasa na kijamii huwa hakuna vurugu wala madhara mpaka pale wao wanapofika na mabomu yao, virungu na bunduki kuanza kutumia nguvu kwenye dhughuli zisizo kuwa na vurugu.

Kwakweli kuna haja ya jeshi kuendelea na utamaduni huu. Waacheni watu wafanye shughuli zao za kulia na kucheka bila kuwaingilia kwa kisingizio cha mikusanyiko.

Kwa muda mrefu polisi na CDM wamekuwa kama wake wenza wanao gombea mume kila siku vitisho na ugomvi Polisi wakiwa ndio chanzo. Polisi kwa leo mmeonesha busara kwa mara ya kwanza.

Namsifu pia mkuu mpya wa mkoa wa Dar es Salaam kwa busara kubwa aliyoionesha kama mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa. Ingekuwa ni yule bwana masifuri leo ingekuwa ni vilio na kusaga meno. Well done!
Masifuri Ziiiiii😀
 
Mbadala tusifie Nguvu ya UMMA nnawasifia vegetable police
 
Tusijidanganye,hawa majamaa waliona kuna viongozi wa kimataifa kwa ajili ya huu msiba wakaona heri wasifanye vurugu ikaleta picha mbaya
 
Kabisaa hapa jama walipiga hesabu wakaona hasara ni nyingi kuliko faidaa...
 
Sote tunajua Jeshi la Police lina weredi, na ukitaka kuhakikisha we ongea na askari mmoja mmoja uone comments zao utashangaa!! Tatizo ni hawa wanasiasa....ila asante WAJUMBE wa Kigamboni amani na iwe kwenu....kazi mliyoifanya ni kubwa mno.

Nafikiri angekuwepo leo asingekubali pua ya mwana CHADEMA isogee pale airport. Sasa hivi tungekuwa tunaongea mengine maana airport ingegeuka uwanja wa vita

Hii ndiyo Tanzania tunayoitaka!!
Wwe jamaa upo dunia ipi? Wale wajumbe wa kigamboni wamesha panda hadhi Sasa hivi wanaitwa WAJUMBE WA TAIFA.
 
Busara au wame ona macho yote yapo TZ kwenye msiba plus lissu wange shtukiwa
 
Namsifu pia mkuu mpya wa mkoa wa Dar es Salaam kwa busara kubwa aliyoionesha kama mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa. Ingekuwa ni yule bwana masifuri leo ingekuwa ni vilio na kusaga meno. Well done!
Makonda amekosea mengi na kufanya mazuri mengi.
Lakini tuwe wakweli daima na tusiongozwe na hisia.

Makond kama RC (wakati wa enzi zake) alikuwa hawezi kuzuwia amri kwa mfano ya IGP kuhusu kuamrisha askari wazuie au wasizuie maandamano bali anaweza kushauri tu.

Makonda ndiye aliye watuliza askari wasitumie nguvu wala kuzuwia watu waliokuwa wanataka kugusa gari iliyokuwa imebeba mwili wa marehemu mtu mmoja maarufu toka uwanja wa ndege kuelekea sehemu flani. Tusiwe na vichwa vya kusahau kama kuku.
Hivyo hata yeye kuna wakati alitumia busara kama ya leo. Tuache kumrushia tuhuma na lawama Makonda kwa matatizo yetu ya kihisia, kiakili, kiuchumi na kiafya. Matatizo ya Makonda abebeshwe lawama yeye na matatizo ya polisi au watu wengine wabebeshwe wao.

Makonda hakuwa mkuu wa mkoa wa Arusha, Iringa, au Morogoro wakati wa maandamano ya CDM kisha kukaibuka vurugu maeneo hayo na kuleta maafa makubwa sababu ya jeshi la polisi kutumia nguvu.

Sasa hayupo kwenye hayo mamlaka anaendelea na maisha yake nasi tuendelee na maisha yetu. Life goes on bwasheikh.
 
Asubuhi nilitoa mada yenye kichwa "Tunasubiri kuona busara ya jeshi la polisi wakati wa kurejea kwa Lissu"

Niseme wazi kwa mara ya kwanza jeshi la polisi limetumia busara kubwa kutozuia na kuingilia mapokezi ya Tundu Lissu.

Hiki ndicho wengi tulikuwa tuna kitaka. Polisi wakijiweka kando katika shughuli za kisiasa na kijamii huwa hakuna vurugu wala madhara mpaka pale wao wanapofika na mabomu yao, virungu na bunduki kuanza kutumia nguvu kwenye dhughuli zisizo kuwa na vurugu.

Kwakweli kuna haja ya jeshi kuendelea na utamaduni huu. Waacheni watu wafanye shughuli zao za kulia na kucheka bila kuwaingilia kwa kisingizio cha mikusanyiko.

Kwa muda mrefu polisi na CDM wamekuwa kama wake wenza wanao gombea mume kila siku vitisho na ugomvi Polisi wakiwa ndio chanzo. Polisi kwa leo mmeonesha busara kwa mara ya kwanza.

Namsifu pia mkuu mpya wa mkoa wa Dar es Salaam kwa busara kubwa aliyoionesha kama mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa. Ingekuwa ni yule bwana masifuri leo ingekuwa ni vilio na kusaga meno. Well done!
Nawapongeza jeshi letu la Polisi.

Nawaomba waendelee hivyo hadi siku matokeo yatakapotangazwa, wasiingilie jambo lolote lile
 
Busara, au walizidiwa na kushangazwa na umati ule?!
Sio umati, ni aibu kutembeza mitama wakati wa msiba na ingekuwa ni credit ya maana sana kiasiasa upande wa pili. Dunia nzima itatushangaa, hujui tu jiwe ilivyomuuma.
 
Asubuhi nilitoa mada yenye kichwa "Tunasubiri kuona busara ya jeshi la polisi wakati wa kurejea kwa Lissu"

Niseme wazi kwa mara ya kwanza jeshi la polisi limetumia busara kubwa kutozuia na kuingilia mapokezi ya Tundu Lissu.

Hiki ndicho wengi tulikuwa tuna kitaka. Polisi wakijiweka kando katika shughuli za kisiasa na kijamii huwa hakuna vurugu wala madhara mpaka pale wao wanapofika na mabomu yao, virungu na bunduki kuanza kutumia nguvu kwenye dhughuli zisizo kuwa na vurugu.

Kwakweli kuna haja ya jeshi kuendelea na utamaduni huu. Waacheni watu wafanye shughuli zao za kulia na kucheka bila kuwaingilia kwa kisingizio cha mikusanyiko.

Kwa muda mrefu polisi na CDM wamekuwa kama wake wenza wanao gombea mume kila siku vitisho na ugomvi Polisi wakiwa ndio chanzo. Polisi kwa leo mmeonesha busara kwa mara ya kwanza.

Namsifu pia mkuu mpya wa mkoa wa Dar es Salaam kwa busara kubwa aliyoionesha kama mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa. Ingekuwa ni yule bwana masifuri leo ingekuwa ni vilio na kusaga meno. Well done!

Kipindi magu anafungua majengo ya NEC Dodoma alitaka Polisi kutowasumbua wapinzani, nadhani ndiyo maana mapokezi ya Lissu yamekuwa na Amani. Siku zote polisi wamekuwa ndiyo chanzo kikubwa cha vurugu katika mikutano ya siasa kwa nia ya kuwafurahisha wakubwa wao.
 
Sio umati, ni aibu kutembeza mitama wakati wa msiba na ingekuwa ni credit ya maana sana kiasiasa upande wa pili. Dunia nzima itatushangaa, hujui tu jiwe ilivyomuuma.
Hahaha sasa huyo jiwe anaumia nini, msiba wa ccm hauwahusu Chadema.

Walitaka maridhiano akakataa, hivyo kila mtu kivyake.

Yeye yuko msibani wao Chadema wanampokea mgombea wao.
 
Walitegemea atakamatwa ili watengeneze tamthilia ya kuhalalisha maneno

Yaliyotokea leo ni pigo kubwa kwa Mabeberu mawakala wao

Serikali iwaache hawa mawakala kwa miezi hii mitatu wajimwage ikiwezekana wawe wanaandamana kila siku

Isiwaguse wala kuwabughuzi kwa lolote lile mpaka uchaguzi utakapoisha nina uhakika watatoa ushindani lakini hawatashinda

Mambo yaanze mapema baada ya uchaguzi kupita sasa kesi zianze kurindima

Hili ni pigo takatifu kwa Mabeberu na mawakala wao hawajaamini kilichotokea they are speechless, wamepigwa mapigo matakatifu
 
Back
Top Bottom