Hongera sana JOTI

Hongera sana JOTI


Kuoa inabidi ufikirie kabla ya kufanya maamuzi manaake wanawake ndani ya nyumba wanaongea kuanzia asubuhi mpaka jioni, they don't know how to shut up hata kama unataka kuangalia mechi muhimu ya football, ukisema ukae na PC yako kuangalia nini kinaendelea kwenye JF anasema unamuignore, sasa basi ukiamua kunywa bia zako ndio kabiiisa atakwambia we kazi yako kulewa tu. Basi tabu tupu.

Daaahhh Jf raha sanaaaa. Umenichekesha sn mkuu....
 
Mkuu salamander hivi viumbe huwa hawatosheni na hakuna jema kwao,ukisema ukae nyumban..,utasemwa sana na hata kwenye majukwaa utaletwa mwanaume gan unatunzwa,ukisema utoke ukatafute utasemwa mwanaume gani hujali mkeo muda wote kazi tu,ukisema muda wa siku moja moja utulie nae,utasikia sasa upo hapo hata kuosha vyombo hufanyi kazi yako kupiga story nakuangalia tv,ukisema umsaidie kuosha vyombo...unapelekwa tena katika vikao kuwa umekamatwa hupindui yeye muda wote upo online...hawa hawana jema hawa....Ndo maana tumepewa amri juu yao kuwatawala nakuwaongoza hawa maana ni watoto hata kama ana miaka mia,..
 
joti ni mfupi sasa janja ndo iyo ya kumpigisha magoti mdada mana yeye kamzidi urefu!
 
nani niliona nipite kimya kimya. ila ukute ndo ukweni hapo hana jinsi

Yaa! inawezekana, na kama ni ukweni lazima uwe mpole, maana Wazazi wamemlea, wamemsomesha, wewe unaenda kula mzigo tu. Daah! we acha tu. Ama kweli kila Mwanamume ana Deni na Akizaa mtoto wa Kike amelipa.
 
Msanii Lucas Mhuvile, almaarufu kama Joti, anayepiga kazi kwenye kampuni ya Orijino Komedi, amemvisha pete mpenzi wake wa siku nyingi, ikiwa ni ishara na dalili njema kwamba safari ya kuelekea kwenye taasisi muhimu zaidi duniani ya NDOA imewadia..

Akiwa na swahiba wake wa siku nyingi, Mr. Mjuni Sylvatory a.k.a Mpoki, Joti alionekana mwenye furaha muda wote kwa kutimiza tendo hilo huku akiwa amealika watu wachache sana kuhudhuria tukio hilo.

Binafsi, nampongeza sana na kumtakia kila la kheri yeye pamoja na mwenza wake. Big up Joti!!!!

View attachment 223523

Halafu mbona kama Protocols zimekiukwa hapa?. Kwani anaetakiwa kupiga magoti ni nani hasa?. Sie wengine hata hizo pete kwetu hazipo. Ni mkeka na Ubani tu, mchezo kwisha! Mkitoka hapo mnaweza kununuliana mapete hadi kumi, ya madini yoyote hata bati au mbao mtajua wenyewe, ni mapenzi yenu tu na uwezo wenu! Mkichokana aaaahgg! Hakuna kupelekana Frend's Conner, ni halali kutengana kwa talaka. Na Ukimpa talaka mara tatu (vipindi vitatu), basi humuoi tena hadi aolewe na kidume kingine, na sheria ya ndoa yetu, ili ndoa ikamilike lazima ale mikwaju kwanza na kukiri yeye mwenyewe kwamba mzee jogoo anawika vizuri. Sasa kama ikitokea wameachana, basi unaweza kuoa tena na zile talaka za mwanza zimefutika.
 
Back
Top Bottom