Hongera sana Pascal Mayalla, Ndio Mwandishi Pekee Uliyemuuliza Swali Rais Magufuli

Chakaza

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2007
Posts
40,455
Reaction score
73,145
Hakika nimefurahishwa sana na Mwandishi huyu Pascal Mayalla wa kipekee aliyemuuliza swali Rais lenye msingi na hata rais kajibu kwa ubabaishaji. Natafuta clip au mwenye nayo aiweke.



Kwanza kaanza kwa kuitaja JamiiForums kwa kusema ni mwanachama mwandamizi wa JamiiForums.

 
Kamuuliza kuwa kapata wapi mamlaka ya kuzuia safari za watumishi nje wakati kuna mihimili mitatu na yote inajiongoza yenyewe?

Pia kwanini mikusanyiko ya kisiasa inatambulika na katiba lakini yeye kaizuia wakati aliapa kutumikia nchi kwa mujibu wa katiba?

Kama wangekuwepo hata watano tuu wenye mwelekeo wa Pasco hakika angependa hayo masaa mawili yaishe aondoke, lakini kwa vile waliopo wengi ni makanjanja basi kawaambia waulize mpaka wachoke wenyewe.
 
Nimemsikia Pasco Mayalla akiuliza swali kwamba Rais amepata wapi mamlaka ya kuwaambia Wabunge (legislature) na Mahakama (Judiciary) waombe ruhusa kwake watakapo kusafiri?

Hoja ya Pasco ni kwamba kuna separation of powers yaani Executive, Judiciary na Legislature ambazo zinatakiwa zifanye kazi bila kuingiliana. Hilo ni sawa ila Pasco kweli hafahamu kwamba Rais wa Jamhuri ni mkuu wa dola na chini ya dola ndio unapata executive arm, judiciary arm na legisleture?

Hajui kwamba Rais wa Jamhuri ni Head of Government na wakati huohuo ni Head of the State?
 
Ila Kajibiwa Kisiasa!
"Unajua Ni Kwanini Hotuba ya Kusitisha Mikutano na Shughuli za Kisiasa Bungeni?Mpiga Chakula na Mgawaji Ndie Ajuaye Chungu Kilivyo!Soma Katiba Ujue Katika Mihimili Yote Mitatu ni Upi Wenye Nguvu"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…