Naomba Musisahau Sio Pasco wa JF, Ni Pasco Mayalla wa Kiti moto cha Enzi zileeeee! Huyu wa JF Ni stooge wa Lumumba!
Katiba iliyopo inampa mamlaka za kimungu Rais... Anaweza fanya lolote ajiskiavyo na hamna kesi.Wataalam wa katiba waje hapa watueleze kama kifungu cha 35 cha katiba kinampa madaraka makubwa Rais dhidi ya mihimili mingine ya dola.
Hahaaaha! Ataacha kuzuga??? Mchezoo!!!!!!Congrats pascor nimeona swali makini umeuliza ad mwisho ikabid azuge kidogo mayala oooyeeee
Amejibu kuwa uko muhimili ambao uko juu ya mingine bila kutaja ni ibara gani ya katiba inamruhusu kuvunja katiba ya nchi aliyoapa kuilinda na kuitetea
PASCO MAYALLA HOYEEEEEE, SWALI LA PASCO MAYALLA HOYEEEEE, MAGUFULI ????? JIBU LA MAGUFULI ZIIIIIIIIIIIIIIII 😡
kuna mwandishi wa kike toka TBC ameuliza mweshimiwa rais wakati unagombea urais kuna kitu ulikuwa unafikiria utakikuta ikulu.. je umekuta kama ulivyokuwa ukifikiria? daaah nilisikitika sana mwandishi wa tbc kuuliza swali kama mwandishi wa shigongoHuyu jamaa ndo mwandishi pekeee tz mwenye akili timamu, rais kashindwa kujibu swali lake kwa 100% .. pole rais wetu kwa kukimbia swali
Hii mada inamzungumzia Pasco na swali lake video yake imeambatanishwa.Ifikie muda tupeane updates hata kwa summary tu haiwezekan mtu anaanzisha thread as if watu wote hapa jf walikuwa online muda huo kufuatilia kuhusu mahojiano hayo,wengine ni waalimu humu wako kwenye mitihani ya 4m 4 na wengine hawakubahatika kupitia hiyo dialogue hebu ni vema ungetuhabarisha kuwa pasco aliuliza hivi na sammy aliulizia hivi sio kutuandikia eti nani kakufurahisha kati ya w/habari,‘eboooo!!!
Hakika nimefurahishwa sana na Mwandishi huyu Pascal Mayalla wa kipekee aliyemuuliza swali Rais lenye msingi na hata rais kajibu kwa ubabaishaji. Natafuta clip au mwenye nayo aiweke.
Kwanza kaanza kwa kuitaja JamiiForums kwa kusema ni mwanachama mwandamizi wa JamiiForums.
Leo nna rahaaaa!!! Nnasikiliza music hapaa!amesema Pasc (njaa) hoyee!!! Huku akitamani ardhi imfukie,chezea pas.co wewe!Kwenye hii news conference uchwara performance ya DU inastahili F.
Pascal amekaa kinjaanjaa lakini ana mavumbaSijui alilenga nini kusema hivyo.
Kapenyezewa na nani?Pasco alipenyezewa lile swali,hakutafakari kwanza
HahaaahaaaahaaaJambo lingine kalisema katika utangulizi kuonyesha hajikombi wala hana njaa (kama jina lake lilivyotafsiriwa, ingawa majina hayatafsiriwi kwani yeye la kati tukimwita Wanzuki au kangara atafurahi?) Ni pale aliposema waandishi binafsi wapate mialiko ya ziara za nje na wanaweza kujilipia.
Hiyo ni kuonyesha hana njaa na hategemei fadhila.
Hata msosi wao wakimnyima waweza kuta msukuma huyu kwenye mkoba wake kajibebea viazi vyake vya kuchemsha yaani manumbu (joke)