Hongera sana Pascal Mayalla, Ndio Mwandishi Pekee Uliyemuuliza Swali Rais Magufuli

Hongera sana Pascal Mayalla, Ndio Mwandishi Pekee Uliyemuuliza Swali Rais Magufuli

Mkuu basi tuseme pacha wake mama moja baba moja. Nadhani sitakosea nikisema uwepo wa Pasco hapa jamvini na ushiriki wake mkubwa umemsaidia kumpanua mawazo ingawaje kuna wakati anakuwa kama wale Buku 7.


Naomba Musisahau Sio Pasco wa JF, Ni Pasco Mayalla wa Kiti moto cha Enzi zileeeee! Huyu wa JF Ni stooge wa Lumumba!
 
Wataalam wa katiba waje hapa watueleze kama kifungu cha 35 cha katiba kinampa madaraka makubwa Rais dhidi ya mihimili mingine ya dola.
Katiba iliyopo inampa mamlaka za kimungu Rais... Anaweza fanya lolote ajiskiavyo na hamna kesi.
 
Ni jibu la kidikteta kwa sababu hakuna kipengele chochote kile ndani ya katiba ambacho kinashabihiana na jibu lake.

Amejibu kuwa uko muhimili ambao uko juu ya mingine bila kutaja ni ibara gani ya katiba inamruhusu kuvunja katiba ya nchi aliyoapa kuilinda na kuitetea
 
Waandishi njaa tuu!! Kaz kupig makofi wakisifiwa na kuambiwa anawatambua,, wanadhan watateuliwa kama wenzao
 
Huyu jamaa ndo mwandishi pekeee tz mwenye akili timamu, rais kashindwa kujibu swali lake kwa 100% .. pole rais wetu kwa kukimbia swali
kuna mwandishi wa kike toka TBC ameuliza mweshimiwa rais wakati unagombea urais kuna kitu ulikuwa unafikiria utakikuta ikulu.. je umekuta kama ulivyokuwa ukifikiria? daaah nilisikitika sana mwandishi wa tbc kuuliza swali kama mwandishi wa shigongo
 
Hakika nami nampokeza Tido Muhando, mtangazaji was BBC na Hongera nyingi kwa Pasco Mayala
 
Mie namfananisha Mr.president na dereva mwenye hamu na shauku kubwa ya kuwafikisha abiria wake salama salimini tena kwa haraka lkn dereva huyu hazingatii kabisa sheria ya barabara. Sasa heri atufikishe salama tutampongeza sana na bila shaka tutapanda gari yake safari nyingine lakini akitubwaga njiani ajue lawama zitamwangukia yeye binafsi na gari lake na pengine inaweza kuwa ndio mwisho Wa kampuni yenyewe yaani KUFILISIKA, Mungu aepushie mbali
 
Ifikie muda tupeane updates hata kwa summary tu haiwezekan mtu anaanzisha thread as if watu wote hapa jf walikuwa online muda huo kufuatilia kuhusu mahojiano hayo,wengine ni waalimu humu wako kwenye mitihani ya 4m 4 na wengine hawakubahatika kupitia hiyo dialogue hebu ni vema ungetuhabarisha kuwa pasco aliuliza hivi na sammy aliulizia hivi sio kutuandikia eti nani kakufurahisha kati ya w/habari,‘eboooo!!!
Hii mada inamzungumzia Pasco na swali lake video yake imeambatanishwa.
Wewe kama mjanja tafuta kwingineko kupata hicho kingine unachotafuta.
Nani akutafunie kila kitu? Ebbo!
 
Pascal kuna kitu cha maana alichouliza zaidi ya kuonesha huwa hasomi katika. Raisi kamjibu asome ibara ya 35 na hivyo amemprove kuwa huwa anakurupuka kama msigwa na sugu. Raisi yuko vizuri na anaisoma katika kweli kweli. Tatizo nyie mnaongozwa na mizuka na mihemko baada ya milija yenu kuzibwa kupitia bilcabas ya mbowe
Hakika nimefurahishwa sana na Mwandishi huyu Pascal Mayalla wa kipekee aliyemuuliza swali Rais lenye msingi na hata rais kajibu kwa ubabaishaji. Natafuta clip au mwenye nayo aiweke.

Kwanza kaanza kwa kuitaja JamiiForums kwa kusema ni mwanachama mwandamizi wa JamiiForums.
 
Leo mimi nimefurahi kuwa MWANAJF kipekee kauliza swali ambalo ni too constructive, tactical, technical na professionally submitted. Imejidhihirisha kuwa kweli JF ni Home of Great Thinkers.
Kingine nilichofurahi ni ule ushauri wetu ambao mimi binafsi niliwahi kuusema humu JF na leo nafurahi Mh JPM kausema. Kwamba hii nchi ilifika sehem mbaya, lakini kiukweli, hayo mambo ya ovyo yawe phased out/away na tuanze upya. Kufukua makaburi kutatufanya tuchelewe kuyafikia malengo na kwa kuwa miaka 5 ni michache, unaondoa mambo ya ovyo, unaanza upya.
 
Kwenye hii news conference uchwara performance ya DU inastahili F.
Leo nna rahaaaa!!! Nnasikiliza music hapaa!amesema Pasc (njaa) hoyee!!! Huku akitamani ardhi imfukie,chezea pas.co wewe!
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Jambo lingine kalisema katika utangulizi kuonyesha hajikombi wala hana njaa (kama jina lake lilivyotafsiriwa, ingawa majina hayatafsiriwi kwani yeye la kati tukimwita Wanzuki au kangara atafurahi?) Ni pale aliposema waandishi binafsi wapate mialiko ya ziara za nje na wanaweza kujilipia.
Hiyo ni kuonyesha hana njaa na hategemei fadhila.
Hata msosi wao wakimnyima waweza kuta msukuma huyu kwenye mkoba wake kajibebea viazi vyake vya kuchemsha yaani manumbu (joke)
Hahaaahaaaahaaa
 
Back
Top Bottom