Pasco kwanza nikupongeze kwa kujenga swali lako vizuri sana
Umewakilisha hoja zetu za kila siku hata kama hawataki au hawakubali mtandao JF
Majibu ya Rais kuhusu swali lako yanazua utata mwingine mkubwa.
Kuna nyakati serikali inasema mihimili mitatu haiingiliani kiutendaji.
Rais anasema mhimili wa serikali ni mkubwa Zaidi
Hili ni tatizo kubwa sana, hakuna mhimili mkubwa katika hiyo mitatu kwa wenzetu walioanzisha system hiyo. Rais anaposema mhimili wake ni mkubwa, tayari ameshakiuka 'separation of power'
Hakujibu swali na alipojaribu aliharibu Zaidi
Pili, hili linaeleza kuwa mhakama na Bunge si mihimili huru. Tumezungumza kila siku kuwa Mahakama inatakiwa iwe na bajeti yake inayoidhinisha katika bajeti ya mwaka. Bunge liwe na bajaeti yake
Hayo ndiyo yataweka vyombo hivyo huru
Ile hoja yetu kuwa mahakama si huru na inatumika, inazidi kupata nguvu kwa hoja za Rais
Pasco Rais amejibu swali lako la siku nyingi kwanini CUF hawakwenda mahakamani
Kwanini UKAWA hawakwenda mahakamani.
Inapofikia masuala ya siasa mahakama zetu hazipo huru na Rais kasema mhimili wake ni mkubwa na yeye ndiye mwenye nyenzo za kuwezesha mihimili mingine. Unategemea nini hapo?
Tatu, swali lako la wapi katika katiba Rais amepata nguvu za kupiga marufuku mikutano.
Rais hakujibu hilo swali kwasababu kikatiba hakuna mahali amepewa nguvu hizo
Hili limehirimisha propaganda za baadhi ya watu kama
MsemajiUkweli ukweli waliojitahidi kutafuta vifungu hovyo.
Wengine wakiandika Makala za kusifu utendaji kwa kupiga marufuku.
MsemajiUkweli na wengine wenye njaa nadhani sasa mnaona mnavyodhalilika
Rais hana jibu kwanini mikutano imezuiliwa, na hii maana yake sisi tuliosema amevunja katiba tupo sahihi kabisa. Hakujibu swali hana jibu, ni ushahidi amevunja katiba
Rais kuvunja katiba ni tendo baya. Nyerere alisema 'Rais asiyeheshimu katiba hatufai'