Hongera sana Pascal Mayalla, Ndio Mwandishi Pekee Uliyemuuliza Swali Rais Magufuli

Hongera sana Pascal Mayalla, Ndio Mwandishi Pekee Uliyemuuliza Swali Rais Magufuli

Yani Pasco ndio kapiga za chembe leo.. Sijui hata kile chakula walichoandaliwa kama kapewa
 
kuna mwandishi wa kike toka TBC ameuliza mweshimiwa rais wakati unagombea urais kuna kitu ulikuwa unafikiria utakikuta ikulu.. je umekuta kama ulivyokuwa ukifikiria? daaah nilisikitika sana mwandishi wa tbc kuuliza swali kama mwandishi wa shigongo
Ndo maana tbc ni ya mwisho kutazamwa na watu
 
Swali zuri nampongeza Pasco pia nampongeza Rais kwa kumpatia jibu sahihi.
 
Pasco kwanza nikupongeze kwa kujenga swali lako vizuri sana
Umewakilisha hoja zetu za kila siku hata kama hawataki au hawakubali mtandao JF

Majibu ya Rais kuhusu swali lako yanazua utata mwingine mkubwa.
Kuna nyakati serikali inasema mihimili mitatu haiingiliani kiutendaji.

Rais anasema mhimili wa serikali ni mkubwa Zaidi

Hili ni tatizo kubwa sana, hakuna mhimili mkubwa katika hiyo mitatu kwa wenzetu walioanzisha system hiyo. Rais anaposema mhimili wake ni mkubwa, tayari ameshakiuka 'separation of power'
Hakujibu swali na alipojaribu aliharibu Zaidi

Pili, hili linaeleza kuwa mhakama na Bunge si mihimili huru. Tumezungumza kila siku kuwa Mahakama inatakiwa iwe na bajeti yake inayoidhinisha katika bajeti ya mwaka. Bunge liwe na bajaeti yake
Hayo ndiyo yataweka vyombo hivyo huru

Ile hoja yetu kuwa mahakama si huru na inatumika, inazidi kupata nguvu kwa hoja za Rais
Pasco Rais amejibu swali lako la siku nyingi kwanini CUF hawakwenda mahakamani
Kwanini UKAWA hawakwenda mahakamani.

Inapofikia masuala ya siasa mahakama zetu hazipo huru na Rais kasema mhimili wake ni mkubwa na yeye ndiye mwenye nyenzo za kuwezesha mihimili mingine. Unategemea nini hapo?

Tatu, swali lako la wapi katika katiba Rais amepata nguvu za kupiga marufuku mikutano.
Rais hakujibu hilo swali kwasababu kikatiba hakuna mahali amepewa nguvu hizo

Hili limehirimisha propaganda za baadhi ya watu kama MsemajiUkweli ukweli waliojitahidi kutafuta vifungu hovyo.

Wengine wakiandika Makala za kusifu utendaji kwa kupiga marufuku.

MsemajiUkweli na wengine wenye njaa nadhani sasa mnaona mnavyodhalilika

Rais hana jibu kwanini mikutano imezuiliwa, na hii maana yake sisi tuliosema amevunja katiba tupo sahihi kabisa. Hakujibu swali hana jibu, ni ushahidi amevunja katiba

Rais kuvunja katiba ni tendo baya. Nyerere alisema 'Rais asiyeheshimu katiba hatufai'
 
Pascal kuna kitu cha maana alichouliza zaidi ya kuonesha huwa hasomi katika. Raisi kamjibu asome ibara ya 35 na hivyo amemprove kuwa huwa anakurupuka kama msigwa na sugu. Raisi yuko vizuri na anaisoma katika kweli kweli. Tatizo nyie mnaongozwa na mizuka na mihemko baada ya milija yenu kuzibwa kupitia bilcabas ya mbowe
Kuna wakati nilikuwa nafuga mbwa wanne kwa ajili ya ulinzi, lakini nikaja gundua kuna mmoja ana tabia ya kubweka hovyo bila sababu ya msingi. Nikamuona ni mwehu tuu.
Lakini hata watu wapo wa aina ile ya mbwa wangu, anaweza kuropoka lolote pasipo sababu ya msingi
 
huyu ndo pekee alijua nini kimempeleka japo swali halijajibiwa ipasavyo na swali la pili ndo kabisaaa.

MUNGU AMBARIKI KWENYE KAZI YAKE
hivi Ruge nae alikuwemo? nimeskia anasifiwa tu na imoo yake.... nilitamani aulize swali la kiboyaboya
 
Waandishi wameshindwa kumuliza mtukufu alipata wapi mamlaka ya kupanga pesa zilizokuwa zimeshapangwa na binge,kama zile za skk ya muungano na ski ya uhuru
 
Hakika nimefurahishwa sana na Mwandishi huyu Pascal Mayalla wa kipekee aliyemuuliza swali Rais lenye msingi na hata rais kajibu kwa ubabaishaji. Natafuta clip au mwenye nayo aiweke.

Kwanza kaanza kwa kuitaji JamiiForums kwa kusema ni mwanachama mwandamizi wa JamiiForums.

Na pia Raid akumbuke katiba ndio imetoa mamlaka kwake na miimili hiyo pia,jukumu la yeye kuwa ndio ana financial miimili hiyo ni LA kikatiba lkn sio kuingilia shughuli zao,wana haki kikatiba na katiba IPO juu ya Rais
 
Nataka kutoa pongezi zangu za dhati kwa mwanajamiiforum mwenzetu kwa swali pekee lililokwenda shule, kwa Rais japo swali limejibiwa kisiasa zaidi,
Wana jf wenzangu hebu tumpongeze member mwenzetu Pasco kwa kutuwakilisha vyema,
Ongera yake ila najua hii ndio itakuwa mara yake ya kwanza na ya mwisho kwenda kwenye kikao cha raisi naa waandishi wa habari alafu harusiwe kuuliza swali.
 
3315528d214ba1b4c43a9d9845436c05.jpg
huyu mwana habari Pascal Mayalla a.k.a Mzee wa "Kitimoto" yeye ndio mwasisi wa kipindi cha KITIMOTO(CHA KUWAHOJI WANASIASA) na mwendeshaji wa kipindi hicho DTV 1995, aliwahi kumhoji suali gumu(msukuma mwenziwe) mwenyekiti wa UDP John Cheyo, kwaivo ujasiri wa Mr Mayala KUWAHOJI WANASIASA bila woga ni hulka na kipaji aliopewa na mungu.
Kwa hivyo nawasihi wanahabari wote waige mbinu zake, ili tz I onekana imo kwenye tasnia hii.
 
Bora ya Pascal Mayalla ambaye pamoja na kujipa promo na kusifia sifia kaweza kuwa na ujasiri wa kuuliza swali la msingi sana na ambalo Magufuli kashindwa kabisa kulijibu kwa ufasaha.

Nimesikitika sana Manyerere Jackton kuanza kulia lia njaa badala ya kuuliza swali la Msingi. Manyerere anaomba apewe tender za Matangazo ya Serikali kwenye gazeti lake, anataka aje ikulu anywe Whisky na mwisho anataka apewe Tuzo.
Ni jambo la aibu kubwa sana kwa Mhariri kulia njaa mbele ya mtawala.
 
Safi sana Mayala, hata kama hajajibu vizuri lakini ujumbe umefika na umewakilisha mawazo ya walio wengi
 
TETESI: SAMMY AWANI NA PASCAL MAYALLA MARUFUKU IKULU.

Pascal kwanza nikupongeze kwa kujenga swali lako vizuri sana
Majibu ya Rais kuhusu swali lako yanazua utata mwingine mkubwa. Kuna nyakati serikali inasema mihimili mitatu haiingiliani kiutendaji. Rais anasema mhimili wa serikali ni mkubwa Zaidi
Hili ni tatizo kubwa sana, hakuna mhimili mkubwa katika hiyo mitatu kwa wenzetu walioanzisha system hiyo. Rais anaposema mhimili wake ni mkubwa, tayari ameshakiuka 'separation of power'
Hakujibu swali na alipojaribu aliharibu Zaidi.


Sammy na wewe nikupongeze kwa kujenga swali lako vizuri sana..
Sammy awani " watu wengi wanahisi anakandamiza demokrasia ya nchi"
Majibu ya Rais kuhusu swali lako yanazua utata mwingine mkubwa.

Kwa maswali hayo nazani kuitwa tena ikulu msahau..

Maswali magumu, majibu mepesi.


Hapa kazi tu

Huu sasa ndio uchochezi. Acha tu huo muswada wa habari upitishwe ili kukomesha watu wa aina yako. Maana kichwa chako cha habari na maelezo yako ndani ni tofauti kabisa. Mtanyooka tu! It is just a matter of time!
 
Huo ni ujinga
Kwalipi kuoelekea kuzuiliwa
Au mnawapa ujiko usio na maana!!!
 
Huo ni ujinga
Kwalipi kuoelekea kuzuiliwa
Au mnawapa ujiko usio na maana!!!

. Achana naye! Yaani hawa ndio wanasababisha mpaka sheria zinatungwa kali kupita maelezo. Mtu aandika utumbo wa kushtusha kiasi hiki. Hao anaowataja sasa hivi wako Ikulu wanakula bata.
 
Back
Top Bottom