Hakika nimefurahishwa sana na Mwandishi huyu
Pascal Mayalla wa kipekee aliyemuuliza swali Rais lenye msingi na hata rais kajibu kwa ubabaishaji. Natafuta clip au mwenye nayo aiweke.
Kwanza kaanza kwa kuitaji
JamiiForums kwa kusema ni mwanachama mwandamizi wa
JamiiForums.
Mayala alianza na mbwembwe za enzi ya "kiti-moto-akiwa na masai studio" kipindi kilikuwa kizuri DTV sijui ikawaje akakipeleka ITV na kukiulia pale, cha ajabu akauliza vitu km mwanahabari aliyebobea kwamba hajui Rais anachofanya.
Rais kamjibu vizuri tu hasa alipomrekebisha kuwa alitegemea angemuuliza kwa nini hotuba ya ubanaji matumizi aliitoa humo ndiyo Rais akatambaa hivi "katika eneo pia llinalopoteza pesa za masikini ni Bunge na kuwaomba wajipange maana yake ni nini, huko nyuma Ofisi ya Bunge ilishakuwa na desturi kuandaa hata safari za nje ambazo hazikuwa na maslahi ili mradi tu kuna watu watafaidika kwa bajeti hiyo.. ufafanuzi Mayala akaambiwa kwa kufanya hivyo hakuliingilia Bunge ni kweli Mihimili ni mi-3 ila Mihimili mmoja ndiyo unaotafuta hizo pesa alizoomba Bunge wajipange hapa ali-deal na Ofisi siyo Mamlaka ya Bunge kwa maana ya Maamuzi ya Bunge WABUNGE AT ALL nini hoja hapo wanaopokea pesa kutoka "Mhimili Serikali" ni "Ofisi ya Bunge" ambao hasa ni waajiriwa wa "Mhimili Serikali" ndiyo maana Bunge walijiongeza karudisha chenji ya Bunge la 10 na ile pesa ya "kujichana" amabayo Ofisi iliomba "Mhimili Serikali" yy akaikata bajeti ya ile sherehe kwa maana ya kuwa ni mtafutaji wa pesa hizo.
Na kikubwa alipomjibu juu ya "Mhimili Mahakama" kuwa wao walikuwa na shida kuwa kesi haziishi hawana pesa na kumweka sawa Mayala kuwa kwa "Mhimili Serikali" kuupa pesa fasta "Mhimili Mahakama" haikuonekana kuwa anaingilia huo Mhimili? Jibu liko clear yeye ha-deal na maamuzi ya "Mhimili Mahakama" kwa maana ya Maamuzi.ya kesi.
Rais hakuishia hapo bali alijitahidi kuufafanua kifalsafa kuwa "Mhimili mmoja umejichimbia chini sana"
Juu ya mikutano ya Vyama aliweka wazi kuwa Katiba isisomwe kwa kuchagua kifungu bali isomwe yote kwa tuliokuwa timamu tuliona ni jinsi gani Mawala alivyokuwa anaingizwa darasani licha ya kujifafanua kuwa ni MWANASHERIA pia,na kuongeza yeye asipokuwa na pesa kuwapa '' Wabunge - bila kubagua "ndiyo maneno yatakuwa mengi mno" but wao (Bunge na Mahakama) mishahara wanalipwa pesa yatoka wapi?" "MHIMILI SERIKALI"
Kiukweli Rais kaonyesha UMAHIRI MKUBWA kuulizwa maswali na Wahariri japo Mayala siyo mhariri.
Ila humu naona anasifiwa MAYALA vipi wale wa kutoka gazeti lile ambalo lilitolewa vyombo nje kwa KUKWEPA KULIPIA PANGO?
Wahariri wakweli leo hawakutaka kuumbuka kwa kuuliza uliza vitu ambavyo RAIS anavitolea ufafanuzi wa kina kila linapotokea jambo tata.
Shida ilikuwa mtandaoni ambako watu WAMELISHWA upupu wa kuaminishwa kuwa kila jambo la MTANDAONI NI SAHIHI.
MAYALA PASCHAL, Mzee wa Shariff Shamba kitambo a.k a. Mzee wa Kiti-Moto LEO KAJIUMBUA..eti "freelance broadcaster(mtangazaji wa kujitegemea).
SIKU NYINGINE MKISIKIA wanatakiwa WAHARIRI(EDITORS),muwe mnaelewa.
VIVA MAGUFULI, LONG LIVE MAGUFULI, ADUMU MAGUFULI.
This for Adults(bakulutu) kids(bamoke) don't touch this. [emoji106] [emoji106] [emoji106]