Hongera sana Pascal Mayalla, Ndio Mwandishi Pekee Uliyemuuliza Swali Rais Magufuli

Hongera sana Pascal Mayalla, Ndio Mwandishi Pekee Uliyemuuliza Swali Rais Magufuli

hivi hawa waandishi wa bbc huwa wamesomea wapi tofauti na hawa wa kwetu?
Jitu limepewa nafasi tandika swali la maana lenyewe linaanza kusifu na bla blaa nyiiingi
Hongera sammy awami hakika unastahili kuwa shirika kubwa kama bbc
 
Pamoja na pongezi kwa Pascal Mayala niseme maswali yake hayakujibiwa kwa kiwango cha kukidhi kiu ya muulizaji na hata sisi wasikilizaji! Rais amejibu maswali magumu kwa njia isiyokidhi viwango na matarajio yetu!
 
Akili za nyumbu hizo. Achana naye! Yaani hawa ndio wanasababisha mpaka sheria zinatungwa kali kupita maelezo. Mtu aandika utumbo wa kushtusha kiasi hiki. Hao anaowataja sasa hivi wako Ikulu wanakula bata.
hivi hawa waandishi wa bbc huwa wamesomea wapi tofauti na hawa wa kwetu?
Jitu limepewa nafasi tandika swali la maana lenyewe linaanza kusifu na bla blaa nyiiingi
Hongera sammy awami hakika unastahili kuwa shirika kubwa kama bbc
 
Aisee huyu nguli amenifurahisha sana leo.. Na kijana Sammy wa BBC pia.. Nafkiri Jf iwe inatoa heshima kwa members kama hawa hata kwa kuwapandisha madaraja tu.. Jf impe tanzanite member huyu nguli Mayalla.
 
Acha kutunga vitu visivyo na kichwa wala miguu, inakusaidia nini?
 
Huu sasa ndio uchochezi. Acha tu huo muswada wa habari upitishwe ili kukomesha watu wa aina yako. Maana kichwa chako cha habari na maelezo yako ndani ni tofauti kabisa. Mtanyooka tu! It is just a matter of time!

Kudadadeki, nyie watu basi tu, kwabile ni jinai kuwaia.
 
Katiba iliyopo inampa mamlaka za kimungu Rais... Anaweza fanya lolote ajiskiavyo na hamna kesi.

Yes. Lakini kama ambavyo Tundu Lisu amekuwa akiuliza kila siku, bado tunataka kufahamu kifungu gani cha Katiba kinampa mamlaka hayo. Tunajua Katiba ni mbovu, lakini tuambiwe ni wapi mamlaka hayo yanapatikana kwenye katiba.
 
Kapenyezewa na nani?
Kama ulielewa jibu alilopewa kuhusu maana ya jina lake...i.e possibly amepewa kitu kido....na kupenyezewa swali ha ha ha haa....mwishoni Mzee kasema...msitumike vibaya
 
TETESI: SAMMY AWANI NA PASCAL MAYALLA MARUFUKU IKULU.

Pascal kwanza nikupongeze kwa kujenga swali lako vizuri sana
Majibu ya Rais kuhusu swali lako yanazua utata mwingine mkubwa. Kuna nyakati serikali inasema mihimili mitatu haiingiliani kiutendaji. Rais anasema mhimili wa serikali ni mkubwa Zaidi
Hili ni tatizo kubwa sana, hakuna mhimili mkubwa katika hiyo mitatu kwa wenzetu walioanzisha system hiyo. Rais anaposema mhimili wake ni mkubwa, tayari ameshakiuka 'separation of power'
Hakujibu swali na alipojaribu aliharibu Zaidi.


Sammy na wewe nikupongeze kwa kujenga swali lako vizuri sana..
Sammy awani " watu wengi wanahisi anakandamiza demokrasia ya nchi"
Majibu ya Rais kuhusu swali lako yanazua utata mwingine mkubwa.

Kwa maswali hayo nazani kuitwa tena ikulu msahau..

Maswali magumu, majibu mepesi.


Hapa kazi tu
Acha upuuzi huo mbumbu wa sheria ya katiba. 1.There is no absolute separation of power. 2. Rais wa TZ ana powers tatu: i.Head of state, ii.Head of the Government, iii. Head of th Armed forces. Huwezi ukamlinganisha Rais na spika au jaji mkuu. Raisi kikatiba ana mamlaka makubwa zaidi. Ktk mfumo wa Tz kikatiba mhimili wa serikali una mamlaka makubwa zaidi kuliko mihimili mingine. Kikatiba,Raisi ni sehemu ya Bunge. Kkatiba raisi huteua majaji wote. Unapoongelea separation of powers, you must also consider limitations of th same, depending on what is in our constitution which os binding.
 
Mkulu alinichekesha sana aliposema ' umesikia kwenye kampeni zangu nimetaja neno katiba? Kwenye kampeni zangu sijataja katiba''
Utegemee mtu atakujibu kuhusu katiba?
Baadhi ya waandishi wa habari ni vibaraka
 
3315528d214ba1b4c43a9d9845436c05.jpg
huyu mwana habari Pascal Mayala a.k.a Mzee wa "Kitimoto" yeye ndio mwasisi wa kipindi cha KITIMOTO(CHA KUWAHOJI WANASIASA) na mwendeshaji wa kipindi hicho TVT 1995, aliwahi kuhojiwa suali gumu(msukuma mwenziwe) mwenyekiti wa UDP John Cheyo, kwaivo ujasiri wa Mr Mayala KUWAHOJI WANASIASA bila woga ni hulka na kipaji aliopewa na mungu.
Kwa hivyo nawasihi wanahabari wote wuige mbinu zake, ili tz I onekana imo kwenye tasnia hii.
Naona umemsifia sana Pascal Mayalla kuliko uhalisia wenyewe.
Kuweka kumbukumbu sawa hapa JF kuhusu Pascal Mayalla.

1/Alikuwa Mtangaziji wa DTV kipindi hicho Kipindi cha Kitimoto kikiwepo.
Kipindi hicho TVT ilikuwa haijaanzishwa. TVT ilianza kwa majaribio kuwa hewani 1999 wakati wa kifo cha Nyerere.

2/Ni kweli Pascal Mayalla ni mwandishi mzoefu sana lakini pia ni mwandishi mwenye njaa pia. Njaa huwa haiangalii uzoefu. Ukimpa chochote kizuri, Pascal anaweza kukupamba mpaka basi.

3/Mbali na taaluma ya mambo ya habari, Pascal Mayalla ni msomi wa sheria. Ni mjuvi sana wa mambo ya katoliki(Huenda alikuwa na mipango ya Upadri) na pia inazaniwa ni mtu wa usalama kwa siri.
 
Si sahihi kusema tu mhimili wa "Executive" una power zaidi ya mihimili mingine. Tuambie power ya mhimili huo dhidi ya mihimili mingine imeelezwa wapi katika Katiba ya sasa. Tuacheni ubabaishaji hasa tunapojadili masuala ya msingi. Kwa nini tunapiga bla bla, kwa swali ambalo linahusu Katiba ya nchi ambayo imendikwa? Taja kifungu ili wataalam watusaidie kuchambua.
 
Hakika nimefurahishwa sana na Mwandishi huyu Pascal Mayalla wa kipekee aliyemuuliza swali Rais lenye msingi na hata rais kajibu kwa ubabaishaji. Natafuta clip au mwenye nayo aiweke.

Kwanza kaanza kwa kuitaji JamiiForums kwa kusema ni mwanachama mwandamizi wa JamiiForums.

Mayala alianza na mbwembwe za enzi ya "kiti-moto-akiwa na masai studio" kipindi kilikuwa kizuri DTV sijui ikawaje akakipeleka ITV na kukiulia pale, cha ajabu akauliza vitu km mwanahabari aliyebobea kwamba hajui Rais anachofanya.

Rais kamjibu vizuri tu hasa alipomrekebisha kuwa alitegemea angemuuliza kwa nini hotuba ya ubanaji matumizi aliitoa humo ndiyo Rais akatambaa hivi "katika eneo pia llinalopoteza pesa za masikini ni Bunge na kuwaomba wajipange maana yake ni nini, huko nyuma Ofisi ya Bunge ilishakuwa na desturi kuandaa hata safari za nje ambazo hazikuwa na maslahi ili mradi tu kuna watu watafaidika kwa bajeti hiyo.. ufafanuzi Mayala akaambiwa kwa kufanya hivyo hakuliingilia Bunge ni kweli Mihimili ni mi-3 ila Mihimili mmoja ndiyo unaotafuta hizo pesa alizoomba Bunge wajipange hapa ali-deal na Ofisi siyo Mamlaka ya Bunge kwa maana ya Maamuzi ya Bunge WABUNGE AT ALL nini hoja hapo wanaopokea pesa kutoka "Mhimili Serikali" ni "Ofisi ya Bunge" ambao hasa ni waajiriwa wa "Mhimili Serikali" ndiyo maana Bunge walijiongeza karudisha chenji ya Bunge la 10 na ile pesa ya "kujichana" amabayo Ofisi iliomba "Mhimili Serikali" yy akaikata bajeti ya ile sherehe kwa maana ya kuwa ni mtafutaji wa pesa hizo.

Na kikubwa alipomjibu juu ya "Mhimili Mahakama" kuwa wao walikuwa na shida kuwa kesi haziishi hawana pesa na kumweka sawa Mayala kuwa kwa "Mhimili Serikali" kuupa pesa fasta "Mhimili Mahakama" haikuonekana kuwa anaingilia huo Mhimili? Jibu liko clear yeye ha-deal na maamuzi ya "Mhimili Mahakama" kwa maana ya Maamuzi.ya kesi.

Rais hakuishia hapo bali alijitahidi kuufafanua kifalsafa kuwa "Mhimili mmoja umejichimbia chini sana"

Juu ya mikutano ya Vyama aliweka wazi kuwa Katiba isisomwe kwa kuchagua kifungu bali isomwe yote kwa tuliokuwa timamu tuliona ni jinsi gani Mawala alivyokuwa anaingizwa darasani licha ya kujifafanua kuwa ni MWANASHERIA pia,na kuongeza yeye asipokuwa na pesa kuwapa '' Wabunge - bila kubagua "ndiyo maneno yatakuwa mengi mno" but wao (Bunge na Mahakama) mishahara wanalipwa pesa yatoka wapi?" "MHIMILI SERIKALI"

Kiukweli Rais kaonyesha UMAHIRI MKUBWA kuulizwa maswali na Wahariri japo Mayala siyo mhariri.

Ila humu naona anasifiwa MAYALA vipi wale wa kutoka gazeti lile ambalo lilitolewa vyombo nje kwa KUKWEPA KULIPIA PANGO?

Wahariri wakweli leo hawakutaka kuumbuka kwa kuuliza uliza vitu ambavyo RAIS anavitolea ufafanuzi wa kina kila linapotokea jambo tata.
Shida ilikuwa mtandaoni ambako watu WAMELISHWA upupu wa kuaminishwa kuwa kila jambo la MTANDAONI NI SAHIHI.

MAYALA PASCHAL, Mzee wa Shariff Shamba kitambo a.k a. Mzee wa Kiti-Moto LEO KAJIUMBUA..eti "freelance broadcaster(mtangazaji wa kujitegemea).

SIKU NYINGINE MKISIKIA wanatakiwa WAHARIRI(EDITORS),muwe mnaelewa.

VIVA MAGUFULI, LONG LIVE MAGUFULI, ADUMU MAGUFULI.

This for Adults(bakulutu) kids(bamoke) don't touch this. [emoji106] [emoji106] [emoji106]
 
Kiboko yetu kwa lipi jipya zaidi ya kukwepa maswali ya msingi. Amejaa ngonjera na Mipasho, kaonesha uwezo wake kuwa Mdogo saana katka kujibu hoja.
Umesema ukweli!!

Hivi kweli kwa majibu hayo anaweza kumudu vyombo vya habari vya kimataifa? Naimagine Magufuli against Christine Amanpour ... hata kama atajibu kwa Kiswahili bado kijasho chembamba kitamtoka!!

Kwa ukweli maswali hayajajibiwa sawsawa zaidi ya mipasho, kejeri na vichekesho!!

Anyway, anatamba uwanja wa nyumbani ..... ajaribu ugenini tuone!! Hivi Kenya, waandishi walipewa muda kumuuliza maswali!!?
 
Back
Top Bottom