Hongera sana Pascal Mayalla, Ndio Mwandishi Pekee Uliyemuuliza Swali Rais Magufuli

Hongera sana Pascal Mayalla, Ndio Mwandishi Pekee Uliyemuuliza Swali Rais Magufuli

Mimi nampongeza tu kwakuitaja jf kwa mh RAIS basi.
 
Hujui kwamba Bunge linaweza kutunga sheria na Rais akakataa kuisaini? Hujui kwamba kwa mujibu wa Katiba Rais anaweza kutoa msamaha wa hukumu yoyote iliyotolewa na mahakama?
na unajua kuwa bunge linaweza kumimpeach rais?
 
Hujui kwamba Bunge linaweza kutunga sheria na Rais akakataa kuisaini? Hujui kwamba kwa mujibu wa Katiba Rais anaweza kutoa msamaha wa hukumu yoyote iliyotolewa na mahakama?
Unajua akikataa nini kinafuata?
 
Katika sehemu ya pili ya Mayalla, ameuliza kuhusu Rais anakopata mamlaka yake ya kuzuia vyama vya siasa kufanya mikutano na mandamano. Nyie wenzangu mmesikia majibu hapo????
Hana ubavu wa kujibu hapo
Badilisha haraka hilo neno " AMEKUKUNA SANA.." alafu umerudia rudia neno "huko nyuma" mara 2 hv ktk thread yako..!!

Do fast.. kama ww ni -ke basi sawa
 
Kweli kauliza maswali ya msingi sana.Lile la kuzuia mikutano ya siasa wala hajathubutu kuligusia.

hana ujanja wa kujibu hilo swali hata akae library miaka 1OO na vitabu vya makatiba
 
haa haa rais anasema muhimili wake uko juu zaidi kwa vile wenyewe ndo unagawa pesa mweh. je ni mhimili gani unapanga matumizi ya pesa za serikali?
 
JamiiForums~The Home of Great Thinkers
 
Kwa haraka haraka na hisi kati ya zile pande mbili kuna upande mmoja haukujiandaa vema kwa tukio kama lile.
 
Mimi naona mkuu alifanya makusudi kabisa kutojibu swali kuhusu haki ya mikusanyiko kama inavyotolewa na katiba, na yeye amepata wapi mamlaka ya kuzuia mikutani ya siasa. Kwa bahati mbaya Tido na Ryoba wakalipotezea kwa makusudi ili mkuu asiadhirike.
 
haa haa rais anasema muhimili wake uko juu zaidi kwa vile wenyewe ndo unagawa pesa mweh. je ni mhimili gani unapanga matumizi ya pesa za serikali?

Unaweza panga lkn huna.. Mh. Rais mbona kajibu vizuri sana sanaaaa... labda kama hamjui Rais ndio kila kitu.. hata pesa ina Picha ya Rais..hadi hapo hujui tu hela ni ya nani..? shauri yenu..!! watu wagumu sana nyie kuelewa..!!
 
Pasco umeenda kutushtaki kwa magu jamiiforum mwenyewe hata haifahamu
 
Swali la Pascal halikuwa na mashiko ndio maana Rais naye kalijibu kwa swali. Rais ndiye anazindua Bunge, Rais anasaini miswada kuwa Sheria, Rais anateua majaji, Rais anaweza kufuta hukumu ya mahakama yoyote.

..mtiririko uko hivi:

1. Bunge linapitisha sheria.

2.mahakama inatafsiri sheria hiyo, au inatoa hukumu.

3.serikali inatekeleza hukumu hiyo.

..Raisi anapotoa msamaha haimaanishi kwamba amefuta hukumu.

..mimi sijawahi kusikia mtu amehukumiwa halafu Raisi akataa kutekeleza hukumu hiyo na kuamuru mhusika asitumikie adhabu. Huko ndiyo kufuta hukumu kwa mtizamo wangu.

..hata mamlaka aliyonayo Raisi ya kutoa msamaha kwa wafungwa amepewa na sheria iliyopitishwa na bunge. Hili siyo suala ambalo Raisi anajiamulia tu kwa utashi wake.

..pia umezungumzia Raisi kuteua mahakimu na majaji. Sasa nikuulize: Mbona Raisi huapishwa ktk nafasi hiyo na Jaji Mkuu?

..Tukijenga dhana kwamba Raisi hana mipaka ktk madaraka yake tunaweza kuiingiza nchi ktk matatizo.
 
Kwakweli kauliza swali zuri japo halijajibiwa hata kidogo, eti mwenye chungu, mara fedha za bunge.....
Tatizo kifanya akili yako kutokua huru ni sbb ya kushindwa kumuelewa jpm.kuna vipengele vya katiba tulio wengi hatuvifaham mafuhum yake.naomba nipatiwe mfano wa hata nchi moja inayoongozwa na mahakama au bunge
 
Swali na Pasco na swali lililohusu maslahi ya waalimu (nahisi aliuliza Tido); huyo mwalimu wa zamani ameshindwa kuyajibu kwa ufasaha.
Waandishi wa nje wameonyesha ukomavu wa kuuliza mawasli ya msingi kwa kiasi kikubwa.
Kuna yule wa ssijui Mlimani nini vile alipiga blabla hata niaondoka zangu mbali ili nisimsikilize.
 
Mimi naona mkuu alifanya makusudi kabisa kutojibu swali kuhusu haki ya mikusanyiko kama inavyotolewa na katiba, na yeye amepata wapi mamlaka ya kuzuia mikutani ya siasa. Kwa bahati mbaya Tido na Ryoba wakalipotezea kwa makusudi ili mkuu asiadhirike.
Hakuwa na majibu
 
Back
Top Bottom