Hongera sana Pascal Mayalla, Ndio Mwandishi Pekee Uliyemuuliza Swali Rais Magufuli

Rais haapi utii kwa jaji bali anaapa utii kwa katiba.
 
[emoji122] [emoji122] [emoji122] Hongera Pascal ingawa raisi amekwepa kujibu kuhusu marufuku ya siasa,kwa maana nyingine umeuliza swali gumu mpaka Raisi imeshindwa kujibu [emoji106] [emoji106] [emoji106] [emoji122] [emoji122] [emoji122] [emoji122] [emoji122]
 
duu kuna koment za watu humu, nahisi lile somo la uraia walifeli kwa alama A.
 
Mi kilichonikera ni hao viongozi wa huo mdahalo Tido Mhando na Dr. Ryoba kwa ujumla wake wameuliza maswali 8 kati ya 20,Tido 5 Ryoba 3 na kwa mtazamo wangu hayakuwa na tija kivileeee,na mwanzoni mwa mdahalo Tido kasema kila mtu swali moja tu,sasa wao kwanini wameuliza mengi na kuwanyima wengine nafasi ya kuuliza? Kwakuwa wao ndo walikuwa waendeshaji? Au ni kamchezo kamefanyika kwamba waulize Mengi ambayo sio makali ili mda usogee wengine wasipate nafasi? Mi kwakweli wamenichefua na sijawaelewa!.
 
Yani wewe huishiwagi vioja tumeshakuzoea...
 
... Pascal alikuwa smart na amejibiwa vizuri swali la mihimili mitatu!
Vizuri? Kwamba kwa kuwa serikali ndio inayotoa hela basi inaweza kuipa maelekezo mihimili mingine? Serikali inatoa pesa, ni sawa. Lakini ni nani anayekusanya pesa? Si ni hiyo hiyo inayojinasibu kukusanya? Je, pesa ipo juu ya katiba na sheria za nchi?
 
Ana PhD alikuwa Mwalimu Alaf unasema hajui hata kiswahili? Tutake radhi mkuu
 
kwa mtazamo wangu hata Manyerere ukiondoa kulilia whisky kipande cha Msimamo wa Tanzania kuhusu SAHARA MAGHARIBI vs MOROCCO , na yule katibu mkuu wa MOAT Mr MUHANIKA pamoja na SAMMY AWAMMY maswali yao yalikuwa magumu kwa rais yalikuwa mazito
 
Jibu lake lilikuwa mtihani mno... mwelekeo wa jibu hatukutegemea
 
Ila Kajibiwa Kisiasa!
"Unajua Ni Kwanini Hotuba ya Kusitisha Mikutano na Shughuli za Kisiasa Bungeni?Mpiga Chakula na Mgawaji Ndie Ajuaye Chungu Kilivyo!Soma Katiba Ujue Katika Mihimili Yote Mitatu ni Upi Wenye Nguvu"

Moderators walikuwa wameandaliwa kulinda maslahi ya mkuu!
 
Vizuri? Kwamba kwa kuwa serikali ndio inayotoa hela basi inaweza kuipa maelekezo mihimili mingine? Serikali inatoa pesa, ni sawa. Lakini ni nani anayekusanya pesa? Si ni hiyo hiyo inayojinasibu kukusanya? Je, pesa ipo juu ya katiba na sheria za nchi?
Ina maana anatumia pesa kuvunja katiba ,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…