Hongera sana Pascal Mayalla, Ndio Mwandishi Pekee Uliyemuuliza Swali Rais Magufuli

Hongera sana Pascal Mayalla, Ndio Mwandishi Pekee Uliyemuuliza Swali Rais Magufuli

Ndugu yangu acha fikra zilizo lala wakati wewe ni muelewa. Kwa mitano hiyo, tunaona mawaziri na viongozi wengine wanaapa utii mbele ya Rais kwa vile ndio bosi wao. Sasa mbona na Rais anaapa utii mbele ya Jaji mkuu?
Ndio tunapokuja kwenye separation of power katika implementation ya majukumu ya uendeshaji.
Sii unajua kuwa hata bunge laweza kufukuza kazi Rais? Ni mambo tuu ambayo yapo katika katiba ili kuleta kuheshimiana
Rais haapi utii kwa jaji bali anaapa utii kwa katiba.
 
[emoji122] [emoji122] [emoji122] Hongera Pascal ingawa raisi amekwepa kujibu kuhusu marufuku ya siasa,kwa maana nyingine umeuliza swali gumu mpaka Raisi imeshindwa kujibu [emoji106] [emoji106] [emoji106] [emoji122] [emoji122] [emoji122] [emoji122] [emoji122]
 
duu kuna koment za watu humu, nahisi lile somo la uraia walifeli kwa alama A.
 
Mi kilichonikera ni hao viongozi wa huo mdahalo Tido Mhando na Dr. Ryoba kwa ujumla wake wameuliza maswali 8 kati ya 20,Tido 5 Ryoba 3 na kwa mtazamo wangu hayakuwa na tija kivileeee,na mwanzoni mwa mdahalo Tido kasema kila mtu swali moja tu,sasa wao kwanini wameuliza mengi na kuwanyima wengine nafasi ya kuuliza? Kwakuwa wao ndo walikuwa waendeshaji? Au ni kamchezo kamefanyika kwamba waulize Mengi ambayo sio makali ili mda usogee wengine wasipate nafasi? Mi kwakweli wamenichefua na sijawaelewa!.
 
Mayala alianza hotuba,kujifagilia na kutangaza kampuni yake na kujipigia debe la kutafuta fursa ikulu .Sehemu kubwa ya aliyonngea yalikuwa hasa ya kujinadi mnadani yeye binafsi.Kwangu naona kama aligeuza Ikulu na ile press conference kama gulio la kujinadi zaidi kuliko kuuliza swali.
Yani wewe huishiwagi vioja tumeshakuzoea...
 
... Pascal alikuwa smart na amejibiwa vizuri swali la mihimili mitatu!
Vizuri? Kwamba kwa kuwa serikali ndio inayotoa hela basi inaweza kuipa maelekezo mihimili mingine? Serikali inatoa pesa, ni sawa. Lakini ni nani anayekusanya pesa? Si ni hiyo hiyo inayojinasibu kukusanya? Je, pesa ipo juu ya katiba na sheria za nchi?
 
Ndiyo maana Luna msemo wa kama hujui bora unyamaze, huyu jamaa kabla hajawahi kuhojiwa na waandishi wengi tuliamini atakuwa vizuri upstairs ila mpaka hapa tumeishapata jibu kuwa ni mweupe. Halafu hawa wasiyojielewa waona kaweza.
Kwa waandishi wa Kimataifa hawezi kabisa, ukizingatia hata lugha yenyewe Kiswahili nacho kina Walakini. Sijui lugha gani yupo vizuri sasa, labda kisukuma.

Kabisa mkuu. Pamoja na Waandishi wengi wao walikuwa wakiuliza maswali yasiyo na tija na yasiyohitaji kufikiri bado kachemka vibaya. Kwa Upstairs kaprove failure kabisa. Sasa tumejua uwezo wake wa kujibu hoja. Internationally anaweza chemka vibaya, ukiangalia asivyojua lugha yoyote kiufasaha ndiyo shida maana inapunguza kujiamini.
Ana PhD alikuwa Mwalimu Alaf unasema hajui hata kiswahili? Tutake radhi mkuu
 
kwa mtazamo wangu hata Manyerere ukiondoa kulilia whisky kipande cha Msimamo wa Tanzania kuhusu SAHARA MAGHARIBI vs MOROCCO , na yule katibu mkuu wa MOAT Mr MUHANIKA pamoja na SAMMY AWAMMY maswali yao yalikuwa magumu kwa rais yalikuwa mazito
 
Jibu lake lilikuwa mtihani mno... mwelekeo wa jibu hatukutegemea
 
Ila Kajibiwa Kisiasa!
"Unajua Ni Kwanini Hotuba ya Kusitisha Mikutano na Shughuli za Kisiasa Bungeni?Mpiga Chakula na Mgawaji Ndie Ajuaye Chungu Kilivyo!Soma Katiba Ujue Katika Mihimili Yote Mitatu ni Upi Wenye Nguvu"
Hakika nimefurahishwa sana na Mwandishi huyu Pascal Mayalla wa kipekee aliyemuuliza swali Rais lenye msingi na hata rais kajibu kwa ubabaishaji. Natafuta clip au mwenye nayo aiweke.

Kwanza kaanza kwa kuitaja JamiiForums kwa kusema ni mwanachama mwandamizi wa JamiiForums.


Moderators walikuwa wameandaliwa kulinda maslahi ya mkuu!
 
Vizuri? Kwamba kwa kuwa serikali ndio inayotoa hela basi inaweza kuipa maelekezo mihimili mingine? Serikali inatoa pesa, ni sawa. Lakini ni nani anayekusanya pesa? Si ni hiyo hiyo inayojinasibu kukusanya? Je, pesa ipo juu ya katiba na sheria za nchi?
Ina maana anatumia pesa kuvunja katiba ,
 
Back
Top Bottom