Hongera sana Pascal Mayalla, Ndio Mwandishi Pekee Uliyemuuliza Swali Rais Magufuli

Nice words...
 
Kungekuwa na maswali ya kufikirisha Rais angeomba muda uishe haraka aondokane na waandishi lakini kwa udhaifu wa maswali yaliyosinyaa hata dakika mbili za mapumziko kazikataa na hata mwishoni kasema waendelee hata mpaka saa nane.

Loo wandishi wa Tanzania kweli waliishajichokea.
 
Naungana na wewe kutoa pongezi kwa paskali wa Jamiiforums.

Lakini kabla ya mkutano wa Rais na waandishi wq habari tuliaminishwa humu kuwa huo mkutano ni usanii tu maswali yameishapangwa.

Na haya maswali ya Paskali wa Jamiiforums yalikuwa yameishapangwa au?
 
Hata hivyo umempatia heshima kubwa sana kumjibu. Mimi nimempuuza huyo.
 
Na uccm wangu ila hapa mh. Presida kazurula mbaya...! Ingekuwa necta angeangukia pua yaani zero.([emoji778] %)
 
Pascal mayalla ameiwekea heshima nchi akumuogopa tembo uchwara
 
Swali kutoka kwa Mr. Mayala.
Mh. Rais uliapa kulinda katiba ya Jamhuri ya Muungano wa TZ, Je ulipata wapi mamlaka ya kuzuia mikutano ya siasa wakat katiba haikupi nafas ya kufanya hivyo?
Jibu....
Mayala kwa kisukuma ni njaa! Yawezekana ww Mayala ulizaliwa kipindi cha njaa! Wote wakacheka[emoji16], akaendelea....
Mh. Mayala uliwahi kujiuliza kwa nn hotuba yangu ya kwanza ya kubana matumizi niliitolea Bungeni Mbele ya Spika? Ukijua mpikaji wa chakula ni nan na mgawaji wa chakula ni nan bas utanielewa.

Hilo jibu la swali lililoulizwa , cjui kama ni vinaendana.
 
Swali la Pasco lilikuwa swali hasa ila wengine mhhhhhhhh.Hadi kilimo cha mihogo hilo si RC tu.
 
Mayala hakufanya follow up
Akaogopa kufuatilia swali
 
Paschal Wewe ni jembe,kwanini Tido kazingua? Rais hajajibu swali lolote pale
 
Rais kasema hivi ''Katika mihimili mitatu upo mmoja uliozama zaidi'' Ukielewa hilo hoja zako zote hapo juu zinakosa mashiko
 
Kajibu mihimili inalingana urefu ila mmoja umechimbiwa zaidi kwa kwenda chini, eleweni
 
ASANTE SANA MAYALLA HAKIKA UMEWEKA UNAFIKI PEMBENI NA KUSEMA AU KUULIZA SWALI LA MBOLEA TENA YENYE RUTUBA KWA WEREVU TUMEKUELEWA ILA KWA WEHU WATAKUWA HAWAJAKUELEWA NA DAIMA HAWATA KUELEWA KISA KUFIKIRI KWA KUTUMIA TUMBO BADALA YA KICHWA.
FUMBO MFUMBIE MJINGA MWEREVU ATALING'AMUA,UJUMBE UMEFIKA SAWIA BIN SAWIA AND THIS IS LIVE AND DIRECT.
BADO MTKUFU HAKUTOAA JIBU AME DIVERT QNS NA KUTOA MAJIBU ANAYOJISIKIA NA SIYO KAMA SWALI LILIVYOTAKA KUJIBIWA.
MUNGU AZIDI KUKULINDA KIJANA MAYALLA KWANI KILA MTU ATATOA HESABU YAKE SIKU ZA MWISHO,JE HAO WAANDISHI WANAFIKI NA MAKANJANJA AMBAO HAWAKUITENDEA HAKI TAALUMA ZAO KISA WOGA NA MASLAHI BINAFSI WATAMJIBU NINI MUUMBA WAO????
 
Separation of powers haina ukuu

Hapa tukubaliane tu kuwa dhana nzima hakuielewa, hilo halina mjadala

Kwamba mhimili unaotoa pesa ndio superior! serious!
 
Hodi hodi mwana wane naingia kupitia mlango wa nyuma..

Jamani kwanza mfahamu ya kwamba Katiba yetu imeandikwa kwa muundo gani kisha ndio tujenge hoja zetu kwa sababu NENO KUTOINGILIA halina maana kuweka USAWA wa KIMAMLAKA. Nachoelewa mimi ina maana kwamba mhimili mmoja hauwezi kuingilia shughuli za mhimili mwingine hivyo rais kama kiongozi wa Serikali ataifanya kazi yake ya shughuli za serikali pasipo kuingiliwa na Bunge ama Mahakama.

Mfano:- Bunge linalokaa na kujadili sheria ama kupitisha Muswada, rais na Mahakama hawana mamlaka ya kuingilia shughuli hiyo. Pia Mahakama inapofanya shughuli zake za kimahakama Rais na Bunge hawaruhusiwi kuingilia maamuzi ya Mahakama. Tofauti na Katiba ya Marekani ambayo Bunge na Mahakama zimeundwa ili kupunguza nguvu za kimamlaka (Power) ya rais na hivyo kwa kila shughuli za Serikali kuu vyombo hivyo vinahusika kwa njia moja ama nyingine (President Executive order or Proclamation)

Kwa wenzetu huwezi kuona mikataba ikiwekwa na nchi za nje pasipo Bunge au Mahakama kupitia, sisi majuzi tu Magufuli katangaza kughairisha sikuu za Uhuru na Muungano na ikawa. Tumeingia mikataba 21 na Morocco, ni mhimili gani umehusishwa? ama ni kifungu gani cha sheria kinachomkataza ama kusema Bunge linaweza kuingilia? Bila shaka sheria inasema wasiingilie sio waingilie. Sijui kaa nakosea lakini ndivyo nachoelewa mimi. Toka mikataba ya Buzwagi, Bulyanhulu hadi Richmond walihusishwa?

Leo hii ndio tumegundua kumbe hata mkataba wa India kuna mazao ambayo tunatakiwa kuzalisha nchini soko limeshapatikana India na fedha zipo mikononi mwetu, nani alijua hayo?. Labda nirudi nyuma kidogo, Magufuli alipopitisha Elimu bure hadi Sekondari lilijadiliwa lini bungeni? Kwa hiyo, kwetu sisi ilani yachama ikisha pita na wananchi kumchagua rais, kinachojadiliwa ni FEDHA TU. Wizara gani imepata kiasi gani na sio mambo gani yatafanyika.

Leo hii tumetangaziwa nchi ya Viwanda! Nini lengo la kuanzisha viwanda nchini ikiwa hatuna masoko nje? Je ni kukimu mahitaji yetu kwa nini wawekezaji watoke nje ama kuuza nje na kama nje tutauza vipi? tumejiandaa vipi kwa masoko nje ya EAC.inaonyesha wazi kwamba wananchi wengi walikuwa hawajui kinachoendelea, hata hao waandishi wa Habari. Kwa maana pana zaidi Bunge lipo pale kupitisha Bajeti tu ya serikali, nimeshangaa hata incentives zinazotolewa waandishi wa habari hawazijui wakaulize wapi vile!.
 
Rais kasema hivi ''Katika mihimili mitatu upo mmoja uliozama zaidi'' Ukielewa hilo hoja zako zote hapo juu zinakosa mashiko

Umezama zaidi kwenda wapi?

Kauli za kujitapa sio nzuri,hiyo kauli ni ya intimidation,sio sawa,itahamsha complexes kwa mihimili itakayojiona "midogo",yote ya nini?Ndio maana inatakiwa busara ya kiutu uzima.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…